Posts

RAPA NAYA WA MITEGO NA ZITTO KABWE WAANDIKA UJUMBEE HUU BAADA YA ROMA KUKAMATWA

Image
Baada ya Mbunge wa Mikumi na staa Bongo Fleva  Joseph Haule  ‘Prof Jay’ kutoa taarifa kupitia account yake ya Instagram kuhusu kukamatwa kwa staa mwingine wa Hip Hop  Roma Mkatoliki  katika studio za  Tongwe Records  na watu wasiojulikana, taarifa hiyo imeamsha hisia za watu mbalimbali wakiwepo mastaa wa Bongo Fleva na wanasiasa. Leo April 6 2017 kupitia account zao za Instgram na Twitter Rapa  Nay wa Mitego  na Mbunge wa Kigoma Mjini  Zitto Kabwe  wameyaandika haya.. >>>” Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?!  Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo.”  – Nay wa Mitego. >>>”Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote.”  – Zitto Kabwe.

Nape kuwaeleza ukweli wapiga kura wake jumamosi hii

Image
Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ametoa shukrani kwa wote waliomuunga mkono katika kusimamia haki huku akisema kuwa ataenda kuwaeleza wananchi wake ukweli wote. Shukrani kwa wote mlioniunga mkono katika kusimamia haki. Narudi Mtama kuwaeleza wapiga kura wangu UKWELI WOTE. Ni Jmosi hii tar 8/4/17,” ameandika Nape kupitia Twitter. Marchi 23, Rais Magufuli alimuondoa Nape kama Waziri wa Habari,Sanaa na Michezo na nafasi hiyo kuchukuliwa na Dkt Harrison Mwakyembe aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria. 

Breaking News: Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande Afariki Dunia

Image
Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande afariki Dunia. Sir Andy amekuwa mwanachama wa Freemasons kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge. Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania). SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS ​ Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi. Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani. Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012. Siyo hiv...

MARAIS WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI WAKIWA MADARAKANI

Image
Tunawaletea marais waliouawa kwa kupigwa risasi wakiwa madarakani. ABRAHAM Lincoln; alikuwa Rais wa 16 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1865 jijini Washington kwa kupigwa risasi kichwani kwa nyuma na John Wilkes. Alikuwa amekaa na mkewe. Bastola iliyotumika inaitwa Deringer.  INDIRA Priyadarshini Gandhi; Alikuwa Rais wa India. Aliuawa mwaka1984 kwa kupigwa risasi na walinzi wake, Satwant Singh na Beant Singh jijini New Delh, India.  JOHN Francis Kennedy ‘JFK’; ni Rais wa 35 wa Marekani. Aliuawa mwaka 1963 mjini Dallas kwa kupigwa risasi na Lee Harvey akiwa kwenye gari la wazi barabarani. LAURENT Desire Kabila; alimng’oa madarakani Rais Mabotu Seseko wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, lakini mwaka 2001 akauawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa ni walinzi wake.  THOMAS Isdor Noel Sankara; alikuwa Rais wa Burkina Faso Alitawala nchi kwa miaka 4 hadi 1984 alipouawa kwa kupigwa risasi inasemekana alihusika kufanya mauaji hayo ni rafik...
Image
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Job Ndugai  ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA)  Halima Mdee  kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017. Aidha Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi wa EALA. Pia Kamati ya Maadili leo imemuita DC Arumeru, Alexander Manyeti ambapo anatakiwa kutokeza mbele ya kamati hiyo kwa ajili ya kuhojiwa leo.

mwakyembe asema kuwa tukio la kuvamiwa clouds hawezi kulifumbia macho

Image
Dk. Mwakyembe aliyasema hayo wakati wa mahojiano na Nipashe kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana, muda mfupi baada ya Spika wa Bunge kusitisha shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria hadi leo saa 3:00 asubuhi. Nipashe ilitaka kujua kinachoendelea kuhusu uchunguzi dhidi ya Makonda ambaye kamati ya watu watano iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ilitoa ripoti ikidai Mkuu wa Mkoa huyo alivamia kituo cha TV cha Clouds akiwa na askari wenye bunduki na kutoa vitisho kwa wafanyakazi wa kituo hicho. Kamati hiyo ilidai kubaini Makonda alifanya hivyo ili kulazimisha video ya mwanamke anayedai kuzaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, irushwe hewani. Katika majibu yake, Dk. Mwakyembe alisema suala hilo ni “zito” na haliwezi kuachwa lipite bila kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua stahiki. Huku akiendelea kuikosoa ripoti ya kamati ya Nape ambayo amekuwa akisisitiza haijakidhi matakwa ya kikatib...

Wabunge wapania kumbana Kassim Majaliwa

Image
WABUNGE wa upinzani wamebainisha mambo manane ambayo wamepanga kumbana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, atakapowasilisha makadirio ya bajeti ya ofisi yake kwa mwaka ujao wa fedha. Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Bunge iliyotolewa Jumatatu na Ofisi ya Katibu wa Bunge, kikao cha leo ambacho ni cha tatu tangu kuanza kwa mkutano wa saba wa Bunge la 11, Waziri Mkuu atawasilisha makadirio ya bajeti yake. Wakizungumza na Nipashe nje ya Ukumbi wa Bunge jana, wabunge wa upinzani walibainisha mambo manane ambayo leo wangependa wapate ufafanuzi kutoka kwa Waziri Mkuu wakati wa mjadala wa bajeti yake. Baadhi ya mambo hayo ni uchunguzi wa miili ya watu iliyoopolewa kwenye Mto Ruvu ikiwa imefungwa ndani ya sandarusi mwishoni mwa mwaka jana, utekelezaji wa kutoa Sh. milioni 50 kila kijiji, kusuasua kwa utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka huu wa fedha, shughuli za serikali kuhamishiwa Dodoma na ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora. KUFYEKWA BAJETI YA B...

VIDEO: Halima Mdee alivyotumia neno "fala" "mpumbavu" Bungeni

Image
 T azama Video:

Chadema, CUF vyatinga Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi EALA

Image
Twaha Taslim aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki pia Mwanasheria wa CUF  VUGUVUGU la Uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki wazidi kulitikisa bunge. tayati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Chama Cha Wananchi CUF vimepanga kutinga mahakamani kupinga matokeo hayo. Jana Mweyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe alitoa kauli ya kupinga matokea hayo mahakamani kutokana na kudai kuwa uchaguzi huo ulikwenda kinyume na taratibu za uchaguzi. Leo akizungumza na Muungwana Blog kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Ahmed Katani, amesema kuwa uchaguzi huo umeendeshwa kinyume cha taratibu na kanuni za uchaguzi huo. Amesema kuwa jana majira ya saa 8 na dakika 37 kabla ya uchaguzi huo alipokea  barua kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi Dk, Thomas Kashililah. Kwa mujibu wa barua hiyo ya Msimamiza wa uchaguzi ambayo alikiri kuwa kwa wagombea wa CUF kuna matatizo na kwamba hatuweza kushiriki kuchaguzi. Katani amesema...

Mbowe amtuhumu Rais Magufuli, kwa jambo hili.

Image
MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe amtuhumu Rais John Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika kwa alichodai kuwa ni kukeukwa kwa taratibu za uchaguzi. Mbowe ameongea hayo jana usiku mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa bunge  ambapo amedai kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Rais Magufuli kuhusika kwenye mchakato wa kuyakataa majin ya wagombea wa Chadema. Mbowe amesema  kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa wa kasoro. Wagombea waliopendekezwa na Chadema  Wenje Na Masha kupigiwa kura za hapana katika  kuwania kuiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki Majina ya wagombea na matokeo KUNDI A: WANAWAKE 1. Ndg. Happiness Elias LUGIKO - KE - CCM - KURA 196 2. Ndg. Fancy Haji NKUHI - KE - CCM - KURA 197 3. Ndg. Happiness Ngoti MGALULA - KE - CCM - KURA 125 ...

Jinsi Facebook ilivyohusika mkasa wa binti aliyejitosa baharini

Image
KISA cha binti mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa kutokana na miaka yake) kujitupa baharini akiwa katika boti ya Kilimanjaro V akitoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar juzi, kinaanzia kwenye mawasiliano yake na mvulana mmoja, kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, imefahamika. Msichana huyo alikuwa akiwasiliana na mvulana huyo ambaye walifahamiana kupitia Facebook, kwa kutumia simu ya mkononi. Nipashe ilifika Kikwajuni, nyumbani kwa msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu (shule inahifadhiwa) na kuikuta familia yake ikiwa na majonzi, huku wakiwa hawaamini kilichotokea na binti huyo akiwa bado hai. Akizungumza kwa huzuni, mama mdogo wa msichana huyo, Asha Saleh Mandhi, alisema palitokea mzozo baina yake na binti huyo baada ya kumkuta na simu ya mkononi wakati wazazi wake hawajamnunulia. Alisema Jumatano iliyopita majira ya jioni akiwa nyumbani hapo na baada ya kupata taarifa kuwa mtoto wake wa kumlea anamiliki simu, alimwita na...

Washindi wa Bunge la Afrika Mashariki

Image
Wabunge watakaoiwakilisha Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki wamepatikana.

Kauli ya ACT Wazalendo kuhusu Rais Magufuli kumteua Mwanachama wao , Prof. Kitila Mkumbo Kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Image
Leo asubuhi Rais John Pombe Magufuli amemteua Mshauri wa Chama chetu Prof. Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Chama cha ACT Wazalendo kimepokea kwa mikono miwili taarifa juu ya uteuzi wa mshauri wa chama chetu Kwa sababu imeonyesha kuwa Rais ameona kuwa hata Watanzania walio kwenye Vyama vya Upinzani wana uwezo, weledi na uzalendo wa kutumikia nchi yetu. Kwa nafasi hii ya Ukatibu Mkuu wa Wizara, ndugu Kitila hawezi kuendelea kuwa Mshauri wa Chama nafasi ambayo inamfanya kuhudhuria vikao vyote vya Chama ikiwemo Kamati Kuu. Ndugu Mkumbo ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya mshauri wa Chama na kubaki kuwa mwanachama wa kawaida tu. Nimeipokea barua yake na kumkubalia Kwa maslahi mapana ya nchi yetu. ACT Wazalendo tunamshukuru ndugu Kitila Mkumbo kwa mchango wake katika uongozi wa Chama chetu kwa wakati wote ambao alikitumikia Chama chetu kama mshauri wa chama. Msimamo wa chama chetu ni utumishi wa kizalendo kwa Ta...

KITILA AMEFUNGUKA HAYA BAADA YA KUTEULIWA NA JPM

Image
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Kitila Mkumbo amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo akichukua nafasi ya Mhandisi Mbogo Futakamba ambaye amestaafu. Prof. Mkumbo ambaye pia ni kada na mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema Rais amempa heshima kubwa kwa nafasi hiyo, na yeye kama mtumishi wa umma hawezi kuikataa kwa kuwa ni kazi aliyotumwa na mkuu wa nchi. “Ukishapewa kazi na mkuu wa nchi, unaipokea na unaifanya kwa bidii kama yalivyo matarajio, kwahiyo nimepokea uteuzi, nimekubali, mkuu wa nchi akikupa kazi utaikataa vipi, mkuu wa nchi akikupa kazi unaifanya, kumbuka mimi ni mtumishi wa umma” Amesema Prof Kitila

Eritrea yapinga vikwazo vya Marekani

Image
Eritrea imepinga vikwazo ilivyowekewa na Marekani kwa kufanya biashara ya vifaa vya kijeshi na Korea kaskazini. Mpango huo ulibainika katika ripoti ya kamati ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ya 2016 iliotolewa mnamo mwezi Februari, ambapo masanduku 45 ya vifaa vya kijeshi vya mawasiliano vilipatikana vikielekea Eritrea kutoka North Korea. Eritrea imepinga matokeo ya ripoti hiyo Mamlaka za Asmara zimeonekana kujibu hatua za Marekani na kuzilaani vikali. Taarifa kutoka wizara ya habari zimesema kwamba hatua ya Marekani siyo ya haki na kwamba haifai kabisa. Asmara imeongeza kwamba sera ya Marekani kwa nchi hiyo ni ya kupotosha na kwamba hatua hii inaambatana na vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyotarajiwa kujadiliwa upya mwezi huu. Marekani huwekea vikwazo kwa taifa lolote ambalo huweka mikataba ya kijeshi na Iran, Korea Kaskazini na Syria. Vikwazo vya sasa vimelenga jeshi la wanamaji la Eriterea pamoja na jeshi la Sudan. Hii inamaana kwamba serikali ya M...

Jacqueline Wolper: Harmonize hawezi nipiga chini

Image
Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amefunguka kwa kudai kuwa mpenzi wake wa sasa Harmonaze hana uwezo wa kumuacha kimapenzi pamoja na tetesi ambazo zimekuwa zikisikika kwamba mwanamuziki huyo kuwa ana warembo wengine anaotoka nao kimapenzi. Wawili hao kwa sasa wako karibu zaidi baada ya wiki chache zilizopita kudaiwa wameachana. Akiongea na mtandao wa Central Filamu wiki hii, Wolper amedai yeye na Harmonize wako vizuri na hawadhani kama wenaweza kutengena hivi karibuni. “Wengi wanaongea sana kuhusu mpenzi wangu kama anatoka na wanawake wengi pengine inaweza kuwa ndio sababu ya kuniacha mimi hicho hakiwezekana wanaongea kama kuna wasichana wanajipendekeza watachezewa tu,” alisema Wolper. Muigizaji huyo amedai Harmonaze hana uwezo wa kumwacha kwani yeye ni muhimu kwake.

Yaliyojiri Mahakamani kwenye kesi ya Mume wa Shamsa Ford

Image
Leo April 4, 2017 ambapo mume wa mwigizaji wa filamu Shamsa Ford aiitwae Chid Mapenzi alifikishwa Mahakama ya Kinondoni kufuatia kuitwa Polisi kwa sakata la dawa za kulevya. Kwa mujibu wa wakili wake aitwae Reuben Simwanza  ameiambia millardayo.com kuwa kesi imeahirishwa mpaka tarehe 13  mwezi April kwa kosa la matumizi ya dawa hizo. ‘Kwa kifupi ni kweli kesi imekuja leo Mahakama ya Kinondoni amesomewa shtaka kwa mara ya kwanza kuhusu sheria ya madawa ya kulevya na usafirishaji wa madawa haramu, kimsingi madawa  yalitajwa kwa lugha inayoeleka ni marujuana huku mshtaki amekana mashtakiwa hayo hiyo yuko nje kwa dhamana na kesi itatajwa tena tarehe 13/4/2017 ndio atarudi Mahakamani’- Wakili

MAMA SALMA KIKWETE AAPISHWA KUWA MBUNGE

Image
Spika wa bunge, Job Ndugai akimwapisha Mama Salma Kikwete kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017. Mama Salma Kikwete akiapa kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mama Salma Kikwete baada ya kuapishwa kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017. Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge mjini Dodoma Aprili 4, 2017. Mheshimiwa Kikwete alikwenda bungeni kushuhudia kuapishwa kwa mkewe mama Salma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ANGALIA NAFASI 92 ZA AJIRA TANZANIA NATIONAL PARKS (TANAPA)

Image
Tanzania National parks (TANAPA) is a Parastatal Organization whose mandate is to manage and regulate the use of areas designated as National Parks. The organization currently manages sixteen National Parks which form part of larger protected ecosystems set aside to preserve Tanzania’s rich natural heritage. In her endeavor to promote professionalism, the organization seeks to recruit high caliber, results oriented and self-driven professionals with integrity to fill Ninety-Two (92) posts of *Park Rangers* to work in various National Parks. Park Rangers Grade IV (92 POSTS) Reporting Relationship:Report to Park Wardens / Heads of Protection Department in the Respective Parks Duty Station: National Parks /(i) Qualifications: Form IV Certificate with Basic Certificate in Wildlife Conservation from Pasiansi Wildlife Conservation Training Institute. Candidates with Certificate in basic military training from the National Service will be ...

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA BAADA YA VIKAO VYAKE KUANZA LEO

Image
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Viwanja vya Bunge kwa ajili ya kushuhudia kiapo cha Mke wake Mama Salma Kiwete aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mbunge. Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akiwasili katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya kula kiapo na kuanza majukumu yake.  Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akisindikizwa na wabunge wanawake kwenda kula kiapo cha kutumikia kazi yake leo Bungeni Mjini Dodoma. Mhe. Salma Kikwete akila kiapo cha kuwa mbunge mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai leo bungeni Mjini Dodoma.  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodom...