Serikali yataifisha magari yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetaifisha jumla ya magari sita yakiwepo magari matatu aina ya Ranger Rover Sports yaliyoingizwa nchini kinyume na sheria baada ya watuhumiwa hao kukiri kuwa wamefanya kosa hilo. Rais Magufuli mwezi Machi mwaka huu alipokwenda bandarini alikuta kuna makontena yenye magari ndani yake huku wamiliki wa makontena hayo wakidai makontena hayo yalikuwa na nguo na mabegi lakini baada ya kufunguliwa zilionekana gari za kifahari zikiwa kwenye makontena hayo, jambo ambalo lilionekana wamiliki wa mahari hayo walikuwa wakiingiza magari hayo kinyume na utaratibu na sheria za nchi. Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, DPP Biswalo Mganga amesema kuwa baada ya mahakama kuwakuta na hatia raia hao wakigeni ambao walidai kuwa kontena hizo zilikuwa na nguo na mabegi wakati ni magari hivyo serikali imetaifisha magari yao na sasa kuwa magari ya serikali. "Rais hao wamekiri makosa yao yote mawili na kutokana na kukiri kwao mahakama ime