Sakata la Lugumi bado halijachacha
Dar es Salaam. Sakata la mkataba baina ya Kampuni ya Lugumi Enterprises na Jeshi la Polisi, halijafa; ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeliibua ikionyesha madoa lukuki. Sakata hilo lilikuwa kama limezikwa baada ya kamati iliyoundwa na Bunge kulichunguza na baadaye kukabidhi ripoti ofisi ya Spika ambayo ilisema ingeishauri Serikali cha kufanya. Juni 30 mwaka jana, Naibu Spika Tulia Ackson alilieleza Bunge kuwa ametumia kanuni ya 117(17) kuikabidhi Serikali matokeo ya uhakiki uliofanywa na kamati ndogo iliyoundwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). Alisema matokeo ya ripoti hiyo yana maoni, ushauri, mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zilizoainishwa na taarifa ya kamati ya PAC na hivyo kuzuia wabunge kujadili suala hilo. Lakini, ripoti ya CAG iliyotolewa wiki iliyopita imeibua upya sakata hilo, ambalo linahusu utekelezwaji mbovu wa mkataba wa uwekaji mashine za kielektroniki za kuchukua alama za