Barron Trump Ndiye mwana wa pekee wa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump na mke wake wa sasa, Melania. Ingawa alijitokeza katika mikutano kadha ya kampeni, kijana huyo wa miaka 10 hakuwa akionyeshwa mara kwa mara hadharani. Anapendelea kucheza gofu na baba yake, pia ana uwezo mkubwa wa kuzungumza Kislovenia kwa ufasaha. Melania Trump Ni mwanamitindo wa zamani, mzaliwa wa Slovenia, aliolewa na Donald Trump Januari 2005. Alijitokeza na kumtetea mumewe, baada ya kanda ya video kutolewa wakati wa kampeni na kumuonesha akijitapa kuhusu kuwadhalilisha kimapenzi wanawake. Julai 2016, aligonga vichwa vya habari baada ya kutoa hotuba katika mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Republican, baada ya Trump kuidhinishwa kuwania urais, ambapo alituhumiwa kuchukua maneno mengi kutoka katika hotuba iliyotolewa na Michelle Obama mwaka 2008. Alipoulizwa na CNN Oktoba ni jambo gani angetaka kubadilisha kwa mumewe, alijibu: “Kuandika