Posts
WACHEZAJI NETBALL TANZANIA WAPEWA MEDALI ZA DHAHABU
- Get link
- X
- Other Apps
Nahodha wa Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ Dorita Mbunda akivalishwa medali na Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Dora Mushi) Kikosi cha Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ katika picha ya pamoja na Viongozi wa Timu hiyo muda mchache baada ya kuvalishwa medali na Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Dora Mushi) Kikosi cha Timu ya Mpira wa Pete ya JWTZ kikiingia kuvalishwa medali na Mkuu wa Jeshi la Anga wa Rwanda Brigedia Jenerali Charles Karamba baada ya kuchukua ubingwa wa Michuano ya Afrika Mashariki katika Uwanja wa Amahoro Kigali Rwanda( Picha na Dora Mushi) Mkuu wa Msafara wa Timu ya Tanzania Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba (katikati) akiongea na Mchezaji Nasra Suleiman aliyeshika Tu...
BREAKING NEWZZZZZZZ;ALIYEKUWA MKURUGENZI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) NA WENZAKE NANE WAFIKISHWA MAHAKAMANI
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa-NIDA- Dickson Maimu (wa tatu kushoto) n a viongozi wengine nane wa taasisi hiyo wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu mapema leo.Habari zaidi tutawaletea. Mnamo m wezi January 2016, Rais Magufuli aliamua kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) Bwana Dickson Maimu na kumsimamisha kazi yeye na wafanyakazi wengine ili kupisha uchunguzi wa namna ilivyotumika kiasi cha shilingi bilioni 179.6 katika zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya taifa wakati bado kuna malalamiko kwamba watu wengi hawajapata vitambulisho hivyo.
WEMA SEPETU AREJEA NA KITU KIPYA BAADA YA KURUDI KUTOKA SOUTH AFRICA,TEAM YAKE WAMWAGIA SIFA
- Get link
- X
- Other Apps
Papa Francis Awatembelea Waliokua Makahaba Zaidi ya 20 Roma
- Get link
- X
- Other Apps
Roma, Italia Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewashangaza makahaba wa zamani 20 alipowatembelea katika ziara ya kushitukiza kwenye makazi yao yenye ulinzi mjini Roma. Papa Francis alizungumza na wanawake hao, ambao baadhi yao walisafirishwa kutoka Afrika na maeneo mengine ya Ulaya, kwa muda wa zaidi ya saa moja. Wanawake hao waliokolewa kutoka kwenye madanguro walikokuwa wametekwa na mwanamume aliyekua akiwauza kama makahaba na sasa wamepewa makazi na ulinzi katika jengo la ghorofa linalomilikiwa na kanisa katoliki katika Mji Mkuu wa Italia. Papa Francis mwenye umri wa miaka 79 amekua akirejelea mara kwa mara kwamba biashara ya kuwasafirisha binadamu “ni uhalifu dhidi ya binadamu”. Papa Francis aliketi na wanawake hao, wakiwemo wanaigeria saba, waromania sita na wanne kutoka Albania, na kusikiliza habari zao kuhusu namna walivyo lazimishwa ukahaba, ulisema utawala wa Vatican. Wengine watatu katika kundi hilo wanatoka Italia,...