Posts

UFAULU WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2016 WAPAA

Image
  Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016. Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26. Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015. Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA (UN) PIA AHUDHURIA MKUTANO WA AU MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Antonio Manuel Olveira Guterres mara baada ya mazungumzo yao. ...

BREAKING NEWS : ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016

Image
THE NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA. English ... NECTA is responsible for the administration of all National Examinations in Tanzania. BOFYA HAPA KUONA MATOKEO YOTE HAPA

BREAKING NEWZZ:MWENYEKITI WA CCM MBEYA ANUSURIKA KUUAWA

Image
Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka 60 amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika. Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 05:45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala kitandani nyumbani kwake Ntembela ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni  kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za gololi. Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na hali yake inaendelea vizuri. Lukula amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi hilo ilikuwa ni kutaka kuumua na kwamba juhudi za kuwatafuta na kuwakamata wahusika zinaendelea

FARU FAUSTA WA NGORONGORO,ATIMIZA MIAKA 54 AISHI CHINI YA ULINZI WA KIJESHI

Image
Ndio faru mzee duniani,sasa haoni Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54.Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona. Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo.Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba. Hivi sasa gharama inayotumika kumlinda Faru Fausta ni kubwa,hivyo uongozi wa Mamlaka umeishauri wizara kuchukua hatua juu ya Faru Fausta

BREAKING NEWZZZZ…TRENI YA ABIRIA ITOKAYO KIGOMA KWENDA DAR YADONDOKA

Image
TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma  kwenda jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani leo jioni Jumapili Januari 29, 2017. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinasema takriban mabehewa 10 kati ya 20 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea na watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa. Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo unmeaning na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio. “Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwe...

WALIOKWAMA KWENYE KIFUSI KWA SIKU MBILI KATIKA MGODI WA RZ NYARUGUSU WAOKOLEWA

Image
Wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ uliopo Nyarugusu, Mkoani Geita wameokolewa wote wakiwa asubuhi ya leo. Wachimbaji hao walikumbwa na kadhia hiyo, siku mbili zilizopita baada ya udongo kufunika sehemu ya kutokea. ila kwa juhudi mbalimbali walizokuwa wakizifanya, waliweza kuwasiliana na waliokuwa nje ya mgodi na hatimae kufanikiwa kuokolewa leo asubuhi. Baadhi ya Raia wa kigeni wenye asili ya China wakimjulia hali mwenzao ambaye alikuwa ni mmoja wa walikumbwa na dhoruba hilo la kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa RZ Nyarugusu, Mkoani Geita. Sehemu ya Askari Polisi na wa Kikosi cha uokoaji wakiendelea na zoezi la uokozi kwa waathirika wa tukio hilo, asubuhi ya leo. Hivi ndivyo zoezi la uokoaji kwa ndugu zetu hao lilizovyofanikiwa kwa jitihada za vikosi vya usalama na uokoaji.

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA KIKAO CHA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA A+ A- Print Email Share this PostFacebook shareTwitter sharePin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. PICHA NA IKULU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. PICHA NA IKULU

Ten(10)Foolish Things to Say or Not to Say When Texting Boys

Image
We live at a time when most of our daily interactions happen through texts. That’s right, we rarely even call people anymore. We just text everyone. So it’s not surprising that a lot of our dating and flirting also happens through text. When you give a guy your phone number you don’t even expect him to call, you know he’ll text. It takes a bit of the pressure off, since you don’t have to speak your mind immediately, you can take your time and write out a perfect response. But texting boys can be tricky, there’s a balance you have to strike. That’s why we compiled a couple of pointers to help you figure out what you should and shouldn’t say when texting boys. 1. You never want to come off as clingy when texting a new boy . It might be a good idea to avoid texts like “I miss you”, and instead text him something like “ Wait till you see what I’m wearing” or “I can’t wait to take you home” . This way you’ll keep him interested and he’ll know you’re thinking of him. ...

Mwanamke Asimulia Alivyokuwa Akimshushia Kipigo Mumewe kwa Miaka 30 Mfululizo

Image
Mara nyingi vitendo vya ukatili na unyanyasaji kijinsia vimezoeleka kufanywa na wanaume dhidi ya wanawake na watoto. Hata hivyo, kampeni ya “Tunaweza” inayoratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Kivulini jijini Mwanza kwa lengo la kutokomeza ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, imebaini kuwa vitendo hivyo pia hufanyika dhidi ya wanaume. Mkazi wa Mtaa wa Mwananchi, Kata ya Mahina jijini Mwanza, Ernest Kibinzaroya (78) ni mfano wa ukatili unaofanywa na wanawake dhidi ya wanaume. Yeye pamoja na mkewe, Maria Kibinzaroya (57) wamejitokeza hadharani kueleza walivyopitia maisha hayo. Inaelezwa kwamba Maria alikuwa akimpa kipigo cha mara kwa mara mumewe kabla ya ‘kuokoka’ na kuwa mke mwema. ‘Wokovu’ huo ni baada ya kampeni hiyo inayofanyika katika wilaya za Ilemela, Nyamagana, Magu, Misungwi, Sengerema mkoani Mwanza kuwafikia wanadoa hao na wote hivi sasa wana mabadiliko na wanapiga vita ukatili na unyanyasaji wa kijinsia. Akizungumza mbele ya mumewe wakati wa mahoji...

BREAKING NEWS : KIONGOZI WA WALINZI WA IKULU YA GAMBIA ATOROKA

Image
Kamanda wa Polisi wa Jeshini (MP) katika ikulu ya Gambia, Luteni Nuha William Jammeh, yasemekana yupo mafichoni. Inasemekana alitoroka Gambia siku chache zilizopita. Kamanda huyu alitoa amri ya kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa jeshi la nchi hiyo walioonekana kumpinga Rais aliyemaliza muda wake, Yahya Jammeh. Kwa sasa Luteni Nuha Jammeh hajulikani alipo. Amekimbia mji mkuu wa Banjul na inaaminika kuwa amekimbilia nchini Senegal. Namba yake rasmi ya simu inayojulikana inaonesha kuwa yupo nchini Senegal ingawa simu yake imezimwa. Akimzungumzia Nuha Jammeh, mtu aliyewahi kusoma nae darasa moja alisema: ” Alikuwa mkimya sana na anayependa sana dini. Ilikuwa ni rahisi sana kuzoeana naye kipindi kile. Baada ya kukutana na Yahya Jammeh, huwezi jua, kwa maana yule dikteta alikuwa na uwezo wa kugeuza watu wazuri kabisa kuwa mashetani.”

KIPIGO CHA WANAJESHI CHA SABABISHA KIFO CHA KONDA WA DALADALA TANGA

Image
Kondakta wa daladala linalofanya safari zake kati ya Nguvumali hadi Raskozone, Salim Kassim amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa ndani ya kambi ya jeshi jijini hapa. Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, kondakta huyo alikufa wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo na chanzo cha kifo bado kinachunguzwa.Mwananchi ilielezwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku, ambapo mashuhuda walidai kuona kondakta huyo akichukuliwa na wanajeshi na kuingizwa kambini na baadaye alitolewa akiwa hajitambui Akizungumzia tukio hilo, Khalid Juma mkazi wa Nguvumali jijini hapa alisema askari hao wamekuwa na desturi ya kuwapiga wananchi bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria. “Tumekuwa tukipata vipigo kila wakati, licha ya viongozi kupata taarifa za matukio hayo wamekaa kimya na hili tukio ni la tatu kutokea hapa,” alidai Khalid. Diwani wa Kata ya Nguvumali ambaye pia ni Meya wa Jiji ...

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEKAMATA MAGARI MATANO.

Image
Kamishina wa Polisi wa kanda maalm ya Dar es Salaam CP Saimon Sirro akizugumza na waandishi wa habari juu ya Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kuhusu kukamata magari matano ambayo yanasadikiwa kuwa yaliibiwa katika vipindi tofauti katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel massaka, Globu ya jamii. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha silaha aina ya SHORTGUN PUMP ACTON iliyo kutwa nyumbani kwa mtuhumiwa huko Boko njiapanda leo jijini Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha kadi bandia za chanjo ya homa ya manjano zilizokamatwa maeneo ya Hospital ya Mnazi mmoja jiji Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha magari yaliyokuwa yameibiwa katika sehemu mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo. Pich...