MAALIM SEIF AWASILI ZANZIBAR AKITOKEA MAREKANI
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sheriff Hamad akiwapungia mkono baaadhi ya wananchama waliofika uwanja wa ndege zanzibar kumpokea akitokea Marekani. Maalim Seif Shari Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi CUF akisalimiana na baadhi ya viongozi waliofika uwanja wa ndege wa Kimataifa Abeid Aman Karume kumpokea. (Picha na Talib Ussi). Na Talib Ussi, Zanzibar Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amerejea Nchini leo akitokea katika ziara zake za Ughaibuni amewataka wanachi na wanachama wa chama hicho kuendelea kuwa na subra. Maalim ameyaeleza hayo nyumbani kwake wakati akitoa salamu kwa wananchgama waliokua kusanya hapo na kuomba kuelezwa chochote. “Tumekutana na watu muhimu katika safari yetu na imekuwa na mafanikio makubwa lakini ni mapema kuwaeleza nini kinaendelea” alieleza Maalim Seif. Alisema kuwa katika safari yake hiyo amepokewa vizuri na kueleza matatizo ya kubakwa kwa demokra