Man U Waitwanga Yeovil 4-0, Sanchez Aibuka Man Of The Match
KLABU ya Soka ya Manchester United imeenedeleza ushindi kwa michezo mitatu mfurulizo tangu itoke mapumzikoni, Dubai ambpo usiku wa kuamkia leo imeitwanga timu ya Yeovil bao 4-0 katika michuano ya Kombe la Shirikisho (FA Cup). Katika game hiyo mchezaji mpya wa Man U aliyesajiliwa hivi majuzi akitokea Arsenal, Alex Sanchez ikiwa ni mechi yake ya kwanza alionyesha uwezo mkubwa huku akiisaidia timu yake hiyo kuibuka na ushindi mnono katika Mji wa Yeovil. Wenyeji Yeovil walianza vizuri lakini walifanya makosa yaliyopelekea kuadhibiwa na klabu hiyo tajiri zaidi duniani kwa sasa. Wafungaji ni; Rashford 40, Ander Herrera 61, Lingard 90, Lukaku 90+3. Yeovil: Krysiak, James, Sowunmi, Nathan Smith, Dickson, Green, Wing, Bird, Gray, Zoko, Surridge. Subs: Connor Smith, Browne, Maddison, Gobern, Whelan, Santos, Fisher. Man Utd: Romero, Darmian, Lindelof, Rojo, Shaw, Ander Herrera, Carrick, McTominay, Mata, Rashford, Sanchez. Subs: ...