Posts

BAADHI YA VIONGOZI WAKILA KIAPO CHA UADILIFU KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

Image
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa akiweka saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuduia kulia ni Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela akimkabidhi Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto). Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa(kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sek

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUANZISHA DESTURI YA KUNUNUA KAZI ZA WASANII

Image
Serikali imewataka wananchi kuanzisha desturi ya kununua kazi za wasanii, kwakuwa ndiyo njia pekee inayoweza kuwanufaisha kwa kazi wanazozifanya.Wito huo umetolewa wiki hii na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa tovuti a Afro Premiere, iliyoanzishwa kwa lengo la kuuza video za muziki za wasanii.Alisema mpango huo unaweza kuwa ni moja ya mikakati muhimu ya kupambana na wezi wa kazi za wasanii, kwakuwa video za muziki zitakuwa zikipatikana kwenye mtandao huo peke yake kwa kipindi maalum na hivyo kuingiza pesa zinazoenda kwa msanii, serikali na watayarishaji moja kwa moja. Pia alidai kuwa kwakuwa Afro Premiere itakuwa ikiweka nyimbo za Kiswahili zaidi, itasaidia kukikuza zaidi Kiswahili, ambacho ni cha 10 kati ya lugha elfu sita duniani na kuahidi kupitia wizara ya mambo ya nje, wizara yake itawaunganisha na Watanzania waliopo nje ya nchi. Prof Ole Gabriel amewataka wasanii w

MAFUNZO YA UKAKAMAVU KIDATO CHA KWANZA JITEGEMEE JKT SEKONDARY YAFUNGWA RASMI JIJINI DAR

Image
Mgeni rasmi wa kufunga mafunzo ya ukakamavu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Jitegemee Sekondari Mgulani JKT, Meja Haule (katikati), akiwa na viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Ofisa Tawala wa Kombania wa shule hiyo, Kepteni Zaujia Shemahonga, Msanifu wa Shule, Meja Rehema Wanjara, , Makamu Mkuu wa Shule Utawala, Kepteni Benitho Lubila na Makamu Mkuu wa Shule Taaluma, Ema Mosha. Paredi la ukakamavu na uzalendo likifanyika. Gwaride likitoa heshima mbele ya mgeni rasmi. Ndugu, wazazi na jamaa wa wanafunzi hao wakifuatilia kwa karibu shughuli hiyo. wanafunzi wa shule hiyo wakifuatilia gwaride hilo. Gwaride likiendelea. wazazi wakiwa kwenye hafla hiyo. Wimbo maalumu ukiimbwa. Kiongozi wa gwaride hilo, Pelegia Nyunga akikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi. Francis Christopher akipewa zawadi. Mwanahawa Shabani akikabidhiwa zawadi. Salehe Hem

Mwanafunzi akipata mimba mzazi jela miaka 30

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema serikali itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa wazazi wote wawili wa mtoto wa kike atakayekatishwa masomo na kulazimishwa kuolewa ama akipata ujauzito. Aidha amesema Serikali itamfunga jela miaka 30 kijana anayetaka kumuoa msichana anayesoma pamoja na wazazi wake. Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumlinda mtoto wa kike katika kuhakikisha kuwa anapata haki yake ya msingi ya kusoma kufikia elimu ya chuo kikuu kwa kujenga mabweni na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu watakaowapa mimba na kuwaozesha katika umri mdogo na kukatisha masomo yao. Majaliwa aliyasema hayo jana wilayani Hanang, mkoani Manyara katika ziara yake ya kikazi ya siku sita kwa mkoa huo. Alisisitiza kuwa kupitia sera ya kuboresha elimu nchini serikali imeondoa michango ya fedha za kulipia bili za maji, umeme, gharama za mlinzi na mitihani ili kumpunguzia gharama mzazi na mlezi na kuwaacha wazazi kushughulikia maeneo mengine muhimu

TCU WATOA ORODHA YA WANAFUNZI WASIO NA SIFA ZA KUSOMA CHUO KIKUU ANGALIA HAPA

Image
Tcu: Orodha ya Vyuo na Majina ya wanafunzi waliokosa sifa za kupewa nafasi za vyuo Tanzania 2016/2017   Tafadhali bonyeza jina la Chuo husika ili uweze kuona Orodha S/No. JINA LA CHUO 1 AJUCO 2 AMUCTA 3 ARU 4 CAWM 5 CBE_DODOMA 6 CBE_MWANZA 7 CDTI 8 CFR 9 CUHAS 10 DIT 11 DMI 12 EASTC 13 ETU 14 HKMU 15 IAA 16 IFM 17 IMTU 18 IRDP 19 ISW 20 ITA 21 JUCO 22 KCMUCo 23 KENYATTA 24 MOCU 25 MUHAS 26 MUM 27 MUST 28 MZUMBE 29 NIT 30 RUCU 31 SAUT_ARUSHA 32 SAUT_MBEYA 33 SAUT 34 SEKOMU 35 SFUCHAS 36 SJUCMC 37 SJUT 38 SMMUCO 39 St. MARKS 40 STEMUCO 41 SUA 42 SUMAIT 43 SUZA 44 TEKU-DAR 45 TUDARCO 46 TUMA-MBEYA 47 TUMA 48 U-BAGAMOYO 49 UDOM 50 UDSM 51 UoI 52 ZIFA