Posts

Serikali ya China kujenga shule ya usafirishaji nchini

Image
Dar es Salaam. Serikali ya China imesema kuwa ipo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania ya kujenga shule ya usafirishaji hapa nchini. Akizungumza leo (Jumamosi) katika hafla ya kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini iliyoandaliwa na taasisi ya Confucius, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youging amesema wakimaliza mazungumzo hayo wataanza ujenzi mara moja. Amesema lengo la ujenzi wa shule hiyo ni kuwaongezea ujuzi wahitimu na wale wasiokuwa wahitimu wa vyuo vikuu. Amesema kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji wa China hapa nchini ni kiasi cha dola bilioni saba huku kampuni zaidi ya 1,000 zikifanya shughuli zake na kutoa ajira 1,200 kwa Watanzania. Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo amezipongeza kampuni za China kwa kuisaidia Serikali kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira. “Wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini wasiichukulie fursa hii kimzaha bali waifanyie kazi kuhakikisha wanakuwa na weledi ...

OKWI RASMI SIMBA, KUZIBA NAFASI YA AJIBU.

Image
Wakati mshambuliaji Ibrahim Ajib akiwa anaelekea Jangwani, klabu ya Simba inaonekana kutokuwa na shida juu ya hilo kwasababu tayari ipo njiani kumvalisha Emannuel Okwi Jezi 25 msimu ujao. Okwi ambaye ameshaitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, ametua Bongo jana usiku na leo mchana nilipata nafasi ya kuzungumza na amethibitisha kwamba yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na Simba. “Ni kweli nipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Simba, naamini tutakubaliana kila jambo na nitasaini kuichezea tena Simba.” – alisema Okwi. Source: Shaffihdauda

MSANII ESTER APANGIWA MJENGO NA MWANAUME

Image
MSANII  wa filamu za Kibongo, Ester Kiama anadaiwa kupangishiwa mjengo na mwanaume ambaye ni mume wa mtu aliyemhamisha ku­toka Kijitonyama alikokuwa anaishi na kumwamishia Mbezi Beach. Chanzo makini kilieleza kuwa kwa sasa Ester anaishi kwenye nyumba nzima yenye hadhi tofauti na alikokuwa akiishi mwanzo ambapo amelipiwa kodi ya mwaka mzima na mwanaume huyo. Risasi Jumamosi  lilimtafuta Ester ili kujibu tuhuma hizo na alipopatikana alikiri kuhamia Mbezi Beach kwenye nyumba ny­ingine nzima lakini ali­pinga suala la kupang­ishiwa na mwanaume. “Ninaishi Mbezi Beach kwa sasa amba­ko nimehamia hivi kari­buni, habari za kwamba nimelipiwa kodi na mwanaume ni uongo, nimejilipia mwenyewe,” alisema Ester.

Serikali kujenga Ikulu ndogo makao makuu ya mkoa Songwe.

Image
Serikali imetoa shilingi billion 4.7 kwa wakala wa majengo nchini tba ili kuanza rasmi ujenzi wa ikulu ndogo na ofisi za makao makuu ya mkoa wa songwe mradi unaoanza mara moja baada ya wananchi kujitolea eneo lenye ukubwa wa hekari 40 zilizopo katika mlima nselewa kata ya mlowo wilayani mbozi. Mkoa wa songwe una zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu kuanzishwa kwake lakini kwa kipindi chote hicho viongozi wa ngazi ya mkoa akiwemo mkuu wa mkoa wamekuwa wakifanya kazi kwa kujibana kutokana na kutokuwa na ofisi hali ambayo bi chiku galawa mkuu wa mkoa songwe amesema ilikuwa haitoi nafasi nzuri katika utendaji kazi ulio bora. Aidha bi galawa amesema ujenzi huo utatosheleza kupatikana kwa ofisi za idara mbalimbali ngazi ya mkoa, nyumba ya mkuu wa mkoa na katibu tawala wake pamoja na ikulu ndogo na kwamba eneo hilo halina fidia kwa wananchi. Mtendaji mkuu wa wakala wa majengo tba elius  mwakalinga amesema bajeti ya mradi ni sh. Billion 4.7, ambapo awamu ya kwanza itatum...

Rais Baldwin Lonsdale afariki ghafla kufuatia mshutuko wa moyo

Image
Rais wa Vanuatu Baldwin Lonsdale amefariki kutokana na mshutuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 67. Bwana Lonsdale, ambaye ni kasisi wa kianglikana, amekuwa kiongozi wa kisiwa hicho cha Pacific tangu Septemba mwaka 2014. Gazeti la Daily Post nchini Vanuatu, lilisema kuwa alifariki ghafla kwenye mji mkuu Port Vila, muda mfupi baada ya usiku wa maane siku ya Jumamosi. Akiwa rais Bwana Lonsdale aliongoza ujenzi mpya wa maeneo ya kisiwa hicho kufuatia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Pam, kilichosababisha watu 75,000 kukosa makao mwezi Machi mwaka 2015. Mwezi Oktoba mwaka huo huo aliapa kupambana na ufisadi nchini Vanuatu, baada ya sakata iliyomhusisha makamu wake. Makamu wake alijiondolea mashtaka pamoja na wabunge wengine 13 wakati Bwana Lonsdale alikuwa nje ya nchi, hatua ambayo aliifuta wakati alirejea nchini.

Ishu ya Mchele wa Plastiki Bongo, Kiwanda Kinachodaiwa Kutengeneza Chavamiwa

Image
D AR ES SALAAM: Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa na uvumi una­osambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, juu ya kuwepo kwa mchele wa plastiki, unaodaiwa kuingizwa nchini na wafanyabiashara wasio waaminifu, unaouzwa katika vibanda vya akina mama n’tilie.   Kinu chenye malighafi ya kutengeneza plastiki hizo. Baada ya uvumi huo kuleta hofu kubwa kwa wananchi, hasa kufuatia video mitandaoni kuonyesha wali uli­opikwa ukiliwa na hata kiwanda kina­chodaiwa kuwepo nchini kinachoten­geneza mchele huo, Risasi Jumamosi liliamua kuufanyia kazi uvumi huo ili kujua mbivu na mbichi ya sakata hilo. Malighafi zinazotumika kutengeneza plastiki hizo hapo kiwandani. Risasi Jumamosi liliambiwa kuwa mchele huo unauzwa katika baadhi ya masoko ya jijini Dar es Salaam yakita­jwa kuwa ni pamoja na yale ya Bugu­runi, Mwananyamala, Makumbusho na Afrikasana. Kikosi kazi kilisambazwa katika masoko hayo na kufanya uchunguzi wake ikiwa ni pamoja na kuzungumza na baadhi y...

TAZAMA PICHA ZA MWANAMAMA HUYU AMBAYE ANAMIMBA YA MIEZI NANE LAKINI AKIFANYA MAZOEZI YA HATARI

Image
Julia Sharpe is a mom of twins, a mechanical engineer, and competes in men's gymnastics. Impressive photos of her doing handstands, as well as gymnastic exercises on the rings and parallel bars while 7 months pregnant with twins have emerged and they are a must-see! Dear men, would you let your wives try this at home when they are this heavy? See more photos below...

MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA YA MAUAJI DHIDI YA MTOTO WAKE YATOKANAYO NA IMANI ZA KISHIRIKINA WILAYANI MAGU.

Image
TAREHE 13.06.2017 MAJIRA YA SAA 01:00HRS USIKU KATIKA KIJIJI CHA KISABO KATA YA BUJASHI TARAFA YA SANJO WILAYA YA MAGU MKOA WA MWANZA, NUNGHU MGETA, MIAKA 35, MSUKUMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KISABO, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI DHIDI YA MTOTO WAKE AITWAYE MISUNGWI NUNGHU MIAKA 06, MTOTO WA KIUME, AMBAPO INADAIWA KUWA ALIMUUA KWA KUMZIBA MDOMO NA PUA KWA MUDA MREFU HALI ILIYOPELEKEA MTOTO KUSHINDWA KUPUMUA NA BADAE KKUPOTEZA MAISHA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI. INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA AKIISHI NA WATOTO WAKE MWENYEWE HAPO NYUMBANI KWAKE, KWANI TAYARI ALIKUWA AMETENGANA NA MKEWE KWA MUDA MREFU. INADAIWA KUWA BAADA YA MTUHUMIWA KUTELEKEZA MAUAJI HAYO ALIMCHUKUA MAREHEMU KISHA KWENDA KUMTUPA KWENYE DIMBWI LA MAJI LILILOPO MBALI NA NYUMBA YAKE ILI IONEKANE AMEKUFA MAJI. ASUBUHI WAKATI WANANCHI WANAPITA MAENEO HAYO NA KUONA MWILI WA MTOTO ALIYEPOTEZA MAISHA UKIELEA KWENYE MAJI WALIPATA MASHAKA KISHA WALITOA TAARIFA KWENYE KI...

LADY JAY DEE AACHIPA PICHA ZA MJENGO WAKE MPYA

Image
Mambo yanazidi kumnyookea mkongwe wa muziki wa Bongo Flava, Lady Jaydee. Msani huyo ameonyesha picha za mjengo wake mpya wa kisasa alioujenga ambao upo maeneo ya Kimara Temboni jijini Dar es Salaam. Kupitia mtandao wa Instagram, mrembo huyo ameweka baadhi ya picha za jumba hilo na kuandika, “Jide Ville.” Mashabiki wameanza kujiuliza, je huo ndio mjengo ambao yatakuwa makazi mapya ya Jide na mpenzi wake Spicy kutoka Nigeria?

Kesi ya waziri Mstaafu Adam Malima, mapya yaibuka

Image
Upelelezi dhidi ya kesi ya kumshambulia askari polisi inayomkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima umekamilika. Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali Esta Martin amemueleza Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwa kutajwa. "Mheshimiwa, kesi hii Leo(jana) imekuja kwa kutajwa lakini upelelezi umekamilika, tu naomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH), alidai Martin. Hakimu Mwambapa aliiahirisha kesi hiyo kwa niaba ya Hakimu Mkazi Respecious Mwijage ambaye ndio amepangwa kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa anaudhuru. "Hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hii anaudhuru, naiahirisha hadi Julai 10 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa PH mbele ya Hakimu husika", alisema Hakimu Mwambapa Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi. Katika hati ya mashtaka ilidaiwa ...

Musukuma aitaka Serikali iwatie Mbaroni ,Ngeleja Chenge na Kafumu

Image
JOSEPH Musukuma  Mbunge  wa Geita Vijijini (CCM),, ameiomba serikali iwakamate Wabunge wote wa CCM  waliotajwa kwenye kashfa ya kusafirisha mchanga wa dhahabu, maarufu kama makinikia, nje ya nchi. Amesema wabunge hao William Ngeleja (Sengerema), Andrew Chenge (Bariadi Mashariki) na Dk. Dalali Kafumu (Igunga), wanapaswa kukamatwa kwa kuwa hawana kinga inayozuia serikali kuwatia nguvuni. Musukuma aliyasema hayo jana wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya 2017/2018, ambapo alisema kwa muda mrefu serikali imekuwa ikipata wakati mgumu kwenye kashfa mbalimbali zilizotokana na wabunge hao ambao wako kwenye chama tawala. “Mheshimiwa Mwenyekiti, hao watu wanaotajwa tunao humu humu na hawana kinga. Kwa nini sasa wasikamatwe?" Alihoji Musukuma. "Kuna mwingine yuko humu baada ya kutajwa kaandika kwenye (mtandao wa kijamii wa) twitter kuwa hawezi kuhojiwa hadi atakapofikishwa mahakamani. "Sasa mtu ametuhumiwa halafu anatamba kwenye mitandao ya kijamii k...

Maneno ya Tundu Lissu juu ya ripoti ya pili ya kamati maalum ya uchunguzi wa madini

Image
For the Record: What Goes Around Comes Around!!! Leo wapinzani wa Serikali ya Magufuli tumesemwa sana na kutishiwa kushughulikiwa bungeni na nje ya Bunge. Kwa sababu hiyo, naomba niweke rekodi ya masuala haya sawa sawa. Mwezi Machi '97 Bunge lilipitisha Sheria 2 kwa siku moja kwa kutumia Hati ya Dharura. 1) Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali mbali za Fedha ya '97 ilifuta au kupunguza kodi nyingi kwa ajili ya makampuni ya kigeni ya madini. 2) Sheria ya Uwekezaji Tanzania '97 iliwapa wawekezaji wa kigeni ulinzi mkubwa na manufaa mengi kama vile kuondosha nje fedha na faida yote wanayopata kwa uwekezaji wao nchini. Mwaka '98 Bunge lilipitisha Sheria ya Madini '98 ambayo ilitamka kwamba mwenye milki ya madini na fedha yote itokanayo na mauzo ya madini ni mwenye leseni ya kuchimba madini hayo. Sheria hizo tatu nimeziita 'Utatu Usio Mtakatifu' (Unholy Trinity) katika maandiko yangu mbali mbali, na nimezichambua sana tangu mwaka ...

MO AKUBALI KUISAIDIA SIMBA MILLIONI 200

Image
Wachezaji muhimu wanataka kusepa Simba baada ya mikataba yao Kuisha Simba walimshirikisha tajiri Mohamed Dewji Kwa Ajili ya kuwasaidia kuwabakiza wachezaji hao mhimu. Kutokana na ripoti ya kocha wa Simba ameshauri waongezwe wachezaji sita wa kazi golikipa mmoja, beki watatu, Winga mmoja, na Mshambuliaji mmoja, Katika ripoti hiyo inatabainisha kuwa wachezaji ambao hawajaisaidia timu hata kwa asilimia 20 waachwe hata kwa kupelekwa Kwa mkopo. Pia ripoti ikasisitizia wachezaji mhimu wasiondoke kwenye timu kama mikataba imeisha waongezewe. Baada ya ripoti hiyo kukabidhiwa kamati ya utendaji ya kupelekwa Kwa kamati ya usajili chini ya Zacharia Hanspope ikajadiliwa na ikaonekana Mapendekezo ya Omog yatafuatwa Kwa asilimia zote tatizo likaja Kwa wachezaji mhimu ambao wanamaliza mikataba ikawa changamoto kubwa. Ndio kamati ikapeleka barua ya ombi Kwa tajiri kijana MO aweze kuwasaidia. Baada ya Mo kupokea barua hiyo aliwakubalia Simba Kwa Sharti moja tu fedha ...

Ngereja, Chenge, Kafumu wavunja ukimya

Image
VIGOGO waliotajwa katika ripoti ya pili ya kuchunguza makontena yenye mchanga wa madini (makinikia)  kuisababishia Serikali hasara ya matrilioni ya fedha kupitia sekta ya madini, walipokuwa wakihudumu katika nyadhifa zao serikalini wamevunja ukimya. Vigogo hao wamezungumzia ripoti hiyo ya pili iliyowasilishwa kwa Rais Dk. John Magufuli Ikulu Dar es Salaam jana, ambapo kamati husika ilichunguza hasara ambayo nchi imepata tangu 1998 usafirishaji wa mchanga wa dhahabu nje ya nchi ulipoanza. Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM), alipoulizwa maoni yake juu ya kutajwa na kamati hiyo, alisema hataki kuzungumza chochote juu ya ripoti hiyo, huku Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), akisema sheria ya madini ya 2010 ingefuatwa, nchi isingekuwa hapa ilipo. Kwa upande wake Kamishna wa Madini wa zamani, Dk. Dalaly Kafumu, alisema kwa sasa  hawezi kuzungumza jambo lolote kwa kuwa ni yeye ni mmoja wa watuhumiwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo. Chenge Baada...

DIAMOND PLATINUMS AFICHUA SIRI NZITO KUHUSU WEMA SEPETU KWENYE CHIBU PERFUME

Image
Msanii wa muziki, Diamond platnumz amefunguka kuuzungumzia mchango wa malkia wa filamu, Wema Sepetu kwenye perfume yake ya ‘Chibu Perfume’. Diamond amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM kuwa, yeye na Wema wanakutana na kuongea sana na wakati mwingine hushauriwa mambo mengi ya kibiashara na mwanadada huyo ambae alikuwa mpenzi wake .“Mimi na Wema labda watu hawajui sisi tunaongea sana wakati mwingine tunakutana tu sana lakini sio kwenye media. Tushakuwa kila mtu ana mahusiano yake tofauti yeye ana familia yake hata ukiangalia katika Perfume yangu lile neno THE SCENT YOU DESERVE alilitoa Wema” alisema Diamond. Muimbaji huyo kwasasa yupo kwenye mahusiano ya Zari na tayari wamefanikiwa kupata watoto wawili.