Posts

Kunyonyana ulimi au kula mate Kunasababisha kuambukiza VVU?

Image
Swali:  Je kunyonyana ulimi au kula mate kunaweza kuambukiza VVU? Jibu: Njia ya mdomo inaweza kuchangia mtu kupata VVU kama mtu atakutana na mtu mwenye VVU mwenye vidonda au michubuko mdomoni nawe pia ukawa una michubuko au vidondamdomoni, ili kuweza kupata VVU kwa njia ya mate inabidi kulambamate lita 2 jambo ambalo ni gumu.

RAIS DKT. MAGUFULI AKIFUNGUA UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wa pili kutoka (kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuashiria ufunguzi rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi hao mara baada ya ufunguzi wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya ufunguzi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald kuashiri

Wakili Msomi Atinga Mahakamani Kudai Wanaume Wafutiwe Mahari

Image
Wakili msomi nchini Zimbabwe, Bi. Priccilar Vengesai ameanzisha kesi mahakamani ya kufutilia mbali mahari zinazotolewa na wanaume pale wanapooa akidai kuwa ni mila iliyopitwa na wakati. Tokeo la picha la pete ya ndoa Wakili huyo amewasilisha malalamishi yake katika mahakama juu nchini humo akitaka kusikilizwa kwa kesi yake huku akilalamika kuwa utamaduni huo unakiuka haki za kibinaadamu. Bi. Priccilar Vengesai anaamini kuwa endapo utamaduni huo utaendelea ,familia zote za mume na mke zinatakiwa kulipa mahari kwa maslahi ya usawa wa kijinsia. Akizungumza na gazeti la serikali nchini Zimbabwe la Herald, Wakili huyo amesema kuwa anataka kuolewa upya baada ya ndoa yake ya kwanza kuvunjika kwani hakuwa na sauti ya kuhoji kiasi cha mahari iliyotolewa na kujiona kama bidhaa. “Nataka kuolewa tena sitaki kupitia kama niliyopitia kwenye ndoa yangu kwani sikushiriki katika kuuliza gharama ya mahari. Sikupewa fursa ya kuuliza kwa nini mahari ilitolewa wa

RAIS MAGUFULI AAMURU WATATU KUCHUNGUZWA KWA KUTAKA KUIIBIA SERIKALI MABILIONI

Image
RAIS Dk. John Magufuli, ameamuru kukamatwa kwa watumishi watatu wa serikali, kwa tuhuma za kuandika madai yasiyo halali, kwa lengo la kuiibia serikali.Rais Magufuli ametoa amri hiyo wakati akizindua Uwanja wa Ndege wa Bukoba wenye urefu wa kilomita 1.5 ambapo amewataja watumishi hao kuwa ni Jackson Kaswahili Robert, Mwachano Msingwa na Gidioni Zakayo. Alifafanua kwamba, Jackson alijaza fomu zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.626 lakini madai hayo yalipochunguzwa, ilibainika kuwa hadai chochote.Akaongeza kwamba Mwachano yeye alijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.754 wakati ukweli ni kwamba anaidai shilingi milioni 2 tu huku Gidioni ZakayoAkijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi milioni 104 wakati si kweli.Hawa wote pamoja na maofisa wizarani walioidhinisha malipo haya, naagiza vyombo vya dola viwashughulikie. Tumekuwa na watu ambao hawana uchungu na wengine,” alisema Rais Magufuli.

Wanachama 12 wa Chadema Wafikishwa Makamani Arusha

Image
Wanachama 12 wa Chadema mkoani Arusha wanaotuhumiwa kumshambulia mgombea udiwani wa CCM katika Kata ya Muriet, Francis Mbise wamefikishwa Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso iliyopo jijini Arusha leo. Miongoni mwa washtakiwa hao ni Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Innocent Kisanyage na mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Mlimani, Yohana Gasper. Baada ya kufikishwa mahakamani wamepelekwa mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabili

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ulioanza leo tarehe 6 na unatarajiwa kumalizika tarehe 8 november, katika ukumbi wa APC Bunju, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)         Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna ya mashine ya kuchora kadi za mifumo ya umeme inavyofanya kazi na Mhandisi Vedastus Sichilima kutoka D.I.T (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​ Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, leo amefungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi. Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya APC Bunju wilayani Kinondoni, umeandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikianana Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ya nchini Finland. Akihutubia washiriki katika

Mwanamfalme Wa Saudi Arabia Afariki Katika Ajali Ya Ndege

Image
MWANA wa mfalme  nchini Saudi, Arabia Mansour bin Muqrin,  amefariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka karibu na mpaka wa nchi hiyo na Yemen, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti. Mwana mfalme huyo,  Mansour bin Muqrin, naibu gavana wa mkoa wa Asir, alikuwa akisafiri  na maofisa kadhaa wa serikali helikopta hiyo ilipoanguka, kituo cha runinga ya Al-Ikhbariya imesema. Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika hadi sasa. Kuna habari kwamba Saudi Arabia ilkuwa imetungua kombora la masafa marefu lililokuwa limerushwa kutoka Yemen likiwa karibu na uwanja wa ndege wa Riyadh Jumamosi. Pia, wakati wa wikiendi, watu wengi wakiwemo wana wa wafalme 11 na mawaziri wanne walikamatwa katika kampeni ya kukabiliana na rushwa ambayo inatazamwa kama njama ya kuimarisha mamlaka ya mrithi mtarajiwa wa ufalme.  Taasisi hiyo ya kukabiliana na ufisadi iliundwa na mwanamfalme wa kwanza kwenye urithi, Mohammed bin Salman. Mansour bin Muqrin, aliyefariki, ni mwana wa mwanam

SIMBA 6 WATOROKA KWENYE HIFADHI YAO WAINGIA MTAANI.

Image
Simba wapatao sita wa Mbuga ya Taifa ya nchini Nairobi wametoroka kwenye hifadhi hiyo na kuingia mjini kwenye makazi ya watu na baade kurudi wenyewe kwenye hifadhi yao.Simba hao walionekana majira ya asubuhi maeneo ya Hhospitali ya Langata wakizunguuka na baadae maeneo ya Kibera ambapo huishi watu wengi hayo yamezungumzwa na Muhudumu wa hifadhi hiyo Paul Udoto kwa mujibu wa chanzo cha habari hii. Aidha baada ya muda wahusika wa hifadhi hiyo kuona Simba hao hawapo walianza kuwafuatilia na baada ya nuda wakiwaona wakirudi wenyewe kuelekea kwenye hifadhi hiyo ambapo hakuna aliyepatikana kujeruhiwa na simba hao

ZARI THE BOSS LADY AUMBULIWA NA MITANDAO YA HABARI NCHINI UGANDA!MAISHA YAKE YA MTANDAONI NA NYUMBANI KWAO MAZITO YAIBUKA

Image
Mwanamama Zarinah Hassan Tlale almaarufu Zari The Boss Lady. Wakati akitajwa kuwa mmoja wa wanawake masta-watafutaji na matajiri wa Afrika Mashariki, mwanamama Zarinah Hassan Tlale almaarufu Zari The Boss Lady ameumbuliwa, Risasi Jumamosi limetonywa. KIJIJINI MAMBO SI MAMBO Zari anadaiwa kuumbuliwa na mitandao ya habari za mastaa ya nchini Uganda ambayo imeeleza kwamba, pamoja na kuwa na fedha nyingi na maisha ya kufuru, lakini huko nyumbani au kijijini kwao, Jinja nchini Uganda mambo si mambo. Akiwa na watoto wake. Kwa mujibu wa mitandao hiyo iliyoamua kumwanika Zari baada ya kutajwa kuwa na utajiri mkubwa miongoni mwa mastaa wa nchini humo, Jinja ndiko alikozaliwa na kukulia kabla ya kuhamia Kampala, lakini maisha ya ndugu zake hasa makazi ni duni au ya hali ya chini ukilinganisha na mbwembwe za utajiri wake. WATU WANASHANGAA “Kwa tunaofahamu kijijini kwao (Jinja), tunashangaa kama kweli ana utajiri kama anavyojinadi maana maisha ya ndugu zake ni ya chin

Tume Ya Uchaguzi Yateua Madiwani 3 Wa Viti Maalum

Image
Tume ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 3 November 2017 imeteua madiwani watatu kujaza nafasi za Udiwani katika Halmashauri mbili za Tanzania Bara.

KAULI YA LOWASSA BAADA YA LAZARO NYALANDU KUIHAMA CCM

Image
ALIYEKUWA Mgombea Urais wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amemkaribisha aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ambaye amejivua uanachama na kuachia nyadhifa zote alizokuwa nazo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Akionyesha kuwa na furaha alipozungumza na Mwananchi leo Jumatatu, Lowassa hakuwa na maneno mengi, akiyafupisha kwa kusema “tumelamba dume”. Nyalandu (47), ambaye pia alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alitumia nafasi hiyo kuomba kujiunga na Chadema, akisema anaiomba imfungulie mlango. Dakika chache tangu Nyalandu aombe kujiunga na Chadema, Lowassa alimkaribisha waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii huku akisema mwanasiasa huyo amechelewa kujiunga na upinzani. “Mbona amechelewa? Alitakiwa awe amejiunga muda mrefu, tena hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu. Ninamkaribisha sana kwa sababu ni mwanasiasa mzuri na anayejua majukumu yake,” alisema Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika Se

Meya wa Jiji la Mwanza Akamatwa na Polisi

Image
James Bwire (kulia). TAARIFA zilizotufikia kwenye dawati letu la habari zinaeleza kuwa, Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire anashikiliwa na Polisi huku ikidaiwa kuwa amri ya kukamatwa kwake ni agizo la mkuu wa mkoa huo, John Mongella. Hayo yamesemwa na Mariam Lima ambaye ni katibu wa mitandao ya taasisi ya Alliance inayomilikiwa na Meya Bwire ambaye ameeleza kuwa kuwekwa kwake sentro ni kunatokana na agizo la mkuu wa mkoa. Hata hivyo, Mongella amekana kuamuru kukamatwa kwa kiongozi huyo anayeshikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Jiji la Mwanza. “Nimepata taarifa za meya kuwekwa mahabusu; mimi sihusiki na ninazifuatilia kujua kinachoendelea,” amesema Mongella leo Jumatatu Oktoba 30,2017. Taarifa zinasema meya Bwire amekamatwa katika Uwanja wa Ndege Mwanza wakati wa mapokezi ya Rais John Magufuli ambaye ziko ziarani mkoani humo. Lima amesema, “Tunafanya jitihada za kumwekea dhamana ingawa tunakabiliana na changamoto nyingi.” Tangu Aprili, Bwire na Mkur

ZITTO KABWE AMPA NENO NYALANDU BAADA YA KUIHAMA CCM

Image
MBUNGE wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumpongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Nyalandu ambaye leo Oktoba 30, 2017 amefanya maamuzi ya kuachana na CCM na kusema kiongozi huyo amefanya maamuzi sahihi. Zitto Kabwe amesema kuwa kutokana na uchumi unavyoporomoka haki za watu zinavyovunjwa jambo alilofanya Nyalandu ni sawa na kuwa huko ndiyo kuonyesha uongozi. “Lazaro Nyalandu, umeonyesha Uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na Uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu Sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na Kwa sababu sahihi. Kila la kheri|” aliandika Zitto Kabwe Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nch

Breaking News: Nyalandu Ajiuzulu Ubunge, Ajivua Uanachama CCM, Kuhamia Chadema

Image
Lazaro Nyalandu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amejiuzulu uanachama na vyeo vyote alivyokuwa navyo ndani ya chama hicho, pamoja na kuachia nafasi ya ubunge, kwa kile alichoeleza kwamba ni kutoridhishwa na mwenendo wa kisiasa ndani ya chama hicho.Akizungumza na waandishi wa habari leo, Nyalandu amesema ameamua kuachia nyadhifa zote ndani ya chama hicho, kuanzia leo, Oktoba 30, 2017 na kama itawapendeza viongozi wa Chadema, anaomba kujiunga na chama hicho. Hiki ndicho alichokiandika Nyalandu: NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017. HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA DARAJA LA WAENDA KWA MIGUU LA FURAHISHA JIJINI MWANZA

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akivuta utepe kwenye jiwe la ufunguzi kuashiria ufunguzi wa wa Daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha liliopo jijini Mwanza. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kufungua daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza. Sehemu ya wananchi waliohudhuria ufunguzi wa daraja la Waenda kwa miguu la Furahisha jijini Mwanza.     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa