Makonda Kujenga Vituo 20 Vya Kisasa Vya Polisi Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi Kituo cha Polisi cha Tandika, Dar. ..Maongezi yakiendelea katika Kituo cha Polisi cha Tandika. Makonda akizungumza na mmoja wa mahabusu alipotembelea vituo vya polisi. Kituo cha Polisi Kigogo, Dar. Muonekano wa Kituo cha Polisi Traffic Mwenge, Dar. Tangu kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi na taarifa za changamoto zifuatazo kuhusu hali ya huduma za kipolisi mkoani kwake;- 1. Wananchi kutokupatiwa huduma kwa saa 24 kutokana na vituo hivyo kufungwa usiku. 2. Mazingira mabovu na yasiyoridhisha ya vituo vya polisi. 3. Polisi kutofika kwenye matukio kwa wakati pindi wapigiwapo simu na wananchi. 4. Polisi kushindwa kutoa huduma kutokana na upungufu wa askari polisi. 5. Majambazi kuvamia vituo vya polisi wakiwa na lengo la kuchukua silaha. Changamoto hizi za msingi na ambazo zinahatarisha uhakika wa usalama wa raia wa Da...