Posts

Wahukumiwa Kifo kwa Kumuua Albino Bukoba

Image
Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo imewahukumu kunyongwa hadi kufa watuhumiwa waili Lameck Bazil na Pankras Minago kwa kumuua albino Magdalena Andrea. Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Firmin Matogolo baada ya kuridhika na ushahidi kuwa watu hao ndiyo waliomuua mlemavu huyo ambaye ni mkazi wa Wilaya ya Biharamulo mwaka 2008. Credit: Fahari News

Hizi Ndizo Shule Zilizofanya Udanganyifu Kwenye Mtihani wa Darasa la 7

Image
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk. Charles Msonde akitangaza matokeo ya Kumaliza Elimu ya Msingi 2016, mapema leo. … Msonde akionyesha baadhi ya nguo za wanafunzi zilizokamatwa katika kipindi cha mitihani zikiwa zimeandikwa majibu ya mitihani hiyo. …Akionyesha kaptula ya mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Tumaini iliyopo Wilaya ya Sengerema yenye majibu ya maswali ya mtihani wa Darasa la Saba iliyokamatwa. … Akionyesha karatasi ya mfano wa majibu inayoonyesha baadhi  ya wanafunzi yenye ufanano wa aina moja katika shule. Mkutano na wanahabari ukiendelea.

BREAKING NEWSS:HAYA NDIO MATOKEO YA DARASA LA SABA

Image
Kuyatazama matokeo ya darasa la saba mwaka 2016; Bofya Hapa  au Bofya Hapa

MANCHESTER UNITED WAITANDIKA MAN CITY NA KUTINGA ROBO FAINALI

Image
      Kikosi cha Manchester United kinachoongozwa na Jose Mourinho usiku huu kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester City. Mchezo huo wa Kombe la EFL uliopigwa kwenye Uwanja wa Manchester United, Old Trafford ulimalizika kwa bao pekee lililofungwa na Juan Mata dakika ya 54. VIKOSI MANCHESTER UNITED: De Gea, Valencia, Rojo, Blind, Shaw, Carrick, Herrera, Mata (Schneiderlin 73), Pogba, Rashford (Lingard 82), Ibrahimovic Benchi: Romero, Depay, Young, Fellaini, Darmian MANCHESTER CITY: Caballero, Maffeo, Otamendi, Kompany (Kolarov 46), Clichy, Garcia Serrano, Fernando, Sane (Sterling 63), Jesus Navas, Iheanacho, Nolito (Aguero 71) Benchi: Gunn, Gundogan, Fernandinho, Adarabioyo

TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA HAFLA YA UTILIAJI SAINI MIKATABA 21 KATI YA TANZANIA NA MORROCO

Image
Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco Akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mgeni wake Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco wakiwaangalia wapigaji ngoma mara baada ya kuwasili Leo Ikulu Jijiji Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mgeni wake Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco wakipiga ngoma mara baada ya kuwasili Leo Ikulu Jijiji Dar es Salaam.   Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa mikataba 21 kati ya Tanzania na Morocco. Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustino Mahiga akiizungumzia mikataba 21 itakayosainiwa kati ya Tanzania na Morocco. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akieleza namna Tanzania itakavyonufaika na mikataba 21 iliyosaniwa katika ya Nchi ya Morocco na Tanzania. Waz

PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA KUWASILI MFALME MOHAMED VI WA MOROCCO, NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU

Image
Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI (aliyetangulia mbele) akishuka katika Ndege mara alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Mfalme wa Morocco Mohammed VI akipokea shada la maua alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mfalme wa Morocco Mohammed VI wakisimama kwa nyimbo za Taifa na mizinga 21 mara baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara ya siku tatu