Posts

Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Aitwa Polisi

Image
MBUNGE wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kama ‘Sugu’ na mratibu wa chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameitwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo huku wakisema hawajui sababu ya wito huo. Wawili hao wamesema wanahisi wito huo unatokana na mkutano wa hadhara alioitisha mbunge huyo katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Sugu amesema leo Jumanne kuwa, juzi jioni alipigiwa simu na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya (RCO) kwamba yeye na Masonga wafike jana ofisini kwa ajili ya mazungumzo lakini alimueleza kuwa itakuwa ni siku ya sikukuu hivyo itakuwa vigumu ngumu kwenda, hivyo walikubaliana wafike leo. “Polisi walinipigia simu juzi jioni wakinitaka mimi na Masonga twende Makao Makuu ya Polisi jana, nikawaambia itakuwa ni sikukuu hivyo tukakubaliana leo asubuhi. Sasa hivi tupo njiani tunaelekea huko kuitika wito. Sijajua sababu, lakini nadhani ni uchochezi,” amesema Sugu. Masonga amesema anaamini sa

Ikulu yatoa neno kuhusu kutokuapishwa kwa Dk. Slaa

Image
Balozi, Dk. Willibrod Slaa. WAKATI zikiwa zimetimia siku 40 baada ya kuteuliwa kuwa balozi, Dk. Willibrod Slaa (pichani), hajaapishwa na kuzua minong’ono hatimaye Ikulu imefunguka na kuweka kila kitu wazi. Itakumbukwa kuwa Rais Dk. John Magufuli alitangaza uteuzi wa Dk. Slaa kushika nafasi ya ubalozi Novemba 23, mwaka jana, lakini tangu wakati huo hajaapishwa. Rais Magufuli amekuwa na utamaduni wa kuteua viongozi na baada ya siku chache wanaapishwa, lakini kwa Dk. Slaa imechukua muda mrefu na kuibua sintofahamu. “Hili ni jambo ambalo siyo la kawaida, tumezoea mtu akiteuliwa kushika wadhifa fulani na rais baada ya siku chache, tunaona au kusikia kuwa ameapishwa, lakini kwa Dk Slaa ni zaidi ya mwezi sasa, kuna sababu zimetolewa? Tujulisheni,” ni moja kati ya simu nyingi za wasomaji wetu waliopiga chumba cha habari kutaka ufafanuzi. Kutokana na hali hiyo, Uwazi liliwasiliana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu ili kujua kwa nini imechukua muda mrefu kumuapisha Dk

SIWEMA AFUNGUKIA KUMUONA MWANAYE KWA NAY

Image
Nay wa Mitego akiwa na watoto wake. MZAZI mweza wa staa mkubwa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Siwema Edson amefungukia ishu ya kumuona mwanaye, Cartes kuwa, si kweli kwamba hajawahi kumuona tangu aondoke kwa jamaa huyo. Siwema mwenye maskani yake jijini Mwanza aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, si kweli kwamba hajawahi kuomuona mtoto wake kwani mara nyingi anapokwenda kumuona kwa mama wa mwanamuziki huyo, Nay anakuwa hajui. “Naongea naye kila mara, nimeshakwenda kumuona zaidi ya mara tatu, sema tu baba yake hajui hivyo angekuwa anamuuliza mama yake angempa jibu,”   alisema Siwema.

Uchangudoa wa Zari Waibua Kimbembe!

Image
MAMBO ni moto! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kukiri kuwa yeye ni changudoa mzee, kauli yake imeibua kimbembe. KUPITIA SNAPCHAT Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Snapchat, mwishoni mwa wiki iliyopita, Zari alitupia ujumbe akionesha kuwa yeye ni changudoa mzee, lakini mwenye mafanikio akimjibu hasimu wake, mwanamitindo Hamisa Mobeto bila kumtaja. “Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+, mama uliyeachwa mara mbili na tuzo juu,” alisema Zari kupitia Snapchat. Kwa muda mrefu, Zari amekuwa kwenye tifu la aina yake baada ya Mobeto kuzaa na bwana wake, msanii wa Bongo Fleva miezi michache iliyopita. KIBEMBE KILIVYOIBUKA Kitendo cha Zari kutoa kauli hiyo, kimbembe kiliibuka mtandaoni mara baada ya ukurasa wa Instagram wa Global Publisher, kutupia habari hiyo ambapo wafausi wa mtandao huo walianza kurushiana maneno makali huku kila m

WATU 120 WAMEKAMATWA WAKIWEMO MAPADRI NCHINI DRC CONGO

Image
Zaidi ya Makanisa 150 yaliandamana nchini DRC Congo December 31, 2017 wakimtaka Rais Joseph Kabila kuondoka madarakani katika maandamano hayo imetolewa taarifa na Msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Congo Florence Marchal Katika taarifa iliyotolewa imesema watu saba wameuawa mjini Kinshasa na mmoja katika mkoa wa Kananga, katikati mwa Congo na kuongeza kuwa watu 82 wamekamatwa wakiwemo mapadri, katika mji mkuu Kinshasa, na 41 katika maeneo mengine ya nchi hiyo. Katika hotuba yake ya kumaliza mwaka, Kabila amesisitiza kuwa kutangazwa  kwa ratiba ya uchaguzi wa December 2018, kumefungua njia ya maandalizi ya uchaguzi huo.

Masoud Kipanya awatoa hofu Watanzania

Image
 KUFUATI taarifa kusambaa mitandaoni jioni ya leo Januari 1,2018 kwamba, mchora katuni maarufu Tanzania, Masoud Kipanya amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za uchochezi, Kipanya kupitia akaunti yake ya Twitter ameibuka na kuwatoa hofu Watanznia kwa kuandika kauli hii. “Poleni kwa usumbufu na asanteni kwa kujali hali za wengine. Niko salama Alhamdulillah. Namshukuru pia aliyesambaza taarifa. ‘AMESAIDIA’.” Taarifa hizo zinadai kuwa, Masoud Kipanya ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds FM, amekamatwa na Polisi baada ya kuchora katuni ambayo ina maudhi ya uchochezi kati ya wananchi na serikali. Aidha katika kauli yake Masoud hajaweka wazi iwapo amekamatwa na amepelekwa kituo kipi cha polisi na kama ameachiwa au bado.

Dk. Shika Atangaza Kuihama Tanzania, Anaelekea Wapi? Soma Hapa

Image
MAPYA TENA! Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda kusihi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo. Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa New York Marekani. “ Sasa hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu halafu mimi nisepe, nikiwa hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa  Bara la Afrika, sasa ni world wide, ofisi itakuwa New York , nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR. “Hata mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto power, hizi

ELIMU YA BURE KWA WENYE MAGARI NA JINSI YA KUNUNUA MATAIRI YA GARI YAKO

Image
Hata kama huna gari kwa sasa naamini katika moja ya ndoto zako ni kumiliki gari, Isomee hii itakusaidia wewe na ndugu zako kama sio na rafiki zako. Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne ( 4 ) tu toka yatengenezwe (Sio toka uyafunge kwenye gari lako).......Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (*2603*) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne. Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. Kwa mfano *2603* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au *2699* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999. KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE......hapo ndio inapotokea tairi mpya umenu

ALICHOKIANDIKA MKE WA KAFULILA BAADA YA KUONANA NA TUNDU LISSU LEO

Image
Leo December 30, 2017 Mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Singida  Jesca Kishoa   alikuwa Nairobi Kenya ambapo alienda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi akiwa nyumbani kwake Dodoma na watu wasiojulikana. Kupitia account yake ya Instagram aliandika jumble usemao.>” Shauku yake ya kulitetea taifa hili imeongezeka mara 100000000000….. Aisee ni kama kuzima moto kwa petrol. Wasiojulikana wamemfanya awe jasiri zaidi.Glory to the Almighty God.Aluta Continua “

TRA Kumchunguza Kakobe Baada ya Kusema Ana Pesa Nyingi Kuliko Serikali

Image
Kufuatia Kauli ya Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe kudai kuwa ana pesa nyingi kuliko serikali, mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamepanga kumchunguza kiongozi huyo wa dini. Hayo yamesemwa leo na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema; “Tupokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao “Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema. “Tunawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe tukaanza kupitia kumbukumbu zetu ili kuona namna Askof

EBITOKE TENA,AIBUKA NA MENGINE KUHUSU BEN POL,AFUNGUKA MENGI LIVE

Image
Mchekesha kutoka kundi la Timamu, Ebitoke amefunguka uhusiano wake na msanii wa RnB Ben Pol ulivyo kwa sasa mara baada ya kupitia drama za hapa na pale. Ebitoke amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa licha ya kutofautiana hapo awali kwa sasa mapenzi yao yanaendelea kama kawaida. Hapana sijaachana naye, baada ya kulalamika kuwa hapokei simu yangu sasa hivi tupo vizuri kabisa, mlikuwa mnatuona hata kwenye baadhi ya show zake tupo pamoja, sasa hivi tupo fresh yeye ndiye boyfriend wangu sina mwingine,” alisema Ebitoke. Uhusiano wa wawili hawa ulianza June mwaka huu mara baada ya Ebitoke kujitokeza katika mitandao na vyombo vya habari na kudai kuwa anavutiwa na Ben Pol na angetamani kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi kitu ambacho kinaelezwa kilikuja kutimia hapo baadaye.

TCRA YASHUSHA GHARAMA ZA MAWASILIANO

Image
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA), imetangaza kupunguza kiwango cha gharama za mawasiliano ya simu nchini Tanzania kutoka 26.96 kwa dakika moja mwaka huu hadi 15.60 kuanzia 2018. Akitangaza punguzo hilo la viwango vipya vya mawasiliano ya simu ambavyo vitaanza kutumika Januari Mosi, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema viwango hivyo vitaendelea kupungua kila mwaka hadi kufikia shilingi 2 mwaka 2022 Aidha Mhandisi Kilaba amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa matumizi ya simu na kuongeza pato la watoaji huduma wa mitandao ya simu na taifa kwa ujumla.

Faida 10 za kutumia Mafuta ya Nazi

Image
1. Mafuta ya nazi kwa afya ya Moyo: Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo ‘lauric acid’ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla. Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum. 2. Mafuta ya nazi huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula: Hii ndiyo moja ya faida ya mafuta ya nazi niipendayo zaidi. Ndiyo mafuta ya nazi yanayo uwezo kusaidia kudhibiti uzito uliozidi kwa sababu mafuta haya ni mepesi kumeng’enywa na hayagandi kama yalivyo mafuta mengine mazito (fatty acids) jambo linalosaidia kuuondoa uzito uliozidi mwilini. Kutokana na kitendo hiki cha kuongeza uwezo w

EBITOKE AANIKA UTAJIRI WAKE

Image
Msanii wa vichekesho hapa bongo Ebitoke, amesema kazi anayoifanya ya kuchekesha imempa mafanikio makubwa kwa muda mfupi, ikiwemo kumiliki mali zake mwenyewe. Ebitoke amesema kupitia sanaa hiyo ameweza kumiliki nyumba yake mwenyewe pamoja na gari ya kutembelea. “Hii kazi ninayofanya imenipa mafanikio sana, ingawa watu wananiona mpaka mafuta, mpaka sasa hivi nina nyumba yangu mwenyewe, na nyumba sio peke yangu ipo ya kwangu na ya bwana mjeshi ndio zipo tayari mpaka sasa, na tutazitambulisha hivi karibuni, pia nina gari yangu mwenyewe, aina gani na ya thamani gani mtaambiwa siku vitakapotambulishwa”, amesema Ebitoke. Sambamba na hilo pia Ebitoke amesema anaushukuru uongozi alionao kwa kumfikisha hapo alipo, kwani siku zote alikuwa na ndoto za kufikia malengo yake na wao ndio wamehakikisha anafikia malengo hayo.

STAA ZARI AMJIA JUU HAMISA.

Image
Bado majina ya baby mama’s wake  Diamond Platnumz  yanazidi kuchukua headlines kila kukicha katika mitandao ya kijamii, ambapo  Zari   na  Hamisa Mobetto  wamekuwa wakirushiana vijembe katika mitandao ya kijamii toka  Zari  afahamu kuwa  Hamisa   amezaaa na  Diamond . Zari  anaonekana kuendelea kurusha vijembe kupitia instagram yake na kujiita kuwa yeye ni mchepuko wa  Diamond Platnumz  kutokana na vijembe ambavyo  Hamisa Mobetto  alivirusha kwake siku chache zilizopita, Kupitia mtandao wa snapchat wa  Zari  alipost picha 7 ambazo kwa kila picha alindika caption na kusemekana kuwa kwa kile alichokiandika amemjibu  Hamisa Mobetto  juu ya vijembe vyake. “mdogoo, kila siku mdogo!! Mdogo na mzuri lakini huwezi kupata mwanaume wako….mwanamke gani haujiamin……kama unajiamini na uzuri na akili basi tuone ni mwanaume gani atakutaka baada ya hizi drama….baba wa mtoto wa tatu anakuja na atakuacha tu” “unaweza kuendele kupost picha zako za zamani na kila kitu nimetengenez

Babu Seya, Papii Kocha ‘Wapigana’ Kumuona Magufuli

Image
WASANII wa muziki wa dansi Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanawe Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ ambao kwa sasa wapo mapumzikoni wanahangaika kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili waweze kumshukuru. Msemaji wa familia hiyo ambaye pia ni msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini Mzee King Kiki amefunguka na kusema kuwa wasanii hao Babu Seya na Papii Kocha kwa sasa wapo mapumzikoni na kuwa wanahangaika kupata nafasi ya kuonana na Rais ili waweze kumshukuru kutokana na kuweza kuwapa msamaha mnamo Disemba 9, 2017 uliowafanya kuwa huru baada ya kutumikia jela kwa zaidi ya miaka 10.  “Saizi Nguza na Papii wapo kwenye mapumziko lakini wanapaswa kurudi nyumbani Congo kwenda kutekeleza mambo ya kimila, hivyo hawapaswi kufanya jambo lolote lile kwa sasa mpaka wakamilishe hilo suala la kimila, ila kabla ya wao kuondoka tumekuwa tukiomba kama tunaweza kupewa nafasi ya kuonana na Mhe. Rais kumshukuru na kumpa ahsante

Polisi: Tutamkamata na Kumhoji Askofu Kakobe kwa Uchochezi

Image
Licha  ya kutokiri moja kwa moja juu ya taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu kumkamata Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGFC) lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi limesema ni lazima litamhoji kiongozi huyo wa kiroho. Kuhojiwa huko kumetokana na kauli yake dhidi ya serikali aliyoitoa wakati wa ibada ya Krismasi. Jana, kulienea taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kueleza kwamba askofu huyo alitiwa mbaroni jana asubuhi na askari wa Jeshi la Polisi huku sababu za kukamatwa zikielezwa kuwa ni ujumbe alioutoa wakati wa mahubiri yake ya ibada ya Krismasi. Akizungumza na Nipashe jana kuhusiana na ukweli wa taarifa za kutiwa mbaroni kwa Askofu Kakobe, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa ni kweli walishakuwa katika harakati za kumkamata. “Ametoa maneno ya kashfa katika mahubiri yake, lakini sina taarifa kama amekamatwa,”  Kamanda Mambosasa alisema na kuongeza: “Taarifa

BABA MZAZI ,ALIYENASWA GESTI NA, MWANAYE WA KUMZAA KIMENUKA!

Image
Fadhil Mshamu, mkazi wa Kibaha mkoani hapa anakula Krismasi na Mwaka Mpya wa 2018, akiwa na stresi kufuatia kusomewa shitaka la kumdhalilisha binti yake wa kumzaa jina linahidhiwa kwa sababu za kimaadili. Kesi hiyo ilitajwa wiki iliyopita ambapo itaanza rasmi kusikilizwa mapema Mwezi Januari, mwakani katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Mshamu alikutwa na kasheshe hilo baada ya miezi kadhaa kunaswa akiwa na binti yake wa kumzaa kwenye nyumba moja ya kulala wageni (gesti) huko Kibaha huku kukiwa na madai ya kumtaka kingono. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Mshamu alinaswa akiwa na binti yake huyo baada ya kuwekewa mtego kufuatia taarifa za kumsumbua kwa muda mrefu akidaiwa kumtaka kimapenzi. Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya familia ya Mshamu, baada ya kunaswa kwenye mtego huo uliowashirikisha polisi na ndugu wa familia hiyo, Juni 26, mwaka huu, Jeshi la Polisi lilimfungulia Mshamu jalada la uchunguzi ambalo lilipelekwa kwa Mwendesha Mas

Mkurugenzi Mtendaji CRDB Atangaza Kung’atuka

Image
MTENDAJI Mkuu wa CRDB Bank, Dr Charles Kimeo, leo ametangaza kustaaafu ifikapo Mei 2019. Dkt. Kimei aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba hatua hiyo ni kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo kupata mtu atakayeshika nafasi yake kwa mujibu wa taratibu na kanuni zilizopo. Kabla ya kujiunga na benki hiyo, Dk Kimei alifanya kazi Benki Kuu ya Tanzania kama Mkurugenzi Mfawidhi wa Shughuli za Benki, Mkurugenzi wa Sera, Uchumi na Utafiti, Meneja wa Idara ya Utafiti wa Uchumi na Sera na nyadhifa nyingine mbalimbali katika Idara ya Utafiti. Hivi sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki Mabenki nchini. Amewahi pia kufanya kazi katika bodi mbalimbali ikiwemo ya Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Mamlaka ya Elimu nchini, Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampuni ya Huduma za Mikopo Midogo ya CRDB na tawi la CRDB nchini Burundi. Dkt. Kimei ana Shahada ya Uzamivu katika Uchumi aliyoipata Chuo Kikuu cha

Ikulu Haina Taarifa ya JPM Kushinda Tuzo ya Mandela

Image
IKIWA ni siku moja baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ametunikiwa Tuzo ya Amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) huko nchini Afrika Kusini, huku kukikosekana taarifa rasmi kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo. Leo Alhamisi, Desemba 28, 2017 kupitia kipindi cha Joto la Asubuhi cha Radio  E-FM, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa amesema kuwa hana taarifa yoyote juu ya tuzo hiyo. “Mimi sina taarifa zozote kwa sababu mtu anapotoa tuzo sio lazima awasiliane na mtu anayempa tuzo, wao wanakuwa na vigezo vyao kadri ya watu walivyowapima viongozi.“ amesema Msigwa. “Mimi sina information zozote kwa hiyo ni vizuri mngewatafuta hao Nelson Mandela wenyewe hicho chuo waweze kuwaeleza tuzo hizo taarifa wanakuwa nazo vyuo wenyewe,“ amesisitiza Msigwa. Hata hivyo tayari Wakfu wa Nelson Mandela nchini Afrika Kusini umebainisha kuwa haukuandaa, kusimamia wala kutoa tuzo