Rais Magufuli atangaza ajira mpya 1500 Polisi, JKT wapewa kipaumbele
RAIS Dk.John Magufuli ametangaza nafasi 1500 za ajira mpya kwa Jeshi la Polisi nchini huku akitoa maelekezo, anataka vijana wa JKT ndio wapewe nafasi hizo na si kutafuta ndugu,jamaa na marafiki wa makamanda wa wilaya na mikoa. Amesema kuna tabia imejengeka pale inapotokea nafasi za ajira kwa ajili ya jeshi la polisi,baadhi ya makamanda wanatafuta watu wao na hivyo hata wakienda kwenye mafunzo wanapewa mafunzo kwa kuangalia waliowapeleka. Rais Magufuli ametoa tangazo hilo wakati anazungumza na wananchi wa Mkoa wa Arusha baada ya tukio la kuzindua nyumba npya za Polisi zilozojengwa kwa ushirikiano wa Serikali na wadau wa maendeleo wa mkoa huo.Ambapo ameagiza nyumba hizo wapewe askari wa vyeo vya chini. Amesema kutokana na kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Jeshi la Polisi nchini kwa kuhakikisha nchi inakuwa salama hivyo ameamua kutoa ajira mpya 1500 na kufafanua anataka kuona wanaopata ajira hiyo ni watoto wa masikini na si vinginevyo. "Na