WIZARA YA HABARI YAZINDUA PROGRAMU YA WADAU TUZUNGUMZE
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) leo Februari 07, 2017 Jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake. Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akizungumza leo Februari 07,2017 Jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau wa sekta zinazosimamiwa na Wizara yake. Picha na Raymond Mushumbusi Na: Genofeva Matemu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imebuni na kutanganza Programu ya kushirikisha wadau inayoitwa wadau tuzungumze itakayosaidia wizara kupata vionjo, maoni, mawazo na fikra za wadau katika kuhakikisha kwamba Wizara inafanya kama wadau wake wanavyotegemea. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.