MBUNGE HUSSEIN BASHE AMWANDIKIA UJUMBEE HUU NAPE NNAUYE
Leo March 23, 2017 kumefanyika mabadiliko katika Baraza la Mawaziri ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison George Mwakyembe kuongoza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo ilikuwa chini ya Nape Nnauye . Baada ya mabadiliko hayo watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa wamekuwa wakilizungumzia hilo katika page zao za mitandao ya kijamii miongoni mwao ni Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe ambaye aliamua kuandika ujumbe kupitia account yake ya Twitter huku akimtaka Nape Nnauye kutovunjika moyo. Bashe ameandika>>> “Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It’s just beginning of a New journey.” Follow Hussein M Bashe @HusseinBashe Karibu back bench tutumikie Taifa letu, Majimbo yetu na Chama chetu usivunjike moyo. It's just beginning of a New journey....