Posts

RAIS JOHN MAGUFULI LEO AMEMTEUA ROGERS W. SIANGA KUWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA.

Image

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA LEO

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia baadhi ya ajenda wakati  kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.  Mawaziri wakijadiliana jambo kabla kikao cha Baraza la Mawaziri hakijaanza kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage. Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba(kushoto), Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) wakizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughul...

UPDATES: IDD AZZAN AWASILI KITUO CHA POLISI CHA KATI KWA AJILI YA MAHOJIANO

Image
Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddy Azzan ameripoti katika kituo cha polisi cha kati kama aliyotakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Azzan amewasili kituoni hapo muda wa saa 09:06 kwaajili ya mahojiano na polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkuu wa mkoa. Azzan ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa na mkuu wa mkoa juzi kutakiwa kufika polisi jijini Dar es Salaam. Jana. Askofu wa kanisa la ufufuo uzima Josephat Gwajima na mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji ambao nao wapo katika orodha hiyo ya mkuu wa mkoa waliripoti.Kamanda wa Kanda Maalumu, Simon Sirro amesema ifikikapo saa 7 mchana atazungumza na waandishi wa habari.

FREEMAN MBOWE AGOMA KWENDA KUHOJIWA POLISI ASEMA MAKONDA HANA MAMLAKA HAYO

Image
Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.  Mbowe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma kufuatia kutajwa katika orodha ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo saa tano asubuhi. Mbowe amekanusha vikali tuhuma hizo za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa anachokifanya RC Makonda ni kuwaepusha watuhumiwa wa kweli wa dawa za kulevya na mikononi mwa sheria. Aidha, Mbowe amesema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi muda wowote endapo njia sahihi zitakapofuatwa.  Pia amesema atamfungulia mashtaka RC Paul Makonda kwa kumchafulia jina lake kufuatia kumtuhumu kwa biashara ya dawa za kulevya. Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani ...

Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe……Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo.

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji  kumhoji. Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Amesema operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.

STAA WEMA SEPETU KUONANA USO KWA USO NA ZARI THE BOSS LADY

Image
Akizungumza live kutoka Clouds Fm, Diamond ametamka rasmi kuwa staa Wema Sepetu ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye sherehe hiyo, kwa upande wa Zari Hassan nae amesema hana shida na ujio wa Wema Sepetu Kwenye Arobaini ya Nillan ambaye waliwahi kuingia kwenye bifu kipindi cha nyuma. Kama kweli Wema akifanikiwa kuhudhuria kwenye sherehe hiyo itakua ndo mara ya kwanza kwa mafahari hao wawili kuonana, na itakua sherehe ya aina yake kwa uwepo wa mastaa hao waliowahi kuingia kwenye vita nzito na kurushiana maneno mtandaoni

MUME AMKATA MASIKIO MKE WAKE, SABABU YATAJWA KUWA AMEMCHOKA

Image
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Zarina mkazi wa mji wa Balkh, Afghanistan amekatwa masikio na mume wake kwa madai kuwa mume wake amemchoka na hataki kuishi nae. Akielezea tukio hilo la kikatili, Zarina alisema amedumu na mwanaume huyo kwa muda wa miaka saba na tukio hilo lilitokea wakati akiwa amelala usiku lakini ghafla aliamka na kukuta akifanyiwa tukio hilo.“Sikuwa nimemfanyia jambo lolote baya, sijui kwanini mme wangu alinifanyia hivi … mahusiano yetu hayakuwa mazuri,” alisema Zarina.Mwanamke huyo mwenye miaka 21 aliongeza kuwa mume wake amekuwa akimfanyia vitendo vya kikatili kwani kuna kipindi alimzuia hata kwenda kuwatembelea wazazi wake.Aidha Zarina alizungumza kuhusu mpango wake wa baadae kama ataendelea kuishi na mwanaume huyo na kusema, “Sihitaji tena kuishi nae.” Zarina kwasasa anapatiwa matibabu katika moja ya hospitali iliyopo Balkh na Polisi mjini humo wamesema mume wake amekimbia na juhudi za kumtafuta zinafanyika ili hatua za kisher...

MZEE WA UPAKO NAE AFUNGUA HAYA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

Image
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Amefunguka na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake. Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano. “Mimi ni mhanga wa dawa za kulevya mwaka 1997 nilituhumiwa kuwa nauza madawa, lakini wale askari walikuwa wastaarabu, waliniandikia samasi nikafika kutoa maelezo yangu, lakini baadaye niliwaambia kuwa wao ni polisi wafanye uchunguzi wao, walifanya uchunguzi na kugundua mimi sihusiki, watu walifuatilia na kugundua siyo kweli, na kila mtu akajitoa kwenye, ilionekana kuwa ni wivu tu, ila mbaya zaidi ile ...

SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA ASKOFU GWAJIMA ATEMA CHECE ,ADAI DC MAKONDA ANATUMIKA

Image
Gwajima:   Nakumbuka Kuna siku Makonda alikuwa anahutubia, akamwambia Waziri mkuu eti nlipiga marufuku shisha lakini imerudi, hawa wavuta shisha waliniletea Milion 5 nikakataa akasema lakini naamini kamanda Siro hizi milioni tano tano zimepita kwao. Makonda alidiliki kumtuhumu Waziri MKuu eti Karudisha Shisha!?. DC Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar, kwanini hakuisemea kwenye Vikao, Kwanini alisubiri Media? Gwajima:   Safari hii kamfikia kiongozi wa Kiroho, huu ni unafiki sana. Huweze kumuita rafiki yako kaka yako namna hii. Gwajima:   Sasa leo nataka niwambie kwanini Makonda anafanya hivi; 1. Nataka niwambie, Rais hajamtuma Makonda atutuhumu sisi 2. System za Serikali zimeparalyse kwa sababu watendaji wa Serikali na Mawaziri wanamuona Makonda ni Mkono wa kiume wa Rais. Wanafikiri labda kwakuwa Makonda ni Msukuma basi atakuwa anatumwa na rais, Rais hawezi kufanya hivyo. Mawaziri wamekosa neno wamekaa ...

MANJI AJISALIMISHA POLISI

Image
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ,Yusufu Manji akiwasili katika kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam mara baada ya kuamua kujipeleka hapo yeye kwa ajili ya kuhojiwa baada ya kutajwa kwenye watu wanaotuhumiwa na madawa ya kulevya. Yusufu Manji akipokelewa na baadhi ya wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi kati mara baada ya kujipeleka leo badala ya kesho Manji akisalimiana na wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi Kati Mnaji akiwa akiwa ameongozana na mawakili wake na wasaidizi kuingia kituo cha kati jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji akisalimiana na Waandishi wa Habari jijini Dar ess Salaam katika kituo cha Polisi Kati

BREAKING NEWS: ANGALIA TUNDU LISSI NAWEMA SEPETU WALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI MUDA HUU WAKIWA KWENYE GARI MOJA

Image
Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu pamoja na Mwigizaji Wema Sepetu wamefikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kujibu tuhuma zinazowakabili.Tundu Lissu anatuhumiwa kwa kutoa kauli za kichochezi mara kwa mara na Wema Sepetu ni kuhusu ishu za dawa za kulevya Wema Sepetu Tundu Lissu Tundu Lissu Tundu Lissu Wema Sepetu V

Wabunge Wapinga Mbowe Kutajwa na Makonda,Zitto Kabwe Atoa Povu Hili..!!!

Image
Hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaja Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe kufika katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapo kesho kuhojiwa, imewachefua baadhi ya wabunge. Wabunge waliohojiwa mjini Dodoma jana, walisema kinachoendelea ni siasa badala ya uhalisia. Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT – Wazalendo), Zitto Kabwe alisema kinachoendelea ni siasa za kuchafuana na kwamba Makonda ajiandae kubeba msalaba wake katika jambo hilo. “Juzi hapa nililalamika bungeni kwamba leo wanakamatwa wasanii, kesho watakamatwa wabunge. Mmeona leo Makonda amemtaja Mbowe. Kinachoendelea ni siasa za kuchafuana. Kitendo cha Makonda kumtaja Mbowe maana yake ni kwamba kazi anayoifanya si yake, ni kazi ambayo ametumwa na wakubwa wake na ndiyo maana wanamuunga mkono,” alisema. Zitto aliwataka wabunge wa upinzani bila kujali tofauti zao za vyama, kuliona suala la Mbowe kuwa si shambulio kwa mbunge huyo wa Hai pekee yake, bali ni mashambulizi dhidi ya wabunge wa ...

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA GHAFLA KUTEMBELEA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE (TERMINAL III) DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na baadhi ya wahandisi na mak...

RC MAKONDA ATAJA LISTI NYINGINE YA MAJINA 65 YA WANAOHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaja majina ya watuhumiwa wengine 65 wa madawa ya kulevya, wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Elikael Mbowe, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Askofu Josephat Gwajima na Mbunge Mstaafu wa Kinondoni, Idd Azzan. Makonda amesema hii ni awamu ya pili ya oparesheni ya kusaka watuhumiwa wa mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya, ambapo amesema awamu hii itakuwa ngumu ikilinganishwa na ile ya kwanza iliyohusisha polisi na wasanii kukamatwa. Makonda amewataka watu wote 65 waliotajwa, kuhakikisha wanaripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Sentro) siku ya Ijumaa saa 5 asubuhi kwa mahojiano zaidi. Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Makonda amesema kuwa, waliokamatwa awali ndiyo waliofanikisha kupatikana kwa orodha hiyo mpya.