Kikosi hatari cha US NAVY 'SEAL' chatua rasmi Korea Kasikazini
NI wazi kuwa jaribio lilifanywa na Korea Kaskazini la Makombora yake ya Nukria limeshtua Marekani ambapo sasa ni rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho ndicho "The Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL inasemekana tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea jimbo la Florida nchini Marekani. Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi yake ni kufanya operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy Seal ni mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi yote ya kimarekani. Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya juu wa kupambana popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali yoyote ile iwe barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu chake ni Sea, Air and Land. Ni Mara chache s