HISTORIA YA MUUZA MADAWA YA KULEVYA NGULI DUNIANI PABO ESCOBAR
Katika milima inayotazamana na mji wa Medellín nchini Colombia, yapo majengo ya kifahari kabisa ndani ya milima hiyo ambayo kwa sasa majengo haya yanatumika kama nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki lakini kabla ya watawa hawa kupewa majengo haya mwaka 2007, majengo haya yalikuwa ni gereza ambalo lilijengwa mwaka 1991 kumuhifadhi mfungwa maalumu raia wa Colombia.Gereza hili lilikuwa ni tofauti kabisa na magereza yote ambayo umewahi kuyasikia kwani gereza hili licha ya kuwa mali ya serikali lakini michoro yake ilichorwa na kubuniwa na mfungwa mwenyewe. Si hivyo tu, bali hata maaskari magereza ambao walikuwa wanalinda gereza hili walichaguliwa na mfungwa mwenyewe na hata polisi wa nchi ya Colombia walikuwa hawaruhusiwi kusogolea gereza hilo hata umbali wa maili 12. Kama hiyo haitoshi gereza hili lilikuwa na uwanja wa mpira wa miguu, lilikuwa na bafu lenye Jaccuzi, lilikuwa na bar, lilikuwa na maporomoko ya maji (water falls) yaliyobuniwa kiustadi, na pia chumba (sel