Posts

Kichwa cha mwandishi aliyetoweka chapatikana baharini Sweden

Image
                 Kichwa cha mwandishi wa Sweden Kim Wall kimepatikana , miezi miwili baada ya kupotea katika ziara na raia mmoja wa Denmark. Waogeleaji walipata mifuko iliokuwa na kichwa chake, miguu na nguo katika eneo la Koge Bay kusini mwa mji wa Copennhagen kulingana na inspekta mkuu wa polisi wa eneo hilo Jens Moller Jensen. Vilipatikana karibu na pale mwili wa Wall ulipokuwa siku chache tu baada ya kupanda katika manuwari tarehe 10 Agosti. Bwana Marsden mwenye umri wa miaka 46 amekana kumuua bi Moller Jensen akisema mabegi hayo yaliopatikana yalikuwa yamechanganywa na kupimwa uzani na vipande vya vyuma. ”Jana alfajiri tulipata begi ambalo lilikuwa na nguo za Kim, suruali ya ndani na viatu.katika begi hilo hilo kulikuwa na kisu na kulikuwa na mabomba ya magari” . Matokeo ya uchunguzi yamebaini kwamba kichwa hicho ni cha bi Wall na kwamba hakina ishara za kwamba fuvu lake la kichwa liliumizwa ama hata kupigwa. ...

Sirro Asema Hataki Malumbano Kuhusu Kushambuliwa Lissu

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro. Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema hataki malumbano na hana majibu kuhusu shinikizo linalotolewa na Chadema na familia ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuruhusu vyombo vya nje kufanya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi kwa mbunge huyo. IGP Sirro amesema hayo leo Jumapili jijini hapa, akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alipojibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kauli yake baada ya familia ya Lissu na viongozi wa Chadema kutamka kuwa hawana imani na Jeshi la Polisi kuhusu uchunguzi huo. Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) alijeruhiwa kwa risasi Septemba 7 mjini Dodoma na sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya. IGP Sirro amesema yeye na jeshi lake wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria kwa kuwatumikia Watanzania wote kuhakikisha wanakuwa sala...

ZARI THE BOSS LADY AKATA MZIZI WA FITNA,AIBUKA NA KUJIBU YOTE LIVE

Image
                 Mpenzi wa Diamond Platnumz, Zarina Hassan maarufu kama Zari The Boss Lady amefunguka na kudai kuwa yeye na mpenzi wake huyo hawajaachana. Akiongea katika U-Heard ya Clouds FM, Zari amedai kuwa hawajaachana kama inavyodaiwa na watu hii ni kutokana na kuwa hakumu-wish happy birtday katika mitandao ya kijamii kama ilivyozoeleka. Hakuna lolote baya linaloendelea kati yake na Diamond, na wanaheshima mikataba aliyonayo na kampuni pia hakuna chochote kibaya kinachoendele,” ameema mrembo huyo. Pia akaongeza kuwa “Nilimu-wish siku yake ya kuzaliwa sema nilitumia njia ya kawaida,na tunajaribu kuhamisha maisha yetu katika mitandao kuwa ya kawaida. Vile vile mrembo huyo alisisitiza kuwa stori zinazoenezwa kuwa Nillan sio mtoto wa Diamond sio za kweli na kuhusu DNA pia sio kweli.

BREAKING NEWS : AJALI MBAYA YA GARI NA TRENI TANGA LEO

Image
Gari iliyokuwa kuwa imepakiza watoto imezima kwenye kivuko cha Kwaminchi na kugongwa na treni. Watoto wawili waliokuwa wamekaa mbele walinusurika kifo baada ya dereva kuwaambia waruke, ila waliumia na kukimbizwa Hospitali.

IGP SIRRO AWAJENGEA UWEZO ASKARI WA MBEYA

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akisalimiana na waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya, aliokutananao Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo leo, IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Katibu Tawala mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja na kamanda wa Polisi mkoani humo (DCP) Mohamed Mpinga, wakiwa katika picha na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa baada ya kikao kazi cha kubadilishana uzoefu katika kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu aliloandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoani Mbeya kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna ya kuwasaidia. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wa kutumia silaha za moto cha mk...

CHADEMA JIMBO LA IRINGA MJINI GIZA NENE, MADIWANI WALIOJIUZULU WATIMKIA CCM.

Image
Na Fredy Mgunda,Iringa. Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimalisha kwa kuvuna wanachama watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na mikakati ya kuja kulikomboa jimbo la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama cha CHADEMA. Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao kutoka kata ya kitwiru mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya aliwapongeza wanachama kwa kutambua kazi inayofanywa na chama cha mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano DR John Pombe Magufuli. “Mimi nimefurahi sana nyie kurudi nyumbani maana mtakuwa na msaada mkubwa sana katika kukijenga chama hapa manispaa ya Iringa ili tuweze kulikomboa jimbo hili katika uchaguzi ujao nah ii ndio mikakati yetu”alisema Rubeya Rubeya  aliwaambia wanachama hao kuwa sasa wapo katika mikono salama ya kisiasa tofauti na walipokuwa kwenye chama cha awali na kuwasihi wasiwe waoga katika kufanya kazi za ku...

Mbowe ampongeza Rais Magufuli

Image
Babati.  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amepongeza kitendo cha Rais John Magufuli kuitenganisha Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa kwa zaidi ya miaka saba kambi hiyo ilikuwa inaishauri Serikali kufanya hivyo. Mbowe amesema hayo leo Jumamosi kwenye mazishi ya marehemu Philip Gekul, baba mzazi wa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul yaliyofanyika kata ya Dareda. Amesema kwa mujibu wa kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa kambi rasmi ya upinzani ilikuwa inashauri wizara hiyo itenganishwe lakini ushauri wao haukufanyiwa kazi. "Wizara ya Nishati na Madini ni wizara nyeti mno na mara nyingi tumekuwa tukiishauri Serikali iitenganishe wizara hiyo kwani ni kubwa na nyeti ila sasa wameona ushauri wetu unafaa na kuzitenganisha," amesema Mbowe. Amesema suala siyo nani anafaa kuwa waziri na nani hafai kuwa waziri au ukubwa wa wizara ila suala ni kuona namna gani ya kuendesha Serikali ya Awamu ya Tano. er 07, 2017 No comments Babati.  Mwenyekiti wa Chadema,...

FT: TANZANIA 1-1 MALAWI kKUTOKA UWANJA WA UHURU

Image
Kikosi cha timu ya Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Malawi leo Uwanja wa Uhuru Dar. Kikosi cha timu ya Malawi. MPIRA UMEKWISHA Dk 90+4 Samatta yuko chini anatibiwa baada ya kugongana na beki wa Malawi wakati akijaribu kufunga, wote wametolewa nje kutibiwa Dk 90+2 Muzamiru analambwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu ya pili kwa Taifa Stars Dk 90 nafasi nyingine ya Taifa, lakini kipa wa Malawi anaokoa Dk 90 nafasi nyingine ya Taifa, lakini kipa wa Malawi anaokoa Dk 88 Mbaraka Yusuf anapoteza nafasi akiwa yeye na lango, kazi nzuri ya Samatta ameshindwa kuitumia Dk 85, Nyoni amepewa kadi nyekundu, mwamuzi anamtuhumu kumpiga mwenzake kiwiko lakini mchezaji huyo wa Malawi, hakuadhibiwa kwa kuwa alimvamia Nyoni Dk 83 Abdul Hilal anayecheza Tusker ya Kenya anaingia kuchukua nafasi ya Simon Msuva anayecheza Difaa Al Jadid ya MoroccoDk 78, inaonekana mashambulizi ya Malawi kutoka upande wa mashariki ni hatari kwa afya ya lango la Tanzania Dk 70, Taifa Star...

ZITTO KABWE AFUNGUKA KUHUSU BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT -Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, ametoa maoni yake juu ya Baraza jipya la Mawaziri lililofanyiwa mabadiliko hii leo, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Kwenye ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe ameandika ujumbe akiwapongeza Mawaziri hao walioteuliwa ambao wengi wao ni vijana, huku akiwataka kuchapa kazi kwa bidiiUteuzi wa vijana kushika nafasi za juu ni hatua nzuri, naona vijana wengi wamepewa majukumu makubwa, ninawaombea watekeleze majukumu kwa weledi mkubwa”, ameandika Zitto Kabwe. Leo Rais Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mpya mbili, baada ya kuzivunja baadhi ya wizara ambazo zilikuwa na vitengo vingi.

JPM Ateua Mawaziri Wapya, Lugola, Shonza Ndani, Maghembe, Kashililah Out

Image
Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri nchini huku akizigawanya baadhi ya wizara zikiwemo Wizara ya Kilimo na Mifugo, Nishati na Madini na kuongeza wizara mpya mbili na kufikisha jumla ya wizara 21. Katika Mabadiliko hayo, Mawaziri wawili na manaibu waziri wameongezwa. Aidha Rais Magufuli ametangaza mabadiliko na kuteua Katibu mpya wa Bunge huku akieleza kuwa aliyekuwa Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila atapangiwa kazi nyingine. ORODHA. Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu: Naibu Waziri – Stella Alex Ikupa Wizara ya Mifugo na Uvuvi: Waziri – Luhaga Mpina, Naibu Waziri -Abdallah Hamisi Ulega. Wizara ya Maji na Umwagiliaj: Waziri- Mhandisi Isack Kamwelwe, Naibu Waziri – Jumaa Hamidu Aweso. Wizara ya Nishati: Waziri – Dk. Medard Kalemani, Naibu Waziri – Subira Khamis Mgalu. Wizara ya Madini: Waziri – Angellah Kairuki, Naibu Waziri -Stanslaus Haroon Nyongo. Wizara ya Maliasili na U...

BREAKING NEWS: JERRY MURO AJIBU TUHUMA NZITO ZA CHADEMA, AMVAA MAZIMA LEMA

Image
      KADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia aliwahi kuwa Msemaji wa klabu ya yanga, Jerry Muro ameibuka na kuwaponda viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku akiwataka waache porojo na badala yake wajikite katika kuwaletea maendeleo wananchi wao.Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Muro amewataka viongozi wa Chadema wanaodai kuwa wanafuatiliwe na watu ili wauawe, waseme wanafuatiliwa na akina nani?“ Nimemsikia baadhi ya wabunge wa Chadema wakisema kuna watu wanawafuatilia, dada yangu kule Bunda (Ester Bulaya) akisema anafuatiliwa na watu waliovaa kininja, nani awafuatilie nyie? Kwani mmeiba makinikia?“Lema naye anasema wamefungua nati za gari lake, pia anadai akiwa kwenye mwendokasi aliona watu wanamfuatilia akaruka kwenye gari akamwachia usukani mkewe, hivi kweli gari lipo kwenye mwendokasi unarukaje kichakani? Acheni maigizo jamani…” Nani akutafute wewe Lema? Mbona husemi wakati ukiwa na nywele za ra...

Wolper Anapozomeana na Kivuli Chake

Image
Jacqueline Wolper Massawe, aliye pia na a.k.a nyingi zikiwemo za Gambe na Amber Rose wa Bongo. MIONGONI mwa waigizaji wa kike niliowahi kufanya naye kazi kwa kipindi kirefu na kwa ukaribu zaidi ni pamoja na mrembo Jacqueline  Wolper Massawe, aliye pia na a.k.a nyingi zikiwemo za Gambe na Amber Rose wa Bongo. Mkononi nimefumbata miaka saba sawa tangu nianze kazi ya uandishi wa habari, kwenye magazeti haya pendwa. Ninao uzoefu mkubwa kwa kuwafahamu watu wengi maarufu kwa maana ya maisha yao ndani na nje ya kazi zao, nawajua sana hususan wasanii wa filamu ambao nafanya nao kazi mara kwa mara. Hata wengi wao wananijua vyema , kwenye eneo la kazi kwamba huwa siruki sentensi kwenye kuanika ukweli. Hivi karibuni, Wolper alikaririwa na mmoja wa waandishi wenzangu akisema kitendo cha kumshika na kumbeba mtoto wa mwigizaji mwenzake, Faiza Ally kimemuondolea gundu ya kutopata mtoto hivyo na yeye kutarajia kupata wa kwake mwakani. Sawa, Wolper yuko sahihi lakini mbo...

FAIZA ALLY AJITOSA SAKATA LA DIAMOND PLATINUMZ NA ZARI THE BOSS LADY,AFUNGUKA LIVE

Image
Huku Tetesi na Stori kibao zikikamata headlines mitandaoni kuwa couple ya @diamondplatnumz Na mama watoto wake @zarithebosslady SASA IMEBAKI STORI, Faiza Ameandika ujumbe Huu :. By @faizaally_ – Diamond kijana mdogo sana anahitaji ku have funny na watoto wenzie na sisi wa dada watu wazima tuangalie watu wa kutoka nao… Go baba and have funny enjoy the world ndio useto down …. jiachie uwe huru ikibidi usiwe na mahusiano , bado hujaiona dunia hata robo, we ni star , hela ipo there is lot to see…nasema with clean heart no hate kwa zari au kwa yoyote , nimezurula sana duniani kabla ya kuzaa na kutulia…jiachie life is today buana

Taarifa Muhimu ya TCU kwa Wanafunzi Waliokosa Vyuo

Image
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia Umma kuwa  awamu ya kwanza ya Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ulimalizika tarehe 30 Agosti 2017. Tume inawaarifu kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo wa 2017/18. Hata hivyo kutokana na  waombaji wengi  kutochaguliwa  kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 4 hadi 10 Octoba 2017 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili: •  Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza; •  Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika  awamu ya kwanza; •  Waombaji wenye vigezo vya Stashahada  walioshindwa kupata Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN); •  Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge”  mwaka 2017 na matokeo yao yameshatoka; na •  Waliokuwa wana...

PENZI LA ZARI THE BOSS LADY NA DIAMOND PLATINUMZ LAYUMBA VIBAYA

Image
  Ule uhusiano maarufu zaidi Afrika Mashariki wa Diamond Platnumz na Zarina Hassan inaelekea upo katika hatua mbaya ya uhai wake kutokana na yanayoendelea katika mitandao ya kijamii. Katika kipindi cha miezi miwili uhusiano huo umepamba vichwa vya habari kabla na baada ya Diamond kukiri kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto. Hata hivyo, baada ya sekeseke hilo kupita ilionekana huenda hali imekuwa shwari hasa baada ya Diamond kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa Zari, Septemba 23 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Inavyoonekana moto unafukuta ndani kwa ndani kwani tangu juzi wapendanao hao wamekuwa wakifuta picha zao za pamoja katika akaunti zao za Instagram. Pamoja na kufuta picha, Zari anaonekana kurusha vijembe katika mtandao wa Snapchat akisema hawezi kufanywa mjinga katika mitandao ya kijamii. Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa Diamond, mashabiki walisubiri kwa hamu kuona atakachoandika Zari kama ilivyo kawaida yake lakini ilipita kimya. Wengi wametafsiri kuwa pamoja...

IGP Sirro Kuhusu Miili Iliyookotwa Coco Beach

Image
IGP Simon Sirro. MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amesema wameunda timu ya wataalamu kuchunguza miili iliyookotwa na sampuli kutoka miili hiyo zimechukuliwa. Amesema iwapo kuna watu ambao ndugu zao wamepotea ni vyema wakafika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa ajili ya vipimo na kufanyika upelelezi. “Bahari ni kubwa inapita katika nchi nyingi na inachukua kila kitu, haya mambo yanapotokea hata nchi nyingine yanatokea, kwa hiyo kimsingi tumeunda timu ya wataalamu ya kupeleleza kuhusu miili hii, wamechukua majimaji kutoka mwilini,” alisema. IGP Sirro alisema, “Kama kuna mtu ambaye ndugu yake amepotea afike makao makuu ya Polisi upande wa DCI tuweze kufanya uchunguzi kuona kama ni ndugu yake.” Alisema miili hiyo haijabainika kuwa ni ya watu wa Taifa gani. “Tatizo letu Watanzania ni kwamba moja kwa moja wanaanza kuhisi, sijui kwa nini tunakuwa tunaishi kwa hisia na hii hisia hisia si nzuri, tuseme kitu tukiwa na uhakik...

ACT- WAMJIBU RAIS MAGUFULI ISHU YA KUTOONGEZA MISHAHARA

Image
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, akizungumza na  waandishi wa habari. CHAMA cha Act-Wazalendo kimesikitishwa  na kauli ya Rais Magufuli aliyoitoa jana kwenye ufunguzi wa mkutano wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) kuhusu mishahara ya wafanyakazi aliposema  alipoingia madarakani hakusema ataongeza mishahara kwa vile hakuchaguliwa kuongeza mishahara na kwamba ana jukumu la kuwahudumia wananchi. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ACT Wazalendo,  Ado Shaibu, alisema: “Swali la kujiuliza baada ya kauli hiyo ni, je, wafanyakazi wa Tanzania wanastahili kufanyiwa hivi na serikali wanayoihudumia? Jibu bila shaka ni hapana.  Serikali inatoa wapi ujeuri wa namna hii dhidi ya wafanyakazi nchini wakati kiuzalishaji na kimapato inawategemea wafanyakazi? “Licha ya mchango wao madhubuti katika ujenzi wa taifa kwenye sekta mbalimbali, kwa utumishi wao wa kutukuka, ukwel...

NASSARI: Maisha Yangu Yapo Kwenye Bonde la Uvuli wa Mauti

Image
Nassari na Lema. MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA) Joshua Nassari amefunguka na kusema maisha yake yapo hatarini na kudai kuwa watu ambao amewaanika kwenye sakata la ununuzi wa madiwani wanamtafuta. Nassari amesema hayo ikiwa imepita siku moja toka alipokwenda kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupeleka ushahidi wake juu ya madiwani wa CHADEMA waliohama chama kwa kuhongwa rushwa na wateule wa Rais John Pombe Magufuli. “Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti, Maisha yangu yapo hatarini kwani Watesi wetu wananitafuta” aliandika Nassari kupitia ukurasa wake wa Facebook. Mbali na hilo wachangiaji mbalimbali kwenye ukurasa wa Mbunge huyo walimtaka azidi kumuomba Mungu huku wakimshauri kuongeza ulinzi zaidi katika maisha yake ya kila siku kutokana na jambo ambalo ameliibua na kumtaka aendelee kupambana, baadhi ya wachangiaji wengine wamedai kuwa anachofanya ni njia ya kujitafutia umaarufu kisiasa. Juzi  M...

Rais Magufuli Amwagia Sifa Makonda..Adai Hata Kama Hajui Kusoma Lakini Kama Anashika Madawa ya Kulevya Kwake ni Msomi Mzuri

Image
        Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemsifia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kupambana vita dhidi ya dawa za kulevya aliyoianzisha huku akitaka viongozi wengine kuiga mfano wa kiongozi huyo . Rais Magufuli amesema hayo kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam ambapo amemtaka Waziri mkuu, Kassim Majaliwa kuwaambie wakuu wa Mikoa wengine kujifunza kwa Makonda. “RC wa Dar es salaam alipojaribu kusema kuhusu dawa za kulevya kelele zikawa nyingi kweli, mara ooh hajasoma. Mimi hata kama hajui ‘a’ lakini kama anashika madawa ya kulevya huyo ni msomi mzuri,” alisema Rais Magufuli. Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa wakati anaanza Urais alitoa milioni mbili kwaajili ya ujenzi wa darasa mkoa wa Dar es salaam, hivyo amemtaka Mkuu wa mkoa huyo kujiandaa maana ataenda kukagua.

Kortini Kwa Kusambaza Uongo Kuhusu Mazungumzo ya Serikali na Acacia

Image
Obadia Frank alipofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. MKAZI wa Chato mkoani Geita, Obadia Frank (41), mapema leo  amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook kuhusu mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia. Akisomewa  hati ya mashtaka na wakili wa serikali, Leonard Challo, amedai mshtakiwa huyo ambaye ni wakala wa Bayport ametenda  kosa hilo Agosti 8 mwaka huu, katika Wilaya ya Chato mkoani Geita. Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri, kuwa siku hiyo mshtakiwa alichapisha taarifa kupitia ukurasa wake wa Facebook uliokuwa ukihusiana na mazungumzo kati ya serikali na kampuni ya Acacia. Mshtakiwa huyo anadaiwa kusambaza maneno kuwa “Taarifa kutoka  kikao cha mazungumzo kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Acacia kuwa wanasheria wa upande wetu wanashindwa kutafsiri baadhi ya vifungu vya sheri...