Posts

TAMISEMI Yaagiza Shule Ichunguzwe Baada ya Wanafunzi Wote Kupata 0

Image
WIZARA ya Ofisi ya Rais –Tamisemi kupitia kwa Naibu Wairi wake, Joseph Kakunda imemuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Njombe kuchunguza matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Viziwi Njombe. Akiji alipojibu swali la mbunge wa Buyungu (Chadema), Samson Bilago, bungeni leo Jumatano Januari 31,2018, Kakunda  amesema katika matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), shule hiyo katika matokeo ya mtihani uliofanyika Oktoba na Novemba mwaka jana watahiniwa wote 21 wamepata daraja sifuri (0) yaani wamefeli. Bilago alitaka kujua ni kwa nini shule za wanafunzi wenye mahitaji maalumu zinafanya vibaya kwenye mitihani, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema walimu waliosoma elimu maalumu watapata ajira bila kikwazo cha kusubiri huku akieleza kuwa anasubiri kupelekewa orodha ya walimu hao.

AIBU YA MWAKA..! WANASWA LIVE WAKIFANYA UFUSKA KAZINI!

Image
Baada ya kunaswa. NI aibu kubwa! Tangu kuanza kwa mwaka 2018, yapo yaliyotokea na kusisimua, lakini hili la mrembo kunaswa na mwanaume wakifanya ufuska kwenye eneo la kazi, limeibua hisia za aina yake kuwa huenda maisha hayaendi, Ijumaa Wikienda linaifumua. Habari kamili, tukio hilo lilijiri kwenye eneo la kazi la mrembo huyo ambalo ni saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini yeye akadaiwa kucheza mchezo wake wa ngono. Saluni hiyo ipo maeneo ya Sinza-Kwaremy jijini Dar ambapo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikidaiwa kujihusisha na uchafu huo na kusababisha kero kwa wananchi wenye maadili yao. …Akiwa uchi baada ya kunaswa. OFM KAZINI Kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, kikiwa kimetulia ndani ya mjengo wa makao yake makuu, Sinza-Mori jijini Dar, kilipokea simu kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi  wa saluni hiyo akimshitakia mwenzake kuwa amekuwa akijihusisha na ufuska na wanaume mbalimbali wakiwemo waume ...

JPM Amjulia Hali Mzee Majuto Hospitalini, Afunguka Alivyomtabiria Makubwa

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtembelea muigizaji mkongwe, Mzee Majuto katika hospitali ya Tumaini jijini Dar es salaam ambako amelazwa akitibiwa. Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Rais, Mzee Majuto amefunguka na kudai yeye ndio mtu wa kwanza kutabiri ujio wa Rais Magufuli katika kuongoza nchi ya Tanzania huku akisisitiza kwamba anajisikia faraja kuona ana misimamo iliyokuwa imara. “Mimi ndiyo mtu wa kwanza kumtabiri kwamba akiwa Rais itakuwa shughuli. Nilishukuru sana kuchaguliwa huyu bwana, tumepata Rais sio masihara watu wote sasa hivi wana adabu zao wanajua nini maana ya kazi”, alisema Majuto. Pamoja na hayo, Mzee Majuto aliendelea kwa kusema “sisi wazee tunafarijika sasa hivi, viwanda kila kona vimetapakaa na leo amekuja kutembea hospitalini hapa sijui kama wengine hawajikojolea huko kwa uoga maana hataki masihara. Hii ndio raha ya kupata viongozi wenye msimamo”. Kwa up...

Mbunge na Mwanasheria Aliyemwapisha Odinga Atiwa Mbaroni

Image
Mwanasheria TJ Kajwang’ (kushoto) na Mbunge Miguna Miguna wakati wa kumuapisha Odinda. JESHI la Polisi nchini Kenya, leo Januari 31, 2018 mchana limemtia mbaroni mbunge wa Jimbo la Ruaraka, Tom J Kajwang’, ambaye alisimamia “kuapishwa” kwa kiongozi wa muungano wa Nasa Raila Odinga kwenye viwanja vya Uhuru Park jana Jumanne. Kajwang amekamatwa na maofisa hao waliokuwa wamevalia kiraia nje ya Mahakama ya Milimani jijini Nairobi muda mfupi baada ya kuhudhuria katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji George Odunga kusikiliza uamuzi wa kesi aliyowawakilisha wabunge wanaopinga kukatwa mishahara yao na posho nchini humo. Kajwang’ na mwanasheria mwingine Miguna Miguna, ndiyo walisimamia matukio yote ya “kuapishwa” Odinga kama ‘rais wa watu’ katika viwanja vya Uhuru Park. Imeelezwa kuwa, Kajwang’ alikuwa amevaa vazi na wigi ambapo alishangiliwa sana na wafuasi wa Nasa wakati Odinga akila “kiapo”.

WEMA SEPETU TENA,CHUCHU AELEZA KUHUSU WEMA KUPATA MTOTO HUKU KUKIWA NA TETESI NA KUWA NA MIMBA

Image
Baada ya baadhi ya mashabiki kumtolea maneno yasiyofaa Wema Sepetu pindi alipoweka picha ya mtoto na Chuchu Hansy katika mtandao wa Instagram, muigizaji huyo amesema Wema hapaswi kuumizwa na hilo kwani utafika wakati wake atapata mtoto. Chuchu Hans ameiambia E-Newz ya EATV kuwa Wema ni rafiki yake na mara kadhaa wao kama wanawake wamekuwa wakiongea na kumshauri na kumtia Moyo. “Nilishamuambia wewe (Wema) utakuja kupata mtoto il sio pale unapohitaji wewe, ni pale ambapo Mungu amekuandikia muda wako ukifika, kwa hiyo hayo maneno wala asimuumie ni changamoto na kutokana na ustaa alionao,” amesema. Mtoto wa Chuchu Hansi anaitwa ambaye amezaa na muigizaji mwenzake, Ray Kigosi.

ANGALIA MPELELEZI ALIYEPOTEZA MIKONO, MIGUU NA UTUMBO,SASA KULIPWA BIL 245

Image
OFISA wa ujasusi (shushushu) katika jeshi la Marekani, Lisa Maria Carter, wa Florida, Marekani, anajitayarisha kulipwa Sh. bilioni 245 (Dola milioni 109 za Marekani) kutokana na kufanyiwa vibaya oparesheni ya kutibu uvimbe uliokuwa umejitokeza katika sehemu ya uzazi mwaka 2010. Lisa Maria Carter alivyo sasa. Hivi sasa, Carter anabidi ahudumiwe kila kitu kutokana na athari aliyopata kutokana na oparesheni hiyo. Mwaka huo, mwanamke huyo akiwa na umri wa miaka 45, alikuwa aondoke kwa ndege kwenda Iraq kukusanya habari za ujasusi ambapo aliambiwa alikuwa na uvimbe kwenye sehemu ya uzazi (ovarian cyst). …Anavyotembea kwa kutumia nyenzo maalum Katika oparesheni iliyofuata ya kumtibu, ambayo ilifanyika vibaya, ilisababisha apoteze mikono yake yote, miguu, utumbo na misuli ya tumbo. Hii ilitokana na kumsababishia kukumbwa na bacteria zilizoula mwili wake na kuharibu sehemu mbalimbali. …Akiwa na mtaalam wa tiba Katika upasuaji huo, shinikizo lake la damu lilishuka s...

Ikulu: Rais Magufuli Akutana na Maafisa Wakuu wa JWTZ

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo kabla hajaanza kuwatambulisha Maafisa Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (hawaonekani pichani) ambao wanatarajia kustaafu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ambaye aliambatana na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao wanatarajiwa kustaafu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaotarajiwa kustaafu ambao ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibolwa wanne kutoka (kulia), Meja Jenerali Michael...

Bunge kuunguruma kesho, wabunge watatu kuapishwa

Image
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza kunguruma kesho (Jumanne) na Mkoani Dodoma kwa kuanza kuapisha Wabunge wapya watatu pamoja na kupitisha miswada miwili ya sheria ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tisa. Hayo yamewekwa wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi za Bunge kupitia Kitengo cha Habari na Mawasiliano na kusema kuwataja wabunge hao ambao watakula kiapo cha uaminifu kuwa ni Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kutokea Songea Mjini, Mhe. Monko Justine Joseph wa Singida Kaskazini na kumaliziwa na Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa wa Longido. Aidha, katika mkutano huo wa 10 kutakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na Wabunge huku wastani wa maswali 16 ya kiwa ya papo kwa hapo kuenda kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo yanatarajiwa kuulizwa siku ya Alhamisi mnamo februari mosi. Kwa upande mwingine, Kamati 16 za Bunge za kudumu ...

Lita 85 za Gongo zakamatwa Manyara

Image
Jeshi la Polisi mkoani Manyara limesema limekamata mitambo ya kutengenezea pombe haramu ya gongo pamoja na lita 85 za pombe hiyo, ambayo ni kinyume na sheria za nchi. Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga, amesema vifaa hivyo pamoja na pombe imekamatwa kutokana na operesheni maalum inayoendeshwa na jeshi hilo. “Mkoa wetu wa Manyara umeendelea na misako mbali mbali ambapo tumekamata mitambo ya gongo pamoja na gongo huko mbulu, kijiji cha hydom Manyara, walimkata mtu mmoja Moshi Bula mwenye miaka 55, akiwa na mitambo minne ya kutengenezea mitambo ya gongo, hivi sasa yupo mahabusu na taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani,”, amesema Kamanda Senga. Kamanda Senga ameendelea kuelezea kwamba...Sambamba na hilo tumekamata lita 65 za pombe haramu ya moshi pamoja na watu watatu wanaohusika na pombe hiyo, ambao ni Neema Doto Matayo, mwenye miaka 21, Law...

Sumaye: wanaojiuzulu nafasi zao hawatambui majukumu yao

Image
picha ya mtandao Waziri Mkuu Mstaafu , Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa kazi ya Mbunge ni kutetea wananchi wa jimbo lake na si kwenda kumsifia Rais na kudai wabunge waliojizulu nafasi zao kwa kigezo cha kumuunga mkono Rais hawakutambua majukumu yao. Sumaye amesema hayo kwenye kampeni za Ubunge wa marudio katika jimbo la Kinondoni zinazoendelea na kusema kuwa kwa Wabunge ambao wamejiuzulu nafasi zao na kwenda chama kingine kugombea tena hawafai kabisa kuwa wabunge kwa kuwa hawatambui maana ya Ubunge. "Kazi ya Mbunge si kwenda kumtetea Rais bali ni kutetea wananchi waliompa kura, kama Mtulia yeye anasema ameondoka na kudharau kura za watu wa Kinondoni kwa sababu amependezeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi akateuliwe na Rais kuwa Mbunge maana kazi yake ndiyo itakuwa kwenda kumtetea na kumsifia Rais. Watu ambao wanahama chama eti kwa sababu Rais ametenda mambo mema pamoja na ukweli kwamba mimi naweza kubishana sana maana hatujaona ...

Nabii Tito Apandishwa Mahakamani, Anyimwa Dhamana

Image
Onesmo Machibya almaarufu Nabii Tito aliyetengeneza vichwa vya habari kutokana na mahubiri yake ya kuhimiza ulevi na uasherati, amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, na kusomewa mashtaka ya kujaribu kujiua. Nabii Tito alifanya jaribio la kujiua Januari 25, mwaka huu akiwa mahabusu, ambapo inadaiwa kwamba alijikatakata na wembe kwa lengo la kuyakatisha maisha yake. Alipotakiwa kujibu mashtaka yanayomkabili, Nabii Tito awali alisema hakumbuki chochote kwa sababu yeye ni mgonjwa wa akili, lakini alipobanwa kwa mara nyingine, alisema ni kweli alitaka kujiua kwa sababu kuna sauti ndani ya kichwa chake iliyokuwa inamuelekeza kufanya kitendo hicho. Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Nabii Tito amerejeshwa rumande huku akiwekewa mapingamizi saba ya dhamana.

Matukio kwa Picha na Video Utambulisho wa Mbosso WCB

Image
WCB wakiwa katika picha ya pamoja, katikati ni msanii wao mpya, Mbosso. BURUDANI ya aina yake imepigwa na wasanii wa Lebo ya WCB usiku wa kuamikia leo wakati kumtambulisha msanii mpya katika kundi hilo, Mbosso ambaye awali alikuwa Yamoto Band kabla ya kundi hilo kuvunjika. Mbosso, Diamond na Rayvanny wakikamua. WCB ikiongozwa na Lejendari, Diamond Platnumz, wamemtambulisha huyo katika Ukumbi wa Hyatt Legency Hotel jijini dar es Salaam na kuhudhuriwa na mastaa kibao wakiwemo, Wema Sepetu na wengine pamoja na wanahabari. Diamond akimsalimia mama yake, Bi Sanura ukumbini hapo. WCB na mashabiki waki-enyoj event. WCB na mashabiki katika picha ya pamoja.   Diamond akikata mauno.

Dk Slaa, JPM wakutana kwa mara ya kwanza Ikulu

Image
Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi mteule, Dk Willibrod Slaa, Ikulu Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 29, mwaka 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema Dk Slaa amemshukuru Rais kwa kumteua kuwa Balozi na kuahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa. Imeeleza kuwa Dk Slaa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uongozi bora na kutekeleza mambo makubwa ikiwemo miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa daraja la juu katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto rufiji na mapambano dhidi ya rushwa. “Kwa kweli naona faraja, ninafurahi Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza hatua kwa hatua karibu yote tuliyokuwa tunayapigania kwa miaka takribani 20 ya huko nyuma, mimi Dk Slaa nilikuwa napiga kelele kwa sababu nilikuwa naon...

Basi lateketea kwa moto Tanga Leo

Image
Basi la kampuni ya Tahmeed ambalo linafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa Nairobi limeteketea moto katika kijiji cha Matumbi mkoani Tanga leo. Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya moto na kusema kuwa hakuna abiria ambaye amepata madhara na moto huo ulioteketeza basi hilo. "Ni kweli basi hilo limewaka moto leo, ila hakuna abiria aliyejeruhiwa wala kupata madhara yoyote kwa kuwa dereva alipoona dalili za moto alipaki gari pembeni na abiri ambao walikuwepo kwenye basi hilo kama 15 hivi wote waliweza kushuka mapema kabla ya moto kushika gari zima" alisema Wakulymba

Mtulia:nimefanya maamuzi ya Kiume

Image
Mgombea wa Jimbo la Kinondoni kupitia CCM, Maulid Said Mtulia amesema amefanya maamuzi ya kiume ya yeye kuhamia chama hicho kwa sasa kwa maana wapo wengi wanataka kufanya hivyo lakini wameshindwa kwa madai wanasubiri kulipwa kiunua mgongo. Mtulia ameeleza hayo wakati alipokuwa anaendelea kujinadi kwa wananchi wa jimbo la Kinondoni ambalo hapo awali alikuwa analishikilia yeye kupitia chama chake cha CUF kabla ya kujivua uanachama wake na kuenda kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kuijenga nchi. "Kujiuzulu Ubunge sio mchezo, nimefanya maamuzi ya kiume maana kuna wenzangu wengine mpaka sasa hawawezi kutoka kwa sababu wanasubiri kiunua mgongo. Sasa kijana kama mimi nikae pale nisubirie kiunua mgongo hivi kweli ntaweza kuishi kwa kusubiri kiunua mgongo", alisema Mtulia. Aidha, Mtulia amesema amejinusuru kwa mengi kukihama chama chake cha awali ili aweze kuwapigania wananchi wa jimbo hilo kwa maana hapo awali alikuwa anashindwa...

DIAMOND PLATINUMZ AFUNGUKA KUMWALIKA WEMA SEPETU,AGUSIA PIA HAMISA MOBETTO,TUNDA NAYE AJAACHWA

Image
Majibu ya Diamond Platnumz Kuhusu Ujauzito wa Tunda HATIMAYE msanii kutoka industry ya Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameamua kuanika ukweli kuhusu tetesi za kumpachika ujauzito Video Vixen wa Bongo, Tunda. Akifanya mahojiano maalum ya , Diamond amekanusha kumpachika mimba staa huyo na kudai kuwa hajawahi hata kutembea naye wala kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.    

Man U Waitwanga Yeovil 4-0, Sanchez Aibuka Man Of The Match

Image
KLABU ya Soka ya Manchester United imeenedeleza ushindi kwa michezo mitatu mfurulizo tangu itoke mapumzikoni, Dubai ambpo usiku wa kuamkia leo imeitwanga timu ya Yeovil bao 4-0 katika michuano ya Kombe la Shirikisho (FA Cup). Katika game hiyo mchezaji mpya wa Man U aliyesajiliwa hivi majuzi akitokea Arsenal, Alex Sanchez ikiwa ni mechi yake ya kwanza alionyesha uwezo mkubwa huku akiisaidia timu yake hiyo kuibuka na ushindi mnono katika Mji wa Yeovil. Wenyeji Yeovil walianza vizuri lakini walifanya makosa yaliyopelekea kuadhibiwa na klabu hiyo tajiri zaidi duniani kwa sasa. Wafungaji ni; Rashford 40, Ander Herrera 61, Lingard 90, Lukaku 90+3. Yeovil: Krysiak, James, Sowunmi, Nathan Smith, Dickson, Green, Wing, Bird, Gray, Zoko, Surridge. Subs:  Connor Smith, Browne, Maddison, Gobern, Whelan, Santos, Fisher. Man Utd:  Romero, Darmian, Lindelof, Rojo, Shaw, Ander Herrera, Carrick, McTominay, Mata, Rashford, Sanchez. Subs: ...

DC aamuru mkandarasi akamatwe

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, John Palingo ameamuru kuwekwa mahabusu mkandarasi wa umeme kutoka Kampuni ya Cyber, Benjamin John baada ya kutuhumiwa kuchukua fedha kwa wananchi kwa madai ya kuwaunganishia umeme wa Wakala wa Nishati Vijijini (Rea) katika vijiji ambavyo havipo kwenye mpango huo. Palingo alitoa amri hiyo jana kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mbozi baada ya baadhi ya madiwani kudai kampuni hiyo imekuwa ikiwatoza baadhi ya wananchi Sh20,000 hadi 140,000 kwa ajili ya fomu na usajili wa mteja kuunganishiwa umeme. Kutokana na malalamiko hayo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Erick Ambakisye alilazimika kuuita uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Songwe na mwakilishi wa Kampuni ya Cyber kutoa ufafanuzi mbele ya baraza hilo. Hata hivyo, Mkandarasi na mwakilishi wa Kampuni ya Cyber, Benjamini John alipotakiwa kutoa ufafanuzi alikanusha madai hayo akieleza kwamba iwapo itathibitika kuwa kampuni yake imehusika, fe...

Trump Uso kwa Uso na Rais Kagame, Atuma Salamu Afrika

Image
Rais Trump (kushoto) akisalimiana na Rais Kagame. RAIS wa Marekani, Donald Trump amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na kumuomba afikishe salamu zake za upenzo kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU. Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi baada ya Mkutano wa Viongozi na Watu Mashuhuri Kuhusu Uchumi na Biashara Duniani. Mkutano huo wa Kagame na Trump umekuja wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kutoa kauli iliyotafsiliwa kama ni kuyakashifu mataifa ya Afrika. Kutoka kusoto ni mama Jeannette Nyiramongi Kagame, Rais Kagame, Rais Trump na Melania Trump. Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana ambapo  amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyakashifu mataifa ya Afrika huku aki kiri kutumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumz...

RUBY ASALIMU AMRI KWA CLOUDS,HATIMAYE AOMBA RADHI

Image
Msanii wa muziki Bongo, Ruby amemaliza tofauti baina yake na Clouds Media Group. Muimbaji huyo ametumia kipindi cha XXL kuwaomba radhi wale wote aliowakwaza katika chombo hicho cha habari. “Yeyote, awe ni mwanakamati wa Clouds, team Clouds au awe ni shabiki wa nje I like to apologize guy to say sorry to my country, sorry to this management Clouds, I love them so much all I need is support mimi naamini kwamba ukiwa mjinga kwenye kila kitu utapata kujua vitu vingi sana,” amesema Ruby. “Nilikaa nikamuomba Boss wangu Ruge samahani, mimi ni mdogo wewe ni mkubwa, of course kwa chochote kile mimi ndio nakosea,” amesema. Clouds Media Group walikuwa wamesitisha kucheza nyimbo za msanii huyo kutokana na tofauti zao, hivyo sasa nyimbo zake zinachezwa na inaelezwa tangu November mwaka jana ilitolewa ruhusu kwa ngoma zake kuchezwa.