Posts

JAMAA ALIYEOA NG,OMBE INDIA MAZITO YAFICHUKA ,SIRI NZITO NDANI YAKE

Image
GUJARAT, INDIA - MARCH, 2016: Arjun, a bull, is dressed and made ready for his wedding to Poonam, a cow, in Ahmedabad city in Gujarat, India. The wedding of Poonam (cow) and Arjun (bull) was solemnised by priests according to Hindu rituals. Vijay Parsana, 44, organized a grand wedding for his Gir cow, Poonam with Arjun, a bull. He spent lakhs to adorn the cow in a sari and gold jewellery. To welcome the first offspring of the cow the 'parents' of the bull came with sweets as the calf named Saraswati turns one month old. Pictures supplied by: Cover Asia Press Unaambiwa ukistaajabu ya Musa, utaona ya firauni! basi firauni kapatikana. Baba mmoja mfugaji nchini India amewatelekeza mkewe na binti zake wawili kwa kudai kuwa hana furaha kuishi nao kwenye nyumba moja na kuamua kufunga ndoa ya kifahari na Ng’ombe. Baba huyo aliyetambulika kwa jina la Vijay Parsana (44) amechukua uamuzi huo baada ya kukosa faraja kutoka kwa mkewe akidai kunyanyaswa na familia yak...

GIGY MONEY,AUNT LULU WAZUA GUMZO,WALINENEPA SASA ‘WAMEPUKUTIKA’

Image
Gift Stanford ‘Gigy Money’. KUNA mastaa ambao walijikuta wakiwaacha wengi midomo wazi kutokana na kuwa na miili iliyoshiba lakini ghafla wakaonekana katika muonekano tofauti wakiwa ‘wamepukutika’ na kuzua viulizo, huku wengi wao wakitoa visingizio mbalimbali. GIGY MONEY Mwanadada huyu anayejulikana kwa jina halisi la Gift Stanford alitikisa mno kwa muonekano wake, jinsi alivyokuwa amenona na kujazia kwenye msambwanda, lakini kitu kilichowaacha wengi hoi ni baada ya kupukutika ghafla, huku sababu mbalimbali zikitajwa, ikiwemo kuharibika kwa mimba kadhaa na `stress’ za mapenzi na hadi sasa mwili wake haujarudi. Amanda Poshy AUNTY LULU Ni moja ya wadada ambao walikuwa gumzo kila kona, huku mara kadhaa akijitapa kuwa wowowo lake ndo kila kitu maishani mwake, lakini siku chache zilizopita mwanadada huyo aliibua taharuki baada ya kuonekana akiwa modo na kalio limeiisha, huku akidai ni kutokana na kufanya mazoezi, hivyo mpaka sasa hajarudi kwenye ubora wake. ...

ANGALIA DIAMOND PLATINUMS NA WCB WASAFI WALIVYOFANYA KUFURU JANA USIKU

Image
officialbelaire for Life! @sallam_sk ….. TABATA KINYEREZI Kinyerezi @wcb_wasafi iko hapo Leo! Tuseme #Hallelujah!    

LEMA NA NASSARI WAANIKA USHAHIDI WA MADIWANI WA CHADEMA WALIVYONUNULIWA

Image
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakijadiliana. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, leo wamewasilisha ushahidi wa jinsi madiwani wa Chadema waliotangaza kukihama chama hicho na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), walivyohongwa ili wachukue uamuzi huo. Wakizungumza na waandishi wa habari, Lema na Nassari wameonesha ushahidi wa video na sauti, ukiwahusisha mkuu wa Wilaya ya Arumeru, katibu tawala na mkurugenzi wa wilaya hiyo, walivyokuwa wakipanga michakato ya kuwanunua madiwani hao. Kwa mujibu wa Lema na Nassari, madiwani hao, kila mmoja amepewa fedha ambazo walitakiwa kulipwa posho kwa vikao vyote walivyotakiwa kukaa mpaka 2020 wakiwa madiwani, wamesaidiwa miradi yao mbalimbali nakila mmoja amepewa shilingi milioni kumi. see more at :- https://youtu.be/yTbqJUmZeag

Hatimaye Zamaradi Mketema wa Clouds Aolewa!

Image
Mtangazaji wa Kipindi cha Take One kinachorushwa na Clouds TV, Zamaradi Mketema akiwa katika pozi la kimahaba na mume wake baada ya kufunga ndoa. Zamaradi na mumewe wakiongea jambo kwa furaha. Shangwe zikiendelea. Mtangazaji wa Kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds, Zamaradi Mketema amefunga ndoa na mwanaume anayetajwa kuwa mtoto wa kigogo mmoja mkubwa wa serikali. Picha za wawili hao wakifunga ndoa, zilipoanza kuzagaa mitandaoni, zilizua gumzo kubwa ambapo baadhi ya watu walidai kuwa si picha za ndoa bali ni filamu huku wengine wakidai kwamba ni ndoa halisi. Habari zaidi kuhusu ndoa hiyo, endelea kutembelea mtandao huu na kusoma magazetila Global Publishers.

Nyumba ya Professor Jay Yabomolewa, Afunguka Mazito

Image
Kushoto ni muonekano wa nyumba ya Professor Jay baada ya kubomolewa. Mbunge wa Mikumi Mjini, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amekumbwa na zoezi la bomoa bomoa linaloendelea maeneo ya Kimara, jijini Dar es salaam kwa kuvunjiwa nyumba yake huku akieleza kuwa uvunjaji huo haukufuata sheria. Professor Jay akithibitisha taarifa hizo kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii amesema zoezi hilo limefanyika wakati yeye akiwa jimboni kwake na mbaya zaidi hakupewa taarifa na zoezi hilo limeendeshwa jioni ambapo sio muda wa kazi kiserikali. Mbunge wa Mikumi Mjini, Joseph Haule maarufu kama Professor Jay. “Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu. Sijawahi kuumia kiasi hiki, nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyowe...

China Yaipatia Tanzania Msaada Wa Sh. Bilioni 29.4

Image
Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Shilingi 29.4bilioni kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu, utalii wa kijiolojia na kuukarabati Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Makubaliano ya msaada huo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango  Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Haodong. Katibu huyo amesema 22.4bilioni  zitatumika kujenga Chuo cha Ufundi Stadi-VETA wilayani Ngara mkoani Kagera. “Fedha hizo zitatumika kujenga vyumba 19 vya madarasa, ujenzi wa karakana 9 za kutolea mafunzo ya elektroniki, ufundi bomba, useremala, ufundi uashi na upakaji rangi” amesema   James Ameeleza kwamba  kiasi hicho pia kitatumika kujenga majengo ya utawala, mabweni, nyumba za walimu na miundombinu mingine itakayosaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwenye chuo hicho. “Tunaamini kwamba msaada huo utakuwa sehemu ya kusaidia jitihada za Serikali za kuj...

Serikali Yalifungia Gazeti la Raia Mwema kwa Kuandika Taarifa za Uongo Kuhusu JPM

Image

Aliyeandika Uongo WhatsApp Kuhusu Polisi Kuonekana Hospitali ya Nairobi

Image
MKAZI mmoja wa Kigamboni, Mbutusyo Mwakihaba (40), amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kusambaza ujumbe katika mtandao kwamba kachero wa Usalama wa Taifa ameonekana jijini Nairobi karibu na hospitali aliyolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu. Mbutusyo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa. Wakili wa Serikali Janeth Magoho alidai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kusambaza taarifa za uongo chini ya kifungu namba 16 cha Sheria ya mtandao namba 4 ya mwaka 2015. Janeth amedai Septemba 11, mwaka huu kupitia mtandao wa ‘WhatsApp’ mshtakiwa aliandika “Huyu ni Kachero wa Usalama wa Taifa anatambulika kwa jina la Jose anaonekana Nairobi karibu na hospitali alikolazwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu…Mwaxcheni mwenzenu” . Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo, upelelezi wa kesi haujakamilika ambapo Hakimu Nongwa alikubali kumpa dhamana kwa masharti ya ku...

Magazeti Ya Tanzania Leo Jumamosi, Septemba 30, 2017

Image