Posts

RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya aenda gengeni kula ugali na nyama choma.Tazama Picha

Image
Rais Uhuru Kenyatta amekichoka chakula cha ikulu ndio maana aliamua kujichanganya na Senator Mike Sonko kwenda gengeni kula ugali na nyama choma. Sonko alimpeleka rais huyo kupata chakula cha usiku kwenye soko la Kenyatta. Aliongoza na waheshimiwa wengine, Sakaja, Madam Shebesh na Kariuki walianza kwa kutembelea soko hilo kuzungumza na wafanyabiashara. Baadaye Sonko aliweka picha akiwa na waheshimiwa hao na kuandika: Together with President Uhuru Kenyatta, Hon Sakaja, Hon Madam Shebesh, Hon Kariuki we made a surprise stop at Kenyatta Market interacted with traders and later on my bestfriend and our President akasema anahisi njaa so I decided to buy lunch at one of the kiosks. Lazima tuinue biashara za watu.”

Ndege mpya ya serikali yatua Dar

Image
Ndege mpya ya serikali, Bombardier Q400 ikiwa katika Uwanja wa Julius Nyerere, Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini mchana wa leo kutoka Canada. Ndege hiyo ikimwagiwa maji mara baada ya kutua. Rubani aliyeileta ndege hiyo akiwa katika pozi baada ya kutua. Baadhi ya watu walioipokea ndege hiyo wakiwa ndani wakifurahia mandhari yake. Baadhi ya Viongozi wa Shirika la Ndege la ATCL wakikagua ndege hiyo. Marubani waliyeileta ndege hiyo na kiongozi mmoja wa ATCL wakiwa katika picha ya pamoja. Ndege ya kwanza kati ya mbili zilizoagizwa na serikali, aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini Canada tayari imewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. Ndege hizi mbili zimenunuliwaili  kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ambalo kwa sasa lina ndege mbili, ambayo moja ni ya kukodi. Ujio wa ndege hizi mbili umeelezwa kuwa umelenga kusaidia katika soko la ndani na kurahisisha usafiri wa anga kwen...

AJALI NYINGINE MBAYA YA MAASI YAGONGANA USO KWA USO

Image
  Basi la Kampuni ya MANING NICE limegongana uso kwa uso na Basi la HOPE SAFARI katika eneo la karibu na Daraja la Mang'ula Baada Dereva wa Basi la Maning Nice kushindwa kulimudu Basi hilo na kusababisha kugongana Uso kwa Uso na basi la HOPE SAFARI. MUHANGA WA AJALI HIYO AKISIMULIA.Baada ya Basi la Hope Safari kuvuka Daraja la Mang'ula ikitokea Morogoro ikipita kibao cha shule ya mlimani ikielekea ifakara ghafla mbele tukaona basi la Maning Nice inashuka ikiwa inaelekea Dar na wakati huo ikiwa imejaa upande wa pili alikotakiwa kupita huyu waliyekuwa wanapishana naye na kwa sababu Maning alikuwa na spidi kali hakuweza kusovu tatizo na ndipo Mabasi yote mawili yakagongana uso kwa uso upande wa abiria baazi wamepata majeraha isipokuwa madreva wote wawili wameumia sana.

Basi la New Force Lapata Ajali na Kuua Watu 12 Njombe

Image
Basi la kampuni ya New Force lenye namba za usajili T429 DEU baada ya kupinduka eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, Mkoani Njombe. Wananchi na polisi wakiwa eneo la ajali.   …Wakiendelea kuokoa watu waliokuwemo kwenye basi hilo.   Muonekano wa basi baada ya ajali.   Watu 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya New Force lenye namba za usajili T429 DEU kupinduka eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, mkoani Njombe. Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Njombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wa kuamkia leo wakati likitokea  Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe.   Kwa mujibu wa habari kutoka shirika la habari la taifa (Shihata) huko Njombe, kati ya watu hao 12 wanawake ni wanane akiwemo mtoto mmoja wa kike  na wanaume wanne akiwemo mtoto mmoja wa kiume.   Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo kas...

JK Avutiwa Na Wimbo Wa Matatizo Wa Harmonize

Image
Msanii wa muziki, Harmonize (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete. Wimbo ‘Matatizo’ wa msanii wa muziki Harmonize, ni moja kati ya nyimbo ambazo zinapendwa na Rais Mtaafu, Jakaya Mrisho Kikwete. Wiki moja iliyopita Mh.Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwaalika viongozi wa WCB pamoja na wasanii wake nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana. “Unajua wakati Mh Jakaya Kikwete anatoka madarakani Diamond Platnumz bado alikuwa hajasaini wasanii wengine chini la WCB Wasafi, hivyo tulikwenda kuwatambulisha kina Harmonize, Raymond pamoja na Rich Mavoko pia na kukabidhi kazi zao, lakini uzuri wakati tunakabidhi kazi Mh Jakaya Kikwete alikuwa amevutiwa na wimbo wa Harmonize wa matatizo, akawa anasema alikuwa kwenye gari aliisikiliza kazi hiyo na kusema kuwa kijana ameimba sana,” Sallam alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV. Sallam alisema hatua ya kukutana na JK wanaimani itawasaidia kuwapa conne...

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 19.09.2016

Image

Fiesta Yawapagawisha Wabunge Na Mawaziri Dodoma

Image
  Mwanamuziki Vanessa na Jux wakitumbuiza kwenye tamasha hilo. Baadhi ya waheshimiwa wabunge waliohudhuria tamasha hilo akiwemo Profesa Maji Marefu (wa pili kulia), Venance Mwamoto (wa kwanza kulia) na William Ngeleja (katikati). Mheshimiwa Waziri Nape Nnauye akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia na Waziri January Makamba. Kundi la weusi likitumbuiza jukwaani kwenye tamasha hilo lililohudhuriwa na mashabiki wengi. Mwanamuziki Adam Mchomvu akitumbuiza mbele ya mashabiki lukuki ndani ya Uwanja wa Jamhuri. Mwanamuziki Belle 9 naye alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha hilo, usiku wa kuamkia leo. Mwanamuziki Darasa akitumbuiza mbele ya mashabiki. Mwanamuziki Darasa akitumbuiza mbele ya mashabiki. Baraka The Prince akitumbuiza usiku wa kuamkia leo. Sehemu ya umati mkubwa wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, usiku wa kuamkia leo. Mwanamuziki Jux akionesha madoido ya kucheza na jukwaa na mpenzi wake ambaye pia ni mwanam...