Khadija Kopa Kuwasha Moto Krismas Morogoro
Mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah, akizungumza jambo na wanahari (hawapo pichani). Kutoka kushoto ni mkuu wa matukio kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Kurugira Maregesi, Hamis Abdallah na Khadija Kopa. Khadija Kopa akizungumza jambo. Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat, akielezea namna atakavyopagawisha mashabiki wake. MALKIA wa muziki wa taarab ambaye ni Mkurugenzi wa Kundi la Ogopa Kopa, Khadija Kopa, anatarajiwa kuwasha moto kwa kutoa burudani ya aina yake katika Tamasha la Muziki wa Taarab lililoandaliwa na mtandao wa habari wa Vijana, Tegemeo Arts Group ambalo linajulikana kwa jina la ‘Nani Zaidi’. Tamasha hilo litakaofanyika siku ya X-Mass ya Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa kumi usiku. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, mwenyekiti na mratibu wa tamasha hilo, Hamis Abdallah, amesema tamsha hilo linalenga kuh...