Posts

Rais Magufuli Amaliza Bifu la Makonda na Ruge Jukwaani

Image
Paul Makonda akishikana mkono na Ruge Mutahaba. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli , amemaliza bifu kubwa lililokuwepo kati ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuwakutanisha wawili hao jukwaani na kuwataka washikane mikono. Tukio hilo la aina yake, limetokea kwenye Kijiji cha Chongoleani, Tanga ambapo kulikuwa na tukio kubwa la uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda mpaka kwenye Bandari ya Tanga.

SOL CAMPBELL WA ARSENAL ANATUA DAR LEO

Image
Beki wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell. BEKI wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell anatarajiwa kutua nchini leo Jumamosi mchana kwa mwaliko wa Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa.Campbell ambaye pia amewahi kuichezea Tottenham Hotspur ya England, akiwa nchini kesho atajumuika na baadhi ya wadau wa soka kutazama mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Arsenal na Chelsea.Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa, Abbas Tarimba, akiwa nchini Campbellpia atafanya mafunzo kwa timu ya Magnet kwenye Uwanja wa Gymkhana na kutembelea timu ya Muungano. “Huyu ni nyota wa pili wa zamani wa soka baada ya Leon Osman wa Everton, tunajua bado watu wanakumbuka ujio wa Everton huu ni muendelezo wa kampuni yetu kuleta hamasa ya soka nchini,” alisema Tarimba.Tarimba alisema SportPesa inaendelea kuwapa hamasa ya soka Watanzania kwa ujio wa nyota huyo ukiachana na udhamini iliyoutoa kwa Simba, Yanga na Singida United.

Povu la Ndikumana kwa Uwoya Lachafua Hali ya Hewa

Image
Ndikumana na Uwoya. Mwanasoka wa Kimataifa kutoka Rwanda, Hamad Ndikumana ambaye ni mume wa ndoa wa staa wa filamu za Bongo, Irene Uwoya , amekubali kumpa talaka Irene ili andelee na maisha yake baada ya kutengana muda mrefu huku akieleza kuchoshwa na skendo chafu za mke wake huyo. Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Ndikumana ameandika ujumbe akisema amekubali kumpa Irene talaka, hivyo asisubiri hadi afe ili aolewe, ili ampe uhuru anaouhitaji aweze kufanya mambo yake bila yeye kuhusishwa. “Ulilia muda kwamba unataka talaka ili uolewe, sina kipingamizi tafuta kila utakacho ulete nitakusainia, usisubiri nife ili uolewe maana naweza kuishi zaidi ya unavyofikiria, Mungu akusimamie”, aliandika Ndikumana. Wanandoa hao wakitambo wakiwa pamoja. (Picha na Maktaba) Pia Ndikumana amesema kitendo cha Irene kumnyima kuzungumza na mwanae tangu watengane, ni kitendo kinachomuumiza sana, lakini yote anamuachia Mungu. “Ungekuwa na roho ya kibinadamu u

Gwajima Anunua Ndege aina ya JET, Pia kuleta Umeme megawati 250

Image
Baaada ya kimya cha muda mrefu Askofu Mkuu wa kanisa la ufufuo na uzima, Mchungaji Josephat Gwajima ameibuka na kutangaza kuleta ndege aina ya 'Jet' Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma kwa watumishi wake. Mchungaji Gwajima ambaye hivi sasa yupo mjini Birmingham, Alabama nchini Marekani kwa shughuli zake za injili na mikutano mbalimbali ameahidi ataleta ndege aina ya 'Jet' "Muda si mrefu nitaleta Tanzania ndege hii 'Jet' kwa lengo la kukuza falme ya Mungu" alisema Gwajima Mbali na hilo Mchungaji Gwajima akiwa katika ziara zake hizo za kiroho alidai kuwa amepata umeme megawati 250 kutoka nchini Ujerumani ambazo anaamini zitasaidia taifa letu la Tanzania katika kukuza sekta ya viwanda. "Nimepata Umeme Megawati 250 kutoka Ujerumani kwa ajili ya Taifa letu katika juhudi za kuunga mkono Tanzania ya Viwanda. Nilimtuma Engineer Mkuu wa Ufufuo na Uzima Duniani Eng.Yeconia Bihagaze huko Ujerumani kufanya ufuatiliaji, Umeme huu ni k

Hii Ndiyo Sababu ya Lowassa Kumpigia Debe Kenyatta

Image
Rais Kenyatta na Edward Lowassa. Zikiwa zimebaki siku mbili nchi ya Kenya kufanya Uchaguzi Mkuu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amefunguka sababu kuu zinazofanya amtetee na kumnadi mgombea Urais kupitia chama cha Jubilee Uhuru Kenyatta kuwa ni kiongozi shupavu. Lowassa ambaye jana alishiriki katika mkutano wa chama cha Jubilee alisema kuwa kuna watu wanauliza kwanini yeye pamoja na CHADEMA wanamnadi kwa kuwa kiongozi huyo ni shupavu na mpenda watu. “Kuna watu wananiuliza kwanini mnamnadi Uhuru Kenyatta, nasema tena hadharani bila aibu yoyote huyu ni kiongozi shupavu anayependa watu, anaweza kuongoza watu wetu, lakini cha pili Uhuru Kenyatta anapenda Afrika Mashariki akiingia madarakani ataturuhusu tuendelee kuzunguka zunguka kwenye mipaka hii kama Namanga pale bila hata shida, la tatu ni kwamba aliingia madarakani nchi ikiwa kwenye vita lakini amewapa suluhu ameingoza nchi imekwenda taratibu na akafanikiwa” alisema Lowassa. Kenyatta akisim

RWANDA: Rais Paul Aweka Historia Ushindi Urais

Image
Rais Paul Kagame akishangilia ushindi. Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda imemtangaza Paul Kagame kuwa mshindi wa urais wa nchi hiyo katika uchaguzi uliyofanyika jana Ijumaa, Agosti 4. Tume hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais huyo ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 17 sasa, atahudumu muhula wa tatu wa miaka saba baada ya kushinda kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Wafuasi wake wanamsifu Kagame kwa kuonyesha utulivu na maendeleo ya kiuchumi nchini humo baada ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya watu waliuaawa. Kutoka kushoto Paul Kagame, Frank Habineza na Philippe Mpayimana. Wapinzani wa Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana ambao amewaburuza vibaya kwenye matokeo hayo ambapo wapinzani hao wamelalamika kuwa wafuasi wao wamepigwa zengwe ndiyo maana imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya kura. Hata hivyo chama tawala kimekana madai hayo. Rais Kagame aliingia madarakani mwa

RAIS DKT MAGUFULI AMWANDALIA RAIS MUSEVENI WA UGANDA DHIFA YA KITAIFA JIJINI TANGA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakati wa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga. Pamoja nao meza kuu ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli. Hii ikiwa ni bado masaa machache kabla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga. Sehemu ya mawaziri na manaibu waziri wa Tanzania na Uganda wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda Ikulu ndogo jijini Tanga Ijumaa usiku Sehemu ya viongozi mbalimbali wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa za nchi hizo mbili na wa Afrika Mashariki kwenye dhifa ya Taifa aliyoandaa Rais Dkt. Magufuli kwa heshima ya

Jinsi ya kutengeneza SABUNI ya kipande YA KUGANDISHA

Image
Utengenezaji wa sabuni hii una njia nyingi Hatua  ya kwanza Chemsha vipimo 7 vya mafuta ya mawese au mafuta ya shea hadi ifikie hatua ya kimiminika chuja na yaweke kwenye chungu cha mfinyanzi au chombo cha plastiki. Hatua ya pili Pima vipimo 5 vya maji baridi kwenye chombo cha plastiki ongeza kipimo 1cha sodium hydroxide kwa uangalifu mkubwa kwenye maji acha hadi mchanganyiko huo uyeyuke. Subiri mchanganyiko wa sodium hydroxide na mafuta ukaribie kupoa. Hatua ya tatu Taratibu ongeza mchanganyiko wa sodium hydroxide kwenye mawese,huku ukikoroga haraka haraka bila kusitisha ukitumia ubao .hii ni njia nzuri zaidi. Njia ya pili Chemsha mafuta kwenye joto la kadiri ya 55C Changanya maji na sodium hydroxide na uache mchanganyiko huu upoe hadi kufikia joto hilohilo. Baada ya kuandaa mchanyiko wako changanya vimiminika hivyo viwili huku ukikoroga kwanguvu sana kadiri uwezavyo, taratibu sabuni itageuka kuwa laini. Kabla sabuni haijawa ngumu mwaga sabuni ndani ya

NIMEKUWEKEA VICHEKESHO NILIVYOVISIKIA MTAANI: VUNJA MBAVU!

Image
MWALIMU : Alex, simba akianza kukufukuza utafanya nini? Alex: Nitapanda juu ya mti. Mwalimu: Je, na simba naye akipanda juu ya mti? Alex: Nitakimbilia mtoni niogelee. Mwalimu: Je simba naye akikufuata mtoni? Alex: Mwalimu uko upande wangu au wa simba? Maana sikuelewi kabisa, kila ninavyojaribu kumkwepa simba we unamwelekeza niliko, kama hunipendi sema tu. Kama hukuwahi kupata mia darasani usijali, utapata ukiwa unachaji simu. Ukimpa ‘demu’ hela mzazi wake hata hamuulizi, mpe mimba uone, utatafutwa hadi ‘Google’. Kumbe bangi haina madhara… nimetoka kuvuta pafu moja nipo fresh kabisa bila tatizo..saivi nimekaa juu ya tv naangalia makochi. Dua zenu jamani nipo ugenini nimefumwa naongeza maji ya ugali nijitetee vipi? Nimepika ugali ya watu wawili nikakula ya mtu mmoja nikashiba alafu nikatoka nje nikabisha mlango kama mgeni, nikaingia na nikakula iyo ingine! Mwili haijengwi na mbao. Mnamkumbuka yule Subira aliyekuwa anavuta her

WAZIRI MWAKYEMBE AWAPA ‘DAWA’ WASANII BONGO

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wasanii. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe  amewataka  Wasanii wa Muziki wa Kizazi   kipya  nchini kuanzisha mfuko wa wasanii kwa lengo la kutatua changamoto ya udhamini inayowakabili. Ameyasema hayo  Jijini Dar es Salaam  katika kikao kazi na Wasanii hao ambacho kilijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na namna ya kukabiliana nazo hivyo kuwataka kutokata tamaa Amesema kuwa kutokana na malalamiko na changamoto mbalimbali zinazowakabili Wasanii, ambazo nyingi zinasababishwa na mikataba inayowanyonya Wasanii katika kazi zao, ni vema sasa Wasanii hao kupitia Chama chao cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) kuanzisha mfuko ambao utakua unatoa mikopo kwa Wasanii ili kuwezesha utendaji wa kazi zao pasipo kutegemea wadhamini. Dkt. Mwakyembe akisalimiana na wasanii. “Ninafikiri dawa tunayohitaji ni kuanzishe mfuko wa Wa

Ofisa wa tume ya uchaguzi ya Kenya aliteswa na kunyongwa

Image
Uchunguzi uliofanywa kwenye mwili wa aliyekuwa mkuu wa idara ya Tehama ya tume ya uchaguzi ya Kenya Bw Chris Msando, umeonyesha kuwa aliteswa na kuuawa. Kwa mujibu wa mwanapatholojia mkuu wa serikali Dk Johansen Oduor na daktari wa familia Dk Bessie Byakika, mwili wa Bw Msando umeonesha kuwa wauaji walitumia mikono kumnyonga na pia walimpiga na kitu chenye ncha kali na kumsababishia jeraha. Matokeo ya uchunguzi wa kipatholojia umekuwa ni msingi wa uchunguzi kufuatia kifo chake, na tayari watu watatu wametiwa mbaroni kuhusiana na kifo cha Bw Msando, lakini bado haijulikani walihusika vipi na kifo chake. Mwili wa Bw Msando pamoja na wa msichana mwanafunzi mwenye umri wa miaka 21 uliokotwa jumamosi kwenye msitu wa viunga vya Nairobi.

Sakata la Acacia, Bangi Vyawaweka Matatani Wabunge Wawili wa Mara

Image
John Heche. Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche anashikiliwa na Jeshi la Polisi Tarime, huku Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matiko naye akisakwa. John Heche amekamatwa na kushikiliwa na Jeshi hilo kwa madai alizungumza bungeni kuhamasisha wananchi kuzuia shughuli za kampuni ya ACACIA huko Nyamongo, North Mara.   Esther Matiko. Jeshi hilo pia linadai Heche kupitia mkutano wa hadhara alisema atapeleka hoja bungeni ili bangi ihalalishwe kuuzwa nje ya nchi, Polisi wanasema kauli hiyo inachochea ulimaji bangi. Halikadhalika linamsaka Esther Matiko ili kumuunganisha katika madai hayo kuwa alizungumza katika mkutano huo kauli zinazochochea kilimo cha bangi. Polisi wamechukua simu za alizokuwa nazo, pia wameagiza simu nyingine iliyopo Dar es salaam kwenye matengenezo pia ipelekwe Tarime. -Makene

RAIS MUSEVENI AWASILI JIJINI TANGA TAYARI KWA SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI HAPO KESHO

Image
  Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (haonekani pichani) na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani. Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani.

HUU NDIO MUONEKANO WA MFANYABIASHARA YUSUPH MANJI LEO MAHAKAMANI

Image
   August 4,2017 Upande wa serikali umewasilisha pingamizi la awali Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga maombi ya dhamana ya mfanyabiashara Yusuf Manji. Pingamizi hilo limewasilishwa leo na wakili wa serikali, Paul Kadushi mbele ya Naibu Msajili, Sian Mustafa kutokana na Jaji Isaya Arufan anayesikiliza maombi hayo kutokuwepo. Katika pingamizi hilo, wakili Kadushi amedai kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana ya Manji. Pia kiapo kilichowasilisha cha kuhusu dhamana kinadosari kisheria, pamoja na kuwepo kwa vifungu visivyo sahihi. Baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, Msajili Mustafa ameahirisha kesi hiyo hadi August 7/2017 kwa ajili ya kusikilizwa. millardayo.com  imezinasa picha hizi ambazo zinamuonesha Mfanyabiashara Yusuph Manji akiwa amefuga ndevu ikiwa ni tofauti na ambavyo amekuwa akionekana.                  

Polisi limetangaza Msako mkali kuanzia jumatatu kwa wafanyabiashara wa TV, Simu na Computer “USED”

Image
Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm limetangaza Msako mkali kuanzia jumatatu ijayo kwa wafanyabiashara na wauzaji wa television,Computer na simu za Mkononi zilizotumika maarufu Used’ baada ya kubaini katk maduka hayo kumekuwa maficho ya mali zinazoibiwa katika maeneo mbali mbali jijini dsm. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm Kaimu Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dsm Lucas Mkondya amesema katika miezi ya hivi karibu kumeibuka wizi wa Uvunjaji majumbani ambao wahalifu huchuku Tv hasa zile Flat screen ambapo jeshi hilo limebaini hupelekwa katika maduka hayo. Jeshi hilo pia litawakamata watu wote wanaoendesha biashara ya magari yasiokuwa katika yard katika maeneo ya jiji la Dsm. Aidha jeshi hilo pia kuanzia jumatatu litaendesha Msako wa Kukamata magari yote yenye Vioo vyeusi maarufu TINTED baada ya kubaini kuwa baadhi ya wahusika hujihusisha na Uhalifu na Uporaji,kuficha mali za wizi lakini pia kufanyia vitendo visivyofaa vya Uzinzi. Akizungumzia matukio y

Wanaomuua Jini Kabula Wajulikana!

Image
WAKATI hali ya staa wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ikiwa bado si shwari, watu ambao wanatajwa kuzidi kumuweka kwenye wakati mgumu na kumsukumizia kwenye kifo wamejulikana, Ijumaa linakupa habari hii ya kusikitisha. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Jini Kabula anayedaiwa kuwa na tatizo la kuchanganyikiwa, alisema anashangaa wakati yuko kwenye matatizo hayo mazito ndipo ndugu na marafiki zake wanamtenga, hali ambayo inaweza kukatisha uhai wake. Alisema anapitia kwenye changamoto nzito kimaisha ambapo anahitaji msaada kutoka kwa watu wake wa karibu lakini kinachomsikitisha ni kwamba, anakimbiwa na kupewa kila aina ya jina baya likiwemo la kuitwa kichaa. “Nimeteswa na kuumizwa sana, eti mimi naitwa kichaa, kweli mimi naweza kuwa kichaa, ama kweli hii dunia ni katili sana na kwa hali hii nitakufa. “Naomba ifahamike kwamba nina matatizo makubwa sana, napitia mateso mazito, nimetengwa na watu wananikimbia, hata wale ambao tulikuwa tunasaidiana