Posts

Kitwanga: Ukiwa msema Ukweli lazima wakuondoe

Image
Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga amefunguka na kusema kuwa mtu ukiwa msema ukweli lazima wakuondoe katika nafasi yako kwa kuwa hawataki watu wasema kweli. Kitwanga amesema hayo bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019, mjini Dodoma na kudai hata ukiwa mtenda haki kwa kila mtu lazima wakuhamishe. "Kichwa changu na kichwa cha Jenista Mhagama ni vichwa viwili tofauti kabisaa na uwezo wetu wa kufikiri upo tofauti kabisaa, kwa hivyo ni vyema tukapima na kuhakikisha kwamba pale anapofaa Jenista Mhagama aende Jenista Mhagama, pale anapofaa Kitwanga aende Kitwanga lakini hii ya kubebe jumla jumla na wakati mwingine ndugu zetu hii tabia ife na mimi siwezi kukubaliana na hilo na bahati nzuri ukiwa msema ukweli hata ukikaa pazuri watakuondoa tu. Na ukiwa unatenda haki kwa kila mtu hata ukikaa Kolomije watakuondoa wakupeleke Mtwara" alisisitiza Kitwanga May 21, 201...

Jacob Zuma amefikishwa Mahakamani

Image
Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amefikishwa mahakamani leo katika mji wa Durban ili kujibu mashtaka ya rushwa, udanganyifu na kujitajirisha kinyume cha sheria. Kesi hii inasikilizwa kwa mara ya kwanza na inahusu biashara ya zamani ya mauzo ya silaha tangu miaka ya 1990.  Rais wa zamani wa Afrika Kusini anashutumiwa kupokea rushwa kutoka kwa Thomson CSF – jina la zamani la kampuni ya Thales – katika mpango wa mkataba wa mauzo ya silaha wenye thamani ya karibu Euro Bilioni 4 ulioafikiwa mnamo mwaka 1999. Wakati huo, Jacob Zuma alikua makamu wa rais wa nchi ya Afrika Kusini. Anashutumiwa kuwa alipokea jumla ya euro milioni 50 kutoka kampuni ya Ufaransa ya Thales. Kwa upande mwingine, aliahidi kupatishia zabuni kampuni hiyo ya Thales. Kwa jumla, Afrika Kusini iliamua kutumia zaidi ya dola bilioni 10 kurejelea upya silaha zake. Silaha ambazo nchi hiyo haikuweza kuzihitaji wakati huo na a...

Rais wa zamani wa Korea Kusini amehukumiwa miaka 24 jela

Image
Rais wa zamani wa Korea Kusini  Park Geun-hye, amehukumiwa miaka 24 jela baada ya kukutwa na hatia katika matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha nchi kushuka kiuchumi. Park Geun-hye aliondolewa madarakani mwaka jana baada ya kutuhumiwa kutumia vibaya wadhifa wake na kusababisha kuanguka kwa uchumi. Rafiki yake Choi Soon-sil, anayehusishwa na kashfa hiyo, alihukumiwa wiki mbili zilizopita hadi miaka 20 jela kwa kupokea hongo iliyotolewa na makampuni ya Korea Kusini, ikiwa ni pamoja na makampuni yai Samsung na Lotte. Katika mashtaka yake, mwendesha mashtaka alimshtaki rais wa zamani kuwa “alisababisha mgogoro wa kitaifa kwa kuacha mtu ambaye hajawahi kushiriki katika usimamizi wa umma kuongoza nchi”. Kesi ya rais wa zamani Korea Kusini ilifunguliwa mwezi Mei mwaka jana. Mahakam inatarajia kutoa uamuzi wake kabla ya mwezi April mwaka huu.

Rais Magufuli atoa Shilingi milioni 100 kumtibu Mgunduzi wa Tanzanite

Image
Leo April 6, 2018 Rais John Magufuli katika Uzinduzi wa Ukuta wa Mirerani amesema serikali yake itatoa kiasi cha Shilingi milioni 100 kwa ajili ya matibabu ya Mzee Jumanne Ngoma ambaye ndiye mgunduzi wa madini ya Tanzanite . Rais Magufuli ameeleza kuwa serikali inatoa pesa hiyo ili Mzee Ngoma ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kupooza akapatiwe tiba kwani ugunduzi wake ndio ulioweka historia ya nchi ya Tanzania kumiliki madini hayo. Takriban mwezi mmoja uliopita Mzee Ngoma alifanyiwa mahojiano na Ayo TV na millardayo.com na kueleza kuwa anatamani kuonana na Rais Magufuli ili amueleze adha anayokutana nayo na jinsi ambavyo kuona hathaminiwi wala kunufaika na chochote licha ya ugunduzi alioufanya. Mzee Ngoma anadaiwa kugundua madini hayo miaka 52 iliyopita .

Cecilia Pareso aseama kama mnataka futeni yu Vyama vya Upinzani

Image
Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Cecilia Pareso amesema kama serikali ina lengo la kuwabana na kuwanyima haki wapinzani, basi ni bora mfumo wa vyama vingi ukafutwa ili ifahamike kwamba nchi ni ya chama kimoja. Pareso ameyasema hayo jana Aprili 5, Bungeni Mjini Dodoma wakati akichangia katika Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2018/19 huku akidai kwamba vyama vya upinzani vimekuwa vikionewa ikiwemo viongozi wake kukamatwa mara kwa mara na kufunguliwa mashtaka huku wengine wakifungwa jela. Amesema vyama hivyo vimekuwa ni adui mwingine kwa kuwa kwa sasa vinapigwa vita na Serikali iliyopo madarakani, kuzuiwa kufanya shughuli za siasa majukwaani. Pia alidai chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni, zilikuwa ni kati ya Chadema na Jeshi la Polisi na kudai kwamba wabunge na madiwani walinunuliwa, wakahama vyama vyao, hivyo kukalazimika kufanyika chaguzi nyingine ndogo alizodai zimegharimu zaidi ya Sh bilioni 6. “Kama mnakataza vyama vya siasa visif...

Breaking News: Wambura Ashindwa Rufaa Yake, Ataendelea na Kifungo

Image
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura. Kamati Ya Rufaa Maadili Ya TFF baada ya kupitia rufaa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo,Michael Richard Wambura imetupilia madai yake yote na adhabu yake itaendelea kama ilivyoamuliwa na  Kamati ya Maadili ya TFF kwa kufungia kutojihusisha na soka maisha yake yote. Mbali na hilo pia kamati hiyo ya rufaa imeshauri, Wambura afikishwe kwenye vyombo vya dola ili suala hilo liweze kushughulikiwa zaidi na wataalam

Mtanzania Mahakamani Uingereza Akidaiwa Kumuua Mkewe

Image
Raia wa Tanzania Kema Salum. RAIA wa Tanzania Kema Salum (38) amefikishwa mahakamani nchini Uingereza akidaiwa kumuua mkewe, Mtanzania pia, aitwaye Leyla Mtumwa. Salum anayedaiwa kumchoma visu Leyla na kumuua wakiwa nyumbani kwao mtaa wa Kirkstall, Haringey, nchini humo Ijumaa iliyopita, amefikishwa katika mahakama ya Crown. Marehemu Leyla Mtumwa. Kutokana na mgomo wa wanasheria nchini humo tangu kuanza kwa mwezi Aprili, kesi hiyo haikusikilizwa na Jaji Anuja Dhir ameahirisha usikilizwaji wake hadi Juni 20 mwaka huu. Kwa mujibu wa mwanasheria Seona White, juhudi zinafanyika ili kupata wakili wa kumtetea Salum mahakamani licha ya mgomo wa mawakili unaoendelea. Mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka yake kwa Kiingereza lakini kupitia mkalimani aliyemwelewesha kwa Kiswahili. Mipango inafanywa kumleta marehemu nchini Tanzania.

JPM Awalilia 12 Waliokufa Ajalini Tabora, Ataka Polisi Kujitathmini

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 12 vilivyotokea katika ajali ya basi kugongana na lori Kijiji cha Makomero, Wilaya Igunga mkoani Taborausiku wa kuamkia leo.

Hatma ya Nabii Tito aprili 13

Image
KESI  inayomkabili Tito Machibya maarufu Nabii Tito, hatma yake kujulikana Aprili 13 mwaka huu baada ya mahakama ya Wilaya ya Dodoma kupokea taarifa za kitabibu jana asubuhi. Mahakama ya Wilaya ya Dodoma jana ilipokea taarifa ya vipimo vya kitabibu vya Tito Machibya, ilivyokuwa imeviagiza hapo awali na kumtaka afanyiwe vipimo katika Taasisi ya magonjwa ya akili ya Isanga mjini Dodoma. Jana Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha alisema mahakamani hapo kuwa alipokea taarifa ya kitabibu kuhusu Nabii Tito kutoka Taasisi ya Isanga hivyo ataipitia na kutoa maamuzi siku hiyo ya Aprili 13. “Nieleze kuwa nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa huyu leo asubuhi hivyo nitaipitia ili April 13 mwaka huu siku ya Ijumaa niweze kuitolea maamuzi,” alisema Karayemaha. Hata hivyo Nabii Tito jana aliweza kuhudhuria mahakamani akitokea mahabusu ya gereza kuu la Isanga baada ya kutofikishwa mahakamani  hapo  mara mbili mfululi...

Mbasha afunguka ishu ya kumpa mimba Agness

Image
Msanii wa nyimbo za Injili nchini, Emmanuel Mbasha amesema amesikitishwa na taarifa alizozipata kuwa amempa ujauzito msichana anayevuma kwenye mitandao ya kijamii Agness na kudai hana mahusiano yeyote na mtu huyo zaidi ya kumfahamu kupitia mitandaoni. Mbasha amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana baada ya kuwepo na tetesi za muda mrefu zinazozidi kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa zinadai kuwa wawili hao wana mahusiano ya kimapenzi na mpaka kufikia hatua ya kukubalia kupeana ujauzito. "Agness mimi namfahamu kama shabiki yangu kupitia mitandao ya kijamii. Sasa sielewi mambo yamegeuka vipi mpaka kufikia hatua ya kuambiwa mimi nina mahusiano naye. Sijawahi kuwa na mahusiano na Agness na wala sijawahi kuwa na chochote kile kinachoashiria mapenzi", amesema Mbasha. Pamoja na hayo, Mbasa ameendelea kwa kusema "sitegemei kupata naye mtot...

Ndugai: Bashe Apeleke Hoja Yake Kwenye Chama Kabla ya Bungeni

Image
Bashe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai amesema suala la Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe kutoa hoja binafsi bungeni, alitakiwa kuipeleka kwenye chama chake kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya kuipeleka bungeni. Ndugai amesema hayo ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kutoka India alikokuwa akipatiwa matibabu. Amesema Kanuni za Bunge zipo na Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Bunge kwa wabunge wa CCM kama chama tawala na zipo, kama kwa wabunge wa kambi ya upinzani ambazo zote ni sehemu ya uendeshaji wa shughuli za Bunge. Ndugai. Amesema Bashe kama mbunge wa CCM, kanuni za wabunge wa CCM zinamtaka aipeleke hoja yake kwenye chama chake kwanza, ikajadiliwe huko na ikikubaliwa Bunge liweze kuipokea. Amesema Bunge bado halijapokea hoja hiyo kutoka kwa Bashe, pia halijapokea taarifa kutoka kwa katibu wa wabunge wa CCM kama wameipokea hoja hiyo na wameshaurianaje. Mwezi uliopita, Bashe alisema amemuandikia barua...

Watu wanne wadakwa kwa tuhuma za wizi katika Ujenzi wa reli ya kisasa

Image
Watu wanne wanashikiliwa na Polisi Ngerengere, Mkoani Morogoro wakituhumiwa kuhusika na wizi wa lita 2510 za mafuta aina ya Dizeli kutoka kambi ya ujenzi wa reli ya kisasa Standard Geuge. Watuhumiwa hao wamekamatwa na polisi kikosi maalumu cha reli nchini kwa kushirikiana na maafisa wa shirika la reli Tanzania ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika. Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Kikosi Maalumu cha Reli Salum Kisai, amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao itakuwa fundisho kwa watanzania wengine wanaofanya kazi katika mradi huo ili kuweza kulinda mali za mkandarasi na kumaliza kwa mradi huo kwa muda unaotakiwa. Kwa upande wake Afisa wa shirika la Reli nchini TRC Catherine Mushi, amesema wananchi wanapaswa kushiriki katika kulinda miundo mbinu ya reli hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza uaminifu kwa wawekezaji nchini kuweza kutoa ajira zaidi kwa watanzania.

Breaking News: Winnie Mandela afariki dunia

Image
Winnie Mandela, mke wa zamani wa Nelson Mandela, ambaye pia alipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini amefariki dunia akiwa na miaka 81. Habari za kifo chake zimethibitishwa na msaidizi wake. Winnie alizaliwa mnamo 26 Oktoba mwaka 1936, na ingawa yeye na mumewe - Nelson Mandela - walitalikiana mapema miaka ya 1990, Winnie Madikizela Mandela kama alivyofahamika rasmi alisalia kutoa mchango katika maisha ya Bw Mandela. Alikuwepo na walishikana mikono alipokuwa akiondoka gerezani baada ya kufungwa kwa miaka 27. Lakini maisha yake pia yalikumbwa na utata. Winnie alikuwa na miaka 20 hivi pale alipojipata katika siasa. Alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa. Kujitolea kwakena ukakamavu wake vilionekana mumewe alipofungwa jela maisha mwaka 1964 na akaachwa kuendeleza harakati za kisiasa. "Kamwe sitakata tamaa na watu wangu hawatapoteza matumaini kamwe, bila shaka tunatarajia kwamba kazi...

WAZIRI MKUU AZINDUA MBIO ZA MWENGE MKOANI GEITA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana sita watakaokimbiza Mwenge huo, Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwansha Mwenge wa Uhuru kuzindua mbio zake kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018

Sababu Za Kuwashwa Baada Ya Kuoga

Image
      “Wataalamu wa afya ya ngozi pia wanabainisha kuwa kuoga muda mrefu na mara kwa mara, matumizi ya sabuni zenye harufu kali na povu jingi ni mambo mengine yanayochangia kutokea kwa mzio pamoja na ukavu wa ngozi kutokana na uwezo wake wa kuondosha kiasi kikubwa cha mafuta yanayolinda ngozi. Ili kupunguza hali ya muwasho, “Tumia sabuni zenye mafuta, lakini zisiwe na marashi makali.” Katika hali ya kawaida kitendo cha kuoga kinapaswa kuchukuliwa kama jambo la kufurahisha kutokana na ukweli kwamba huufanya mwili uburudike na kuwa safi. Lakini kwa baadhi ya watu mambo ni tofauti. Kuoga huwa sawa na karaha. Moja ya matatizo ya kiafya ambayo yanayosumbua watu wengi duniani na kuwanyima raha ya maisha, ni tatizo la mwili kuwasha mara baada ya kuoga. Muwasho baada ya kuoga unaweza kujitokeza mwili mzima au unaweza kuhusisha baadhi ya sehemu. Hali hii inaweza kuwa inajitokeza kwa muda wa dakika chache au inaweza kuchukua muda mrefu na kwa baadhi ya watu, h...

Sakata la Wambura lafikia Patamu

Image
RUFAA ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura, sasa imefikia patamu baada ya juzi Jumamosi kusikilizwa katika makao makuu ya shirikisho hilo, Karume jijini Dar es Salaam na hivi sasa watu wengi wanataka kujua nini kinachofuatia. Hivi karibuni, Wambura alikata rufaa Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF kupinga maamuzi ya Kamati ya Maadili ya shirikisho hilo ya kumfungia maisha kujihusisha na soka kwa madai ya kufanya ubadhirifu wa fedha za shirikisho hilo pamoja na makosa mengine. Wakili wa Wambura, Emmanuel Muga, ameliambia C hampioni Jumatatu kuwa, kamati hiyo iliziita pande mbili zote zinazochuana katika sakata hilo na kuzisikiliza kwa umakini mkubwa. Alisema katika kikao hicho, mambo yalienda vizuri, kwa hiyo kinachosubiriwa tu hivi sasa ni maamuzi ya hiyo kamati. “Kamati imesikiliza kwa umakini utetezi wa Wambura, vilevile TFF nao wakizungumza ya kwao kuhusiana na mustakabali mzima wa kesi hiyo. Kwa hiyo tun...

Mamba akutwa katika bwawa la kuogelea Florida, Marekani

Image
Polisi katika jimbo la Florida, Marekani wamesema mamba wa urefu wa futi 11 alipatikana kwenye bwawa la kuogelea la familia moja katika jumba hilo. Polisi wamepakia picha za mamba huyo mtandaoni, Wakazi wa Nokomis waliwapigia simu polisi na kuomba usaidizi baada ya kumgundua mnyama huyo. Afisa wa polisi wa eneo la Sarasota alipakia mtandaoni picha ya afisa wa wanyama aliyeitwa kumnasa akiwa anamburuta mnyama huyo kutoka kwenye maji Jumamosi. Polisi wanasema mamba huyo alifanikiwa kupita kwenye uzio uliokuwepo na kuingia kwenye bwawa hilo, Mamba nchini Marekani kwa kawaida hukua hadi kuwa na futi kati ya 11 na 15 na wanaweza kuwa na uzani wa kilo 454. Mamba wa Marekani hupatikana mashariki mwa Marekani katika majimbo ya Florida na Louisiana, kila jimbo likiwa na zaidi ya mamba milioni moja. Eneo la kusini mwa Florida ndilo pekee ambalo mamba wa Marekani na mamba wa kawaida huishi kwa pamoja. Ingawa awali walikuwa wameorodheshwa kama wanyama walio hatari...

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo

Image
Bonyeza links zifuatazo Kusoma zaidi na Kuapply: 200+ Vacancies in Public and Private institutions in Tanzania, March 2018 Job Opportunity at the US Embassy Tanzania: Chauffeur Job Vacancy at Save the Children Tanzania - FINANCE ASSISTANCE Job Opportunity at UN Organization - Consultancy Process Expert Volunteer Job Opportunity at UN Organization - Marketing & Promotional Materials Expert Volunteer Job Opportunity at UNHCR - Registration Officer Job Opportunity at a Reputable NGO - Consultant to Conduct Assessment of BEST-Dialogue Support to Print Media Job Opportunity at Plan International Tanzania Nafasi zingine ingia  www.ajirayako.co.tz

Gabo, Wema na Kitale walivyoshinda tuzo za SZIFF April 1

Image
Usiku wa April 1 2018 Mlimani City Dar es Salaam zilifanyika tuzo za Sinema Zetu International Film Festival SZIFF na kuhudhuriwa na mastaa na watu mbalimbali kutoka tasnia tofauti tofauti. Rais mstaafu wa awamu ya nne Dr Jakaya Mrisho Kikwete ndio alikuwa mgeni rasmi na alishuhudia tuzo 19 zikitolewa kwa wasanii wa filamu, watayarishaji, wahariri na wabunifu wa sound track za movie hiyo. Miongoni mwa mastaa wa filamu waliyofanikiwa kushinda tuzo hizo ni pamoja na muigizaji Wema Sepetu aliyeshinda tuzo mbili za Best Actress na People’s Choice Award na Gabo ambaye ameshinda tuzo ya Best Actor huku Kitale akishinda tuzo ya Best Comedian. Alichozungumza Wema Sepetu baada ya ushindi wa tuzo ya Best Actres s

Aamka na kukuta Jeneza Nje ya Nyumba!

Image
MBEYA:  NELSON Edson, mkazi wa Mtaa wa Nsalaga Kata ya Nsalaga jijini hapa amejikuta kwenye taharuki kubwa baada ya kuamka na kukuta jeneza tupu dogo nje ya mlango wa nyumba yake. Tukio hilo lililoibua hekaheka mtaani hapo lilijiri asubuhi ya Machi 27, mwaka huu. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Nsalaga, Paul Ngonde, alipokea taarifa kutoka kwa Edson na kuamua kwenda eneo la tukio ili kushuhudia. Alisema kuwa, baada ya kuwashirikisha wazee wa mila juu ya jambo hilo, walilifungua jeneza hilo na kukuta likiwa tupu, lakini likiwa na sanda nyeupe iliyoviringishwa ndani yake. “Nimeshangaa asubuhi kuamka na kukuta jeneza nje ya mlango wa nyumba yangu, sijaelewa ni nini madhumuni ya kuwekewa jeneza hilo,” alisema Edson huku akionesha kustaajabishwa na tukio hilo. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, mtaa huo umekuwa na matukio ya ajabuajabu yakiwemo ya kutupa watoto, lakini tukio hilo la jeneza limekuwa ni tukio la kwanza kutokea mtaani kwake.   Kwa upande wake, Kam...