Posts

Mzee Akilimali aliamsha dude Yanga

Image
Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali amemtaka Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Clement Sanga kujiuzulu kwa madai kuwa yeye ndiye chanzo cha matatizo yote yanayotokea ndani ya Klabu hiyo. Mzee Akilimali amesema wamegundua mgomo uliotokea hapo jana kwa wachezaji kutohudhuria mazoezi ni njama iliyopangwa na Sanga wakidai kuwa wachezaji hawajalipwa mishahara yao suala ambalo sio sawa. "Mimi naona tu kwamba Sanga sasa imefikia hapa, ili tufanye vizuri nawasihi Watanzania wote hususani wana Yanga na wapenzi wa Yanga bwana Sanga sasa hivi atamke kujiuzulu, chonde chonde Bwana Sanga iache Yanga watu tuketi pamoja na wewe mwenyewe tuchague viongozi Yanga tusonge mbele" amesema Mzee Akilimali Mzee Akilimali amesema siku moja kabla ya mazoezi alionekana Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sanga akiwa na Nahodha wa Timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' pamoja na Mshambuliaji wa Kimataifa Thaban Kamusoko ambapo baada ya kutoka hap

Irene Uwoya: Napenda mwanaume mwenye sura ya kiume

Image
MWIGIZAJI maarufu wa kike wa filamu za Bongo anayeitingisha Bongo Movie ambae pia aliwahi kuolewa na mcheza soka kutoka Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Katauti’, mlimbwende Irene Uwoya, amesema kuwa mpenzi wake wa sasa ana ngeu nyingi mwilini mwake kutokana na kuchanwa visu. Uwoya amesema watu kama hao ndiyo anaowataka yeye, kwa sababu inaonyesha uanaume halisi, na si wanaume kuwa laini kama mtoto wa kike. Alipoulizwa juu ya hilo alifunguka: “Sijasema napenda wanaume wenye sura mbaya. Nimesema napenda mwanaume mwenye sura ya kiume, mwanaume uwe na ngeu. Mimi bwana’angu ana ngeu za kuchanwa visu, viwembe na nahisi hata bunduki zimemkosakosa,” alisema Irene Uwoya Mwigizaji huyo kwa sasa hajaweka wazi mahusiano yake tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake, msanii wa Bongo Fleva, Msami Baby, na amesema hataweka tena mahusiano yake wazi. NA : SAMSON JEREMIAH/GPL

Rais Magufuli Azindua Barabara Mererani Mkoa Wa Manyara Leo

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera alipowasili kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia maelfu ya wananchi alipowasili Mererani kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa Mererani wakati wa kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani mkoani Manyara leo Septemba 20, 2017. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe M

Miili ya Ndugu 13 Waliofariki kwa Ajali Uganda Ilivyoagwa Dar (Pichaz)

Image
Wanajeshi wa JWTZ wakibeba miili ya marehemu hao kupeleka eneo maalum kwa ajili ya kuaga. SIMANZI, vivlio na majozni imetawala wakati wa kuaga miili ya Watanzania 13 ambao ni ndugu wa familia moja waliofariki kwenye ajali mbaya ya gari iliyotokea nchini Uganda hivi karibuni. Waziri Angella Kairuki akiteta jambo na Betty Kamya ambaye ni mwakilishi wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. Miili ya wanafamilia hao imeagwa leo Septemba 20, 2017 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam na baadaye kusafirishwa kuelekea Arusha, Kilimanjaro na Mpwapwa kwa ajili ya mazishi. Waombolezaji wakati wa shughuli ya kuaga marehemu. Katika ibada hiyo ya kuwaaga marehemu, viongozi mbalimbali wa serikali walikuwepo wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala), Angela Kairuki, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles John Mwijage, Waziri Maalum wa Kusimamia Jiji la Kampala, Betty Kamya kutoka Uganda aliyemwakilisha Rais wa nch

Serikali Yatangaza Nafasi za Ajira kwa Walimu wa Shule za Msingi

Image

RAIS MAGUFULI ALIAGIZA JESHI LA WANANCHI KUJENGA UKUTA ENEO LA TANZANITE

Image
              Rais John Magufuli. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Wananchi (JWTZ)kushirikiana na Suma JKT kujenga ukuta eneo lenye madini ya Tanzanite wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 20, 2017 akiwa ziarani mkoani Manyara alipowahutubia wananchi wa Simanjiro akizindua Barabara ya Lami kutoka Kia hadi Mererani. Nchi hii ni tajiri, tulipewa madini na Mungu ambayo hayapatikani nchi yoyote, lakini hayatusaidii sisi na tunapata shida. Kwa nini tupewe Tanzanite, tena Simanjiro pekee halafu wanachi wapate shida za maji na barabara? Kwa nini tuibiwe? Kwani Mungu alifanya makosa kutupa hayo madini? Haiwezekani, tuanze kubadilika sasa. “Tatizo letu sio vyama, bali ni vipi tunatumia rasilimali zetu. Tanzanite ingekuwa nchi nyingine, hapa pangekuwa kama Ulaya. Ipo siku Tanzanite haitakuwepo, tutaachiwa mashimo tu! Hakuna haja ya kumung’unya maneno, Tanzani

Majibu ya Ndugai kwa Lema kuhusu lissu

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amejibu tuhuma za mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, na kumtaka asipotoshe wananchi, bali apeleke malalamiko yake kwenye kamati. Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiendesha bunge, na kusema kwamba bunge lina utaratibu wake kwenye kila jambo linalohusika bungeni hapo. "Lema asipotoshe wananchi aende hadharani kwenye kamati kuzungumzia hayo, bunge haliwezi kusimama kwa shambulio la Lissu bali kanuni zinasema mbunge akifariki bunge linasimama kwa siku moja. Na iwapo Spika akiletewa jambo la maadili linapelekwa kamati ya maadili, suala la jinai linapelekwa polisi", amesema Spika Ndugai Pia Spika Ndugai amesema suala la Tundu Lissu kuchangiwa fedha za matibabu na wabunge wakati yeye alitibiwa nje ya nchi ni kwamba matibabu ya Tundu Lissu yameenda kinyume na utaratibu wa bunge. "Wabunge wanaopelekwa nje (India) wanapewa rufaa kutoka hospital ya Muhimbili lakini si kama alivyop

Breaking News: Mahakama ya Kisutu yamuachia huru Yusuph Manji

Image
KISUTU: Mahakama imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji katika kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo ikionyesha kuwa hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yake. Manji na watuhumiwa wenzake watatu walikuwa wakikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya uhujumu uchumi, kukutwa na mihuri miwili ya JWTZ, ukiwemo wa Mkuu wa Kikosi cha 21 JWTZ, wa Mkuu wa Kikosi Makutupora Dodoma (JWTZ) na wa Commanding Officer Korogwe na plate number mbili za magari ya serikali. Watuhumiwa wengine walioachiwa huru kwenye kesi hiyo ni Deogratius Kasinda na Thobias Pwere na mwingine ambaye jina lake halikufahamika mara moja.

JESHI LA POLISI DODOMA LASIKITISHWA NA KITENDO CHA DEREVA WA TUNDU LISSU KUTOFIKA POLISI

Image
        Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ameeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutokufika polisi na kutoa maelezo yake. Kamanda Muroto amesema hayo leo Jumatano wakati akijibu swali la upelelezi unaendeleaje kuhusu tukio hilo. Amesema upepelezi unaendelea kuhusu tukio la Lissu kupigwa risasi na watu mbalimbali wanaendelea kuhojiwa wakiwemo wamiliki nane wa gari aina ya Nissan ambazo zilikamatwa kuhusiana na shambulizi hilo. Wamiliki wa gari tumewahoji na tunapogundua hakuna muunganiko wowote basi tunaachana nao maana hakuna haja ya kuendelea kuwashikilia au kushikilia gari hizo,” amesema.Hata hivyo Kamanda Muroto amesema anasikitishwa na kitendo cha aliyekuwa dereva wa mbunge huyo wakati wa tukio kutoonyesha ushirikiano kwa jeshi la polisi. Tunasikia yupo nje ya nchi na hadi leo hajaitikia wito wa kufika polisi kupata maelezo yake ambayo yangesaidia katika upepelezi wa tukio hilo.”

“Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani yetu”: Waziri Mkuu

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ipo salama na imara na kwamba mtu yeyote atakayejaribu kutaka kuvuruga amani atachukuliwa hatua kali za kisheria. Ametoa kauli hiyo jana (Jumatano, Septemba 13, 2017) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Bw. Mousa Farhang jijini Dar es Salaam. “Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote kutoka popote atakayejaribu kuvuruga amani yetu. Nawaomba wananchi muwe makini na muendelee kuidumisha amani yetu.” Amesema kwa sasa Serikali ipo katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi, rushwa, biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na wahujumu uchumi. Waziri Mkuu amesema licha ya Tanzania kuwa ni nchi ya amani na yenye utulivu wa kisiasa, wameendelea kuwahamasisha wananchi wake kudumisha mshikamano. Amesema mbali ya kuimarisha amani nchini, pia Serikali imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji jambo ambalo litawawezesha watakaokuja kuwekeza nchini kupata tija. Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribis

Lusekelo: Tusimtumie Lissu kupata umaarufu

Image
 Mchungaji Lusekelo ameandika ujumbe huo kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mbona watu hao hawakuonekana kulaani mauaji ya Kibiti au kuitisha maombezi baada ya watu Kibiti kuuawa. "Tusitumie tatizo la ndugu yetu Tundu lissu kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini, mtu yeyote ambaye anatumia tukio hili kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini namfananisha na wale wahuni ambao basi likianguka anaenda kuchukua simu kwanza, ni jambo ovu sana wewe unakuwa ni sehemu ya watu walio mpiga risasi Tundu lissu. Mwenzako anaumwa wewe unatumia ugonjwa wake kujipatia umaarufu wa kidini au wakisiasa ni jambo baya sana, mbona sikusikia wakilaani mauaji ya kibiti au kuitisha maombezi watu wakibiti walipo uwawa, mbona hawaja laani utekaji na mauaji ya watoto Arusha hata wa Marekani (umoja wa ulaya) sikusikia wanalaani mauaji ya kibiti" aliandika Mzee wa Upako Aidha Mchungaji huyo amesema kuwa yeye anaamini watu hao wanatumia matatizo ya Tundu Lissu

Man U, PSG, Barcelona na Chelsea Zaua Ligi ya Mabingwa Ulaya

Image
Mchezo ukiendelea wa Ligi ya Mabingwa Ulaya  Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Manchester na Basel. MANCHESTER United imerejea kwa nguvu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Basel, kama ilivyo kwa wababe wa Hispania, Barcelona waliopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus. Msimu wa 2017/18 wa michuano hiyo hatua ya makundi ulifunguliwa usiku wa kuamkia leo ambapo kulikuwa na mechi nyingi kwenye viwanja tofauti huu vigogo wengi wakiibuka na ushindi. Fellaini akishangilia baada ya kutupia bao la kwanza kwa Man Utd. MANCHESTER UNITED 3- 0 BASEL Ikicheza kwenye uwanja wake wa Old Traff ord, United ilipata ushindi huo muhimu katika Kundi A, mpira ukiwekwa wavuni na Marouane Fellaini dakika ya 35 na Romelu Lukaku dakika ya 53, mabao yote yakifungwa kwa kichwa huku Marcus Rashford akitokea benchi na kuifungia timu yake bao la tatu. Katika mchezo huo, kiungo wa United, Paul Pogba aliyekuwa nahodha wa kikosi chake aliumia da

BREAKING NEWZ: Mchekeshaji MC Pilipili amepata ajali

Image
Taarifa zilizoifikia muda huu kuhusiana na mchekeshaji MC Pilipili amepata ajali ya gari akiwa katikati ya  Nyasamba na Bubiki mkoani  Shinyanga . MC Pilipili amepata ajali akiwa kwenye garia aina ya Prado na kukimbizwa hospitali, kwa matukio na habari zaidi zinafuatilia kwa ukaribu ili kuweza kukuletea habaria kamili.

ANGALI PICHA WEMA SEPETU AKIWA MAHAKAMANI KWENYE KESI YAKE,SHAHIDI AFICHUA ALIPOIKUTA BANGI

Image
                    Wema Sepetu akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu MKaziKisutu Dar. Wema na mama yake wakielekea kupanda gari. SHAHIDI upande wa serikali kesi ya Wema Sepetu kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya amesema msokoto wa bangi ulikutwa ukiwa kabatini jikoni kwake. Hayo yamesemwa na ofisa wa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Inspekta Willy akimweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula. Inspekta Willy anakumbuka Februari 4, mwaka huu aliitwa na mkuu wake wa kazi na kupewa jukumu la kufanya upekuzi nyumbani kwa              Wema Sepetu ambapo aliongozana na maofisa wenzake hadi nyumbani anakoishi huko Ununio jijini Dar es Salaam. Alisema baada ya kufika nyumbani kwa Wema walimkuta mfanyakazi wake wa ndani wa kike ambaye walimuomba waonane na mjumbe wa shina wa maeneo hayo ambapo baada ya kufanikwa kumwona walimweleza shida yao na kuanza kazi ya uchunguzi ili kutafuta dawa za kule

JPM Amjulia Hali Meja Jenerali Mstaafu Aliyejeruhiwa kwa Risasi

Image
Rais Magufuli akimjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini Lugalo. RAIS John  Magufuli leo Jumanne ametembelea Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam na kumjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wakati akiingia nyumbani kwake Ununio, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli akisalimiana na mtoto. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Mritaba alishambuliwa kwa risasi jana  mchana na kisha kupelekwa katika hospitali ya jeshi Lugalo kwa matibabu. Rais Magufuli akimjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini Lugalo. Mkuu wa kituo cha tiba cha hospitali hiyo na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Brigedia Jenerali Paul Massawe amemueleza Rais Magufuli kuwa Mritaba anaendelea vizuri baada ya madaktari kufanikiwa kutoa

Zitto Kabwe amjia juu Spika Job Ndugai

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumjia juu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kusema kuwa anamsikitika sana kama haoni jeshi heshima ya Bunge inavyoshuka. Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuagiza na kuwataka wabunge Zitto Kabwe pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo wamezitoa hivi karibuni. Kufuatia wito huo Zitto Kabwe amesema yeye atafika kwenye kamati hiyo ya maadili na Madaraka ya Bunge kama ambavyo Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza na kusema kuwa spika huyo kama angeweza kujua nguvu yake wala asingehaika na wabunge ambao wanakosoa kwa staha. "Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu kama imefikia haoni heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya Maadili, Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu k

HAMISO MOBETTO AFUNGWA MDOMO,KISA KUZAA NA MSANII

Image
             Hamisa Mobetto. MAMA mzazi wa mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobetto ambaye hivi karibuni alijifungua mtoto anayedaiwa kuzaa na msanii wa Bongo Flava, amecharuka akisema kuwa, japokuwa mtoto wake huyo anapigwa vijembe, lakini kamwe hawatamsikia akisema kwa sababu amemwambia afunge mdomo. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, mama Mobetto alisema kuwa, yeye kama mama anasikia uchungu kuona mwanaye huyo anavyosengenywa, lakini kwa busara amemtaka kutofungua mdomo kujibizana na mtu yeyote kuhusiana na ishu hiyo. Hamisa hatafungua mdomo kuzungumza chochote kuhusiana na mtoto wake na siyo mjinga kunyamaza, ila tu hatutaki malumbano na mtu,” alisema mama Mobetto.

Katibu Mkuu Chadema Ahojiwa Kuhusu ‘Watu Wasiojulikana’

Image
Dk Vincent Mashinji. KATIBU Mkuu wa Chadema , Dk Vincent Mashinji amesema polisi wamemhoji wakitaka kujua kuhusu kauli zake za watu wasiojulikana kama anaweza kuwatambua. “Watu wasiojulikana ambao tulikuwa tunawaongelea ni kwamba, imezoeleka kwa polisi kunapokuwa na tukio kubwa wanasema watu wasiojulikana, kwa hiyo lengo langu lilikuwa ni kuita wananchi  kurudi kwenye Polisi Jamii ili kuondokana na hili la watu wasiojulikana,” alisema Dk Mashinji. Katibu mkuu huyo wa Chadema, leo Jumatatu ameamua kwenda kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini hapa. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene ilisema Dk Mashinji aliambatana na wasaidizi wake kutoka makao makuu ya chama hicho. “Katibu mkuu amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, kuitikia wito wa Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (