Fangasi Sehemu za Siri za Mwanaume
Watu wengi wanaamini kuwashwa sehemu za siri kunasababishwa na fangasi tu, ndiyo maana nimepata maswali ya wasomaji juu ya matibabu na jinsi ya kujikinga na fangasi kwa kuwa wanaamini muwasho unaowasumbua kwa muda mrefu ni matokeo ya maambukizi ya fangasi. Watu wanapaswa kufahamu kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani ndani ya mwili wako pengine isiwe ni fangasi na ikawa ni mzio (allergy) tu. Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe kitu hicho kikiondolewa. Kuondolewa kwa kitu hicho kunatia ndani matibabu sahihi na kuendelea na njia bora za kujikinga kutopata maambukizi tena. Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi. Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari. Kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu kunaweza sababisha ugonjwa kusambaa mwilini na kuongeza hatari ya kifo. Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri za Mwanaume? Kuwashwa uume au sehemu zingine za s