DC Hapi Atembelea Wajasiriamali Wa Airtel Fursa
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akikagua bidhaa za wajasiriamali wadogo waliowezeshwa kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Kulia aliyeambatana naye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano. …Hapi akipata maelekezo ya changamoto mbalimbali zinazowakabili kutoka kwa mjasiriamali aliyewezeshwa na Airtel Fursa (aliyeko kulia). …Hapi akiendelea kukagua nembo za TBS na Bar Code katika bidhaa za wajasiriamali hao waliowezeshwa na mpango mkakati wa Airtel Fursa. …Hapi akikabidhiwa keki na Diana Moshi aliyokuwa ameiandaa (kushoto) ambaye ni mjasiriamali anayemiliki kampuni yake iitwaye Diana’s Oven aliyowezeshwa na Airtel Fursa. Mjasiriamali wa kuchora aitwaye, Theresia Deus (kushoto) akimuonyesha bidhaa zake mkuu huyo baada ya kuwezeshwa Laptop kwa ajili ya kuchorea na Airtel Fursa miezi mitano ilyopita sasa. Hapi na RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda wakiangalia mayai ya kienyeji kutoka kwa mjasiriamali wa kufuga kuku wa Wilaya ya...