Hivi Ndivyo Vitu Hatari Vinavyoweza Kuharibu Na Kuvunja Ndoa Ya Wapendanao Katika Familia
WAPENZI wanagombana, ndoa zinavunjika na familia nyingi zipo kwenye msoto kwa sababu ya ubinafsi. Tunazungumza mengi lakini ukweli ni kwamba endapo kila mmoja atafanikiwa kuushinda ubinafasi, upendo utashamiri kila kona. Ubinafsi una matawi mengi. Mtu anaposaliti, maana yake ametekwa na tamaa binafsi. Anashindwa kutambua kwamba yeye ni mpenzi wa mtu, kwa hiyo anatakiwa kulinda penzi la mwenzake. Hajui kama anachokifanya ni dhuluma ya hali ya juu. Ukweli ni kwamba unapoanzisha uhusiano na mtu, maana yake umeamua kumchagua yeye ndiye amiliki penzi lako. Kwa hiyo ukienda kulitoa kwa mwingine, huo ni ubinafsi. Umeingiwa na umimi kwa kuona kwamba unatoa rasilimali za ndani ya mwili wako mwenyewe. Kwa nini ukimfumania mwenzi wako panachimbika? Ni kwa sababu alichokitoa kwa mtu mwingine ni chako, kwa maana hiyo amekutendea dhuluma. Ndiyo maana ukawa na jeuri ya kupigana kwa sababu haki yako imetumika ndivyo sivyo. Hivyo basi, usaliti ni ubinafsi. Umei