Posts
Magari Waliyozawadiwa Wachezaji wa Leicester City Baaada ya Kutwaa EPL
- Get link
- X
- Other Apps
Magari hayo yalikuwa nje ya uwanja wa Leicester City wa King Power. Mmiliki wa Klabu ya Leicester City, Mthailand Vichai Srivaddhanaprabha amewanunulia wachezaji wake gari aina ya BMW i8 ambayo kila mchezaji aliyewezesha timu hiyo kuchukua ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza msimu uliopita amepatiwa gari lina thamani ya Pauni laki Moja kila moja ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 300 za Kitanzania
ANGALIA PICHA ZA UZINDUZI WA MASHINDANO YA OLYMPIC
- Get link
- X
- Other Apps
Jana Ijumaa, Julai 5, 2016 Mashindano ya Olimpiki 2016 yalizinduliwa rasmi mjini Rio De Jeneiro nchini Brazil na kupambwa na burudani ya tamaduni za nchi hiyo kama kawaida ya mashindano mengine amabayo tumekuwa tukiyaona yakiwemo Fainali za Kombe la Dunia, Uefa Euro na mengine. Pamoja na hivyo ufunguzi wa mashindano hao haukubarikiwa na raia wengi wa Brazil waliojikusanya nje ya uwanja kuandamana kuyapinga. Wananchi hao walipambana na polisi waliotumia mabomu ya machozi kuwatawanya. Ndani ya uwanja huo wa Maracana wenye uwezo wa kuchukua watu 80,000 kulikuwa na viti vitupu vingi.
MAALIM SEIF AWASILI ZANZIBAR AKITOKEA MAREKANI
- Get link
- X
- Other Apps
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sheriff Hamad akiwapungia mkono baaadhi ya wananchama waliofika uwanja wa ndege zanzibar kumpokea akitokea Marekani. Maalim Seif Shari Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi CUF akisalimiana na baadhi ya viongozi waliofika uwanja wa ndege wa Kimataifa Abeid Aman Karume kumpokea. (Picha na Talib Ussi). Na Talib Ussi, Zanzibar Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amerejea Nchini leo akitokea katika ziara zake za Ughaibuni amewataka wanachi na wanachama wa chama hicho kuendelea kuwa na subra. Maalim ameyaeleza hayo nyumbani kwake wakati akitoa salamu kwa wananchgama waliokua kusanya hapo na kuomba kuelezwa chochote. “Tumekutana na watu muhimu katika safari yetu na imekuwa na mafanikio makubwa lakini ni mapema kuwaeleza nini kinaendelea” alieleza Maalim Seif. Alisema kuwa katika safari yake hiyo amepokewa vizuri...