Posts

Mke wa Lissu aamua kufunguka

Image
Nairobi. Kwa mara ya kwanza, Alicia Magabe ambaye ni mke wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia tukio la mumewe kushambuliwa kwa risasi na kudokeza kwamba haliwezi kuwa limetokana na sababu nyingine isipokuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya. Pia amezungumzia kuhusu afya yake na kueleza kuwa bado siyo nzuri na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombea. Mbali ya Alicia ambaye pia ni mwanasheria, dereva wa Lissu naye amezungumza akisema ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo huku akiahidi kuripoti polisi mara baada ya kurejea nchini. Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu alipopelekwa huko baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari nje ya nyumba yake mjini Dodoma mchana wa Septemba 7 akitokea bungeni. “Watanzania wote wanajua Lissu maisha yake yote amekuwa ni mtetezi wa wanyonge na tukio hili amelipata kutokana na kazi zake hizo hivyo nawaomba tumuombee tu,” alise...

NACTE: MAOMBI MAPYA AWAMU YA PILI KWA DIPLOMA NA CHETI YAMESHAANZA KUPOKELEWA

Image
ATTENTION Please read carefully the information in this page before attempting to do anything. WELCOME TO STUDENT’S ADMISSION VERIFICATION SYSTEM Welcome to Student’s Admission Verification System for Certificate and Diploma Applicants. The System allows you to apply for Admission for Further Education in Certificate and Diploma programmes for  academic year 2017/2018 . Currently Available Application Categories:- – Admission Verification for Certificate/DiplomaHealth and Allied Sciences (Including Community Health, Health Records etc) :-  Deadline 01/10/2017 Mafunzo ya Ualimu :-  Deadline 01/10/2017   IMPORTANT NOTES: You are advised to select your most preferred category according to prior qualifications that you hold, because your selection depends on your choices and qualifications. To proceed with the this application you must have the following 1. Valid and Working Email Address2. Valid Phone Number3. Payment Mpesa Confirmation Co...

CHUO CHA TUMAINI JIPYA MAFINGA KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO

Image
 MKUU WA CHUO CHA AFYA CHA  TUMAINI JIPYA MAFINGA ANA FURAHA KUWATANGAZIA KUWA CHUO KIMEANZA KUPOKEA MAOMBI YA MASOMO KWA MWAKA WA MASOMO 2017/18 KATIKA KOZI ZIFUATAZO.                                                      1. CERTIFICATE IN CLINICAL MEDICINE YAANI TABIBU MSAIDIZI KWA MIAKA MIWILI Sifa za mwombaji: Awe na ufaulu wa kidato cha nne kwa angalau alama D nne yakiwemo masomo ya sayansi yaani Fizikia (Physics), Kemia (Chemistry) na Baolojia (Biology) 2. CERTIFICATE IN COMMUNITY HEALTH (Uhudumu wa afya ngazi ya jamii) MWAKA MMOJA Sifa za mwombaji: Awe na ufaulu wa kidato cha nne kwa angalau D nne likiwemo somo la Baolojia (Biology) MUHULA MPYA UTAANZA MWEZI SEPTEMBA, 2017. YOTE HAYO YANAZINGATIA MWONGOZO WA WIZARA YA AFYA NA NACTE. CHUO KIMESAJILIWA KWA USAJILI WA KUDUMU KWA NAMBA 144. ADA ZETU NI NAFUU NA ZINALIPWA KWA AWAM...

Mzee Akilimali aliamsha dude Yanga

Image
Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali amemtaka Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Clement Sanga kujiuzulu kwa madai kuwa yeye ndiye chanzo cha matatizo yote yanayotokea ndani ya Klabu hiyo. Mzee Akilimali amesema wamegundua mgomo uliotokea hapo jana kwa wachezaji kutohudhuria mazoezi ni njama iliyopangwa na Sanga wakidai kuwa wachezaji hawajalipwa mishahara yao suala ambalo sio sawa. "Mimi naona tu kwamba Sanga sasa imefikia hapa, ili tufanye vizuri nawasihi Watanzania wote hususani wana Yanga na wapenzi wa Yanga bwana Sanga sasa hivi atamke kujiuzulu, chonde chonde Bwana Sanga iache Yanga watu tuketi pamoja na wewe mwenyewe tuchague viongozi Yanga tusonge mbele" amesema Mzee Akilimali Mzee Akilimali amesema siku moja kabla ya mazoezi alionekana Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sanga akiwa na Nahodha wa Timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' pamoja na Mshambuliaji wa Kimataifa Thaban Kamusoko ambapo baada ya kutoka hap...

Irene Uwoya: Napenda mwanaume mwenye sura ya kiume

Image
MWIGIZAJI maarufu wa kike wa filamu za Bongo anayeitingisha Bongo Movie ambae pia aliwahi kuolewa na mcheza soka kutoka Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’, mlimbwende Irene Uwoya, amesema kuwa mpenzi wake wa sasa ana ngeu nyingi mwilini mwake kutokana na kuchanwa visu. Uwoya amesema watu kama hao ndiyo anaowataka yeye, kwa sababu inaonyesha uanaume halisi, na si wanaume kuwa laini kama mtoto wa kike. Alipoulizwa juu ya hilo alifunguka: “Sijasema napenda wanaume wenye sura mbaya. Nimesema napenda mwanaume mwenye sura ya kiume, mwanaume uwe na ngeu. Mimi bwana’angu ana ngeu za kuchanwa visu, viwembe na nahisi hata bunduki zimemkosakosa,” alisema Irene Uwoya Mwigizaji huyo kwa sasa hajaweka wazi mahusiano yake tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake, msanii wa Bongo Fleva, Msami Baby, na amesema hataweka tena mahusiano yake wazi. NA : SAMSON JEREMIAH/GPL

Rais Magufuli Azindua Barabara Mererani Mkoa Wa Manyara Leo

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera alipowasili kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia maelfu ya wananchi alipowasili Mererani kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa Mererani wakati wa kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe M...

Miili ya Ndugu 13 Waliofariki kwa Ajali Uganda Ilivyoagwa Dar (Pichaz)

Image
Wanajeshi wa JWTZ wakibeba miili ya marehemu hao kupeleka eneo maalum kwa ajili ya kuaga. SIMANZI, vivlio na majozni imetawala wakati wa kuaga miili ya Watanzania 13 ambao ni ndugu wa familia moja waliofariki kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea nchini Uganda hivi karibuni. Waziri Angella Kairuki akiteta jambo na Betty Kamya ambaye ni mwakilishi wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. Miili ya wanafamilia hao imeagwa leo Septemba 20, 2017 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kuelekea Arusha, Kilimanjaro na Mpwapwa kwa ajili ya mazishi. Waombolezaji wakati wa shughuli ya kuaga marehemu. Katika ibada hiyo ya kuwaaga marehemu, viongozi mbalimbali wa serikali walikuwepo wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala), Angela Kairuki, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijage, Waziri Maalum wa Kusimamia Jiji la Kampala, Betty Kamya kutoka Uganda aliyemwakilisha Rais wa nch...

Serikali Yatangaza Nafasi za Ajira kwa Walimu wa Shule za Msingi

Image

RAIS MAGUFULI ALIAGIZA JESHI LA WANANCHI KUJENGA UKUTA ENEO LA TANZANITE

Image
              Rais John Magufuli. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Wananchi (JWTZ)kushirikiana na Suma JKT kujenga ukuta eneo lenye madini ya Tanzanite wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 20, 2017 akiwa ziarani mkoani Manyara alipowahutubia wananchi wa Simanjiro akizindua Barabara ya Lami kutoka Kia hadi Mererani. Nchi hii ni tajiri, tulipewa madini na Mungu ambayo hayapatikani nchi yoyote, lakini hayatusaidii sisi na tunapata shida. Kwa nini tupewe Tanzanite, tena Simanjiro pekee halafu wanachi wapate shida za maji na barabara? Kwa nini tuibiwe? Kwani Mungu alifanya makosa kutupa hayo madini? Haiwezekani, tuanze kubadilika sasa. “Tatizo letu sio vyama, bali ni vipi tunatumia rasilimali zetu. Tanzanite ingekuwa nchi nyingine, hapa pangekuwa kama Ulaya. Ipo siku Tanzanite haitakuwepo, tutaachiwa mashimo tu! Hakuna ha...

Majibu ya Ndugai kwa Lema kuhusu lissu

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amejibu tuhuma za mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, na kumtaka asipotoshe wananchi, bali apeleke malalamiko yake kwenye kamati. Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiendesha bunge, na kusema kwamba bunge lina utaratibu wake kwenye kila jambo linalohusika bungeni hapo. "Lema asipotoshe wananchi aende hadharani kwenye kamati kuzungumzia hayo, bunge haliwezi kusimama kwa shambulio la Lissu bali kanuni zinasema mbunge akifariki bunge linasimama kwa siku moja. Na iwapo Spika akiletewa jambo la maadili linapelekwa kamati ya maadili, suala la jinai linapelekwa polisi", amesema Spika Ndugai Pia Spika Ndugai amesema suala la Tundu Lissu kuchangiwa fedha za matibabu na wabunge wakati yeye alitibiwa nje ya nchi ni kwamba matibabu ya Tundu Lissu yameenda kinyume na utaratibu wa bunge. "Wabunge wanaopelekwa nje (India) wanapewa rufaa kutoka hospital ya Muhimbili lakini si kama alivyop...

Breaking News: Mahakama ya Kisutu yamuachia huru Yusuph Manji

Image
KISUTU: Mahakama imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo ikionyesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yake. Manji na watuhumiwa wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya serikali. Watuhumiwa wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

JESHI LA POLISI DODOMA LASIKITISHWA NA KITENDO CHA DEREVA WA TUNDU LISSU KUTOFIKA POLISI

Image
        Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ameeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutokufika polisi na kutoa maelezo yake. Kamanda Muroto amesema hayo leo Jumatano wakati akijibu swali la upelelezi unaendeleaje kuhusu tukio hilo. Amesema upepelezi unaendelea kuhusu tukio la Lissu kupigwa risasi na watu mbalimbali wanaendelea kuhojiwa wakiwemo wamiliki nane wa gari aina ya Nissan ambazo zilikamatwa kuhusiana na shambulizi hilo. Wamiliki wa gari tumewahoji na tunapogundua hakuna muunganiko wowote basi tunaachana nao maana hakuna haja ya kuendelea kuwashikilia au kushikilia gari hizo,” amesema.Hata hivyo Kamanda Muroto amesema anasikitishwa na kitendo cha aliyekuwa dereva wa mbunge huyo wakati wa tukio kutoonyesha ushirikiano kwa jeshi la polisi. Tunasikia yupo nje ya nchi na hadi leo hajaitikia wito wa kufika polisi kupata maelezo yake ambayo yangesaidia katika upepelezi wa t...

“Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani yetu”: Waziri Mkuu

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ipo salama na imara na kwamba mtu yeyote atakayejaribu kutaka kuvuruga amani atachukuliwa hatua kali za kisheria. Ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Septemba 13, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Bw. Mousa Farhang jijini Dar es Salaam. “Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote kutoka popote atakayejaribu kuvuruga amani yetu. Nawaomba wananchi muwe makini na muendelee kuidumisha amani yetu.” Amesema kwa sasa Serikali ipo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi, rushwa, biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na wahujumu uchumi. Waziri Mkuu amesema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, wameendelea kuwahamasisha wananchi wake kudumisha mshikamano. Amesema mbali ya kuimarisha amani nchini, pia Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija. Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribis...

Lusekelo: Tusimtumie Lissu kupata umaarufu

Image
 Mchungaji Lusekelo ameandika ujumbe huo kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mbona watu hao hawakuonekana kulaani mauaji ya Kibiti au kuitisha maombezi baada ya watu Kibiti kuuawa. "Tusitumie tatizo la ndugu yetu Tundu lissu kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini, mtu yeyote ambaye anatumia tukio hili kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini namfananisha na wale wahuni ambao basi likianguka anaenda kuchukua simu kwanza, ni jambo ovu sana wewe unakuwa ni sehemu ya watu walio mpiga risasi Tundu lissu. Mwenzako anaumwa wewe unatumia ugonjwa wake kujipatia umaarufu wa kidini au wakisiasa ni jambo baya sana, mbona sikusikia wakilaani mauaji ya kibiti au kuitisha maombezi watu wakibiti walipo uwawa, mbona hawaja laani utekaji na mauaji ya watoto Arusha hata wa Marekani (umoja wa ulaya) sikusikia wanalaani mauaji ya kibiti" aliandika Mzee wa Upako Aidha Mchungaji huyo amesema kuwa yeye anaamini watu hao wanatumia matatizo ya Tundu Lissu...

Man U, PSG, Barcelona na Chelsea Zaua Ligi ya Mabingwa Ulaya

Image
Mchezo ukiendelea wa Ligi ya Mabingwa Ulaya  Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Manchester na Basel. MANCHESTER United imerejea kwa nguvu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Basel, kama ilivyo kwa wababe wa Hispania, Barcelona waliopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus. Msimu wa 2017/18 wa michuano hiyo hatua ya makundi ulifunguliwa usiku wa kuamkia leo ambapo kulikuwa na mechi nyingi kwenye viwanja tofauti huu vigogo wengi wakiibuka na ushindi. Fellaini akishangilia baada ya kutupia bao la kwanza kwa Man Utd. MANCHESTER UNITED 3- 0 BASEL Ikicheza kwenye uwanja wake wa Old Traff ord, United ilipata ushindi huo muhimu katika Kundi A, mpira ukiwekwa wavuni na Marouane Fellaini dakika ya 35 na Romelu Lukaku dakika ya 53, mabao yote yakifungwa kwa kichwa huku Marcus Rashford akitokea benchi na kuifungia timu yake bao la tatu. Katika mchezo huo, kiungo wa United, Paul Pogba aliyekuwa nahodha wa kikosi chake aliumi...

BREAKING NEWZ: Mchekeshaji MC Pilipili amepata ajali

Image
Taarifa zilizoifikia muda huu kuhusiana na mchekeshaji MC Pilipili amepata ajali ya gari akiwa katikati ya  Nyasamba na Bubiki mkoani  Shinyanga . MC Pilipili amepata ajali akiwa kwenye garia aina ya Prado na kukimbizwa hospitali, kwa matukio na habari zaidi zinafuatilia kwa ukaribu ili kuweza kukuletea habaria kamili.

ANGALI PICHA WEMA SEPETU AKIWA MAHAKAMANI KWENYE KESI YAKE,SHAHIDI AFICHUA ALIPOIKUTA BANGI

Image
                    Wema Sepetu akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu MKaziKisutu Dar. Wema na mama yake wakielekea kupanda gari. SHAHIDI upande wa serikali kesi ya Wema Sepetu kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya amesema msokoto wa bangi ulikutwa ukiwa kabatini jikoni kwake. Hayo yamesemwa na ofisa wa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Willy akimweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula. Inspekta Willy anakumbuka Februari 4, mwaka huu aliitwa na mkuu wake wa kazi na kupewa jukumu la kufanya upekuzi nyumbani kwa              Wema Sepetu ambapo aliongozana na maofisa wenzake hadi nyumbani anakoishi huko Ununio jijini Dar es Salaam. Alisema baada ya kufika nyumbani kwa Wema walimkuta mfanyakazi wake wa ndani wa kike ambaye walimuomba waonane na mjumbe wa shina wa maeneo hayo ambapo baada ya kufanikwa ...