Posts

TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA HAFLA YA UTILIAJI SAINI MIKATABA 21 KATI YA TANZANIA NA MORROCO

Image
Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco Akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mgeni wake Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco wakiwaangalia wapigaji ngoma mara baada ya kuwasili Leo Ikulu Jijiji Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mgeni wake Mfalme Mohamedi wa Sita wa Morocco wakipiga ngoma mara baada ya kuwasili Leo Ikulu Jijiji Dar es Salaam.   Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliohudhuria hafla ya utiaji saini wa mikataba 21 kati ya Tanzania na Morocco. Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustino Mahiga akiizungumzia mikataba 21 itakayosainiwa kati ya Tanzania na Morocco. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akieleza namna Tanzania itakavyonufaika na mikataba 21 iliyosaniwa katika ya Nchi ya Morocco na Tanzania....

PICHA MBALIMBALI ZA TUKIO LA KUWASILI MFALME MOHAMED VI WA MOROCCO, NCHINI KWA ZIARA YA SIKU TATU

Image
Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI (aliyetangulia mbele) akishuka katika Ndege mara alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Mfalme wa Morocco Mohammed VI akipokea shada la maua alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mfalme wa Morocco Mohammed VI wakisimama kwa nyimbo za Taifa na mizinga 21 mara baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara ya siku tatu ...

PANYA ROAD APEWA KIPIGO KIZITO NA WANANCHI, AZINDUKA AKIWA MOCHWARI

Image
Mtoto Isack Ernest (16) anayetuhumiwa kuwa ni mhalifu, maarufu Panya Road, amezinduka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) katika Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam. Isack ni miongoni mwa vijana watano waliopigwa na wananchi wenye hasira kwa madai ya kuiba mali zao hali iliyosabisha apoteze fahamu na kudhaniwa amefariki dunia. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Gilles Muroto, alisema baada ya polisi kupigiwa simu na raia wema kuwa kuna vijana watatu wamefariki dunia, walikwenda eneo la tukio na kuwakuta wakiwa na hali mbaya. “Mmoja wao anayeitwa Kelvin Nyambocha (14) alifariki dunia baada ya kupigwa na kuchomwa moto na wananchi.   “Kabla ya kufariki, Kelvin alifuatana na wenzake kwa lengo la kwenda kuangalia tamasha la kuibua vipaji vya muziki wa singeli lililoandaliwa na Radio Clouds Fm lililofanyika Mbagala Zakhem,” alisema ...

Khadija Kopa Kuwasha Moto Krismas Morogoro

Image
Mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  akizungumza jambo na wanahari (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni mkuu wa matukio kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kurugira Maregesi,  Hamis Abdallah na Khadija Kopa. Khadija Kopa akizungumza jambo. Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat, akielezea namna atakavyopagawisha mashabiki wake. MALKIA wa muziki wa taarab ambaye ni Mkurugenzi wa Kundi la Ogopa Kopa, Khadija Kopa,  anatarajiwa kuwasha moto kwa kutoa burudani ya aina yake katika  Tamasha la Muziki wa Taarab  lililoandaliwa na mtandao wa habari wa Vijana, Tegemeo Arts Group ambalo linajulikana kwa jina la ‘Nani Zaidi’. Tamasha hilo litakaofanyika siku ya X-Mass ya Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi usiku. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah,  amesema tamsha hilo linalenga kuh...