Posts

Waziri Mkuu: Nitahamia Dodoma Septemba Mwaka Huu

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  alipokuwa akiwasalimia na kuwashukuru mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi  waliojitokeza kushuhudia  maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma. *Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi. Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma. “Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma waliohudhuria maadhimisho hayo.

Mtuhumiwa Mauaji ya Mwangosi Akutwa na Hatia.

Image
Daud Mwangosi. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa leo imemtia hatiani, Pacificius Cleophace Simon ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa  mwandishi wa habari wa Channel Ten na Mwenyekiti  wa Chama cha Waandishi wa  Habari Mkoa  wa  Iringa, Daud Mwangosi kwa kuua bila kukusudia. Mahakama imesema itatoa hukumu ya kesi hiyo keshokutwa Julai 27, mwaka huu. Pacificius anatuhumiwa kumuua Mwangosi katika tukio lilitokea katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi Mkoani Iringa Septemba 2, 2012.

Babu Seya taabani

Image
yaStori: Elvan Stambuli, Wikienda DAR ES SALAAM: Mwanamuziki nguli nchini anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’ anadaiwa yu taaban ambapo amekimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa matibabu. Mwandishi wetu alimshuhudia Babu Seya akiwa Muhimbili chini ya ulinzi wa askari magereza watatu na wafungwa wengine watano katika Jengo la Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) huku akiwa amedhoofu. Haikuweza kujulikana mara moja ugonjwa uliosababisha Babu Seya ahamishiwe Muhimbili kwa matibabu kwa sababu Jeshi la Magereza lina hospitali yake na mwandishi alipoomba kwa mmoja wa askari magereza ili aweze kumsalimia mwanamuziki huyo, hakupewa ruhusa. Baadhi ya wananchi waliomshuhudia mwanamuziki huyo akiwa Muhimbili na kuingizwa katika chumba cha daktari namba 112 walisema, anavyoonekana ni dhahiri ni mgonjwa kwa sababu hakuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake. “Nguza (Babu Seya) mara nyingi huwa mchangamfu lakini leo ameku

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 25.07.2016

Image

MAGAZETI YA UDAKU LEO TAREHE 25/7/2016

Image

BREAKING NEWSS: BAADA YA JPM KUWA MWENYEKITI CCM,ZITTO ATOA UJUMBE HUU DHIDI YAKE

Image
KATIKA hali isiyo ya kawaida,Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo leo hii muda mfui tu mara baada ya Rais Magufuli kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa tano wa CCM,aliasambaza ujumbe mzito mitandaoni kuhusu hatua hiyo. Zitto ambaye mara kadhaa amekuwa akisikika kumtuhumu JPM kuwa ni Dikteta,aesambaza ujumbe huo wenye lengo la kumpongeza Dr JPM  na kuhaidi kuwa atampa ushirikiano ote unaohitajhika katika kuboresha siasa ya tanzania. Facebook Comments

Mlipuko Waua 80 Afghanistan

Image
Wizara ya afya  nchini Afghanistan imesema takribani watu 80 wameuawa na zaidi ya wengine 150 kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga lililofanyika kwenye Mji Mkuu Kabul. Baadhi ya taarifa zinasema kulikuwa na milipuko miwili. Shambulio hilo linaonyesha kuwa lililenga maandamano ya maelfu ya watu kutoka jamii ndogo ya Hazara, ambao hujikuta wakidhalilishwa na kufanyiwa ukatili. Walikuwa wakiandamana kupinga mpango wa serikali wa kuhamisha umeme kutoka kwenye majimbo yao katikati ya nchi.

WOLPER AREJEA CCM

Image
Wolper akitangaza sababu za kurejea CCM. Wolper akiongea na Mwenyekiti Mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete. Wolper akiongea wakati wa hafla ya wasanii ya kumuaga Mwenyekiti Mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete. Na Leonard Msigwa/GPL MWANADADA gumzo kwenye tansia ya Bongo Movie nchini, Jacqueline Wolper hatimaye jana ametangaza rasmi kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM). Wolper ambaye alikuwa kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mfuasi mkubwa wa aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa alitangaza uamuzi huo wakati wa hafla ya wasanii ya kumuaga Mwenyekiti Mstaafu Mhe. Jakaya Kikwete mjini Dodoma. Baada ya kupewa nafasi kuongea, Wolper alikuwa na haya; “Nilipotea kwenda kule, nimeamua kurudi nyumbani” Ikumbukwe kwamba Wolper alikuwa mstari wa mbele miongoni mwa wasanii wa kike nchini kumpigia debe bila kificho Edward Lowassa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana na alienda mbali zaidi kwa kumwita Edward Lowassa kam

Msindai arudi CCM

Image
Mgana Msindai (kulia) akiongea jambo. ALIYEKUWA Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida na baadaye kuhama chama na kujiunga na Chadema, Mgana Msindai amerudi CCM leo.  Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman  Mbowe alipokuwa akimkabidhi kadi Mgana Msindai (katikati). Msindai alitangaza uamuzi huo leo mjini Dodoma baada ya kupewa nafasi na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete wakati anaendesha mkutano mkuu wa CCM uliomchagua Rais Dk John Magufuli kuongoza chama. Msindai alisema aliamua kurudi CCM baada ya kuona hakuna cha kupinga baada ya Rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais wa nchi. Msindai aliingia Chadema baada ya aliyekuwa mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa kujiunga na Chadema mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu.

Rais Magufuli avunja rekodi ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa

Image
Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amevunja rekodi baada ya kutangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa kupata asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa. Rekodi hiyo ya kupata asilimia 100  ya kura zote kwenye uchaguzi wa aina hiyo (Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa) haijawahi kufikiwa na kiongozi yeyote ndani ya CCM tangu kuanzishwa kwa chama hico Februari 5, 1977 ambapo ni miaka 39 sasa. Wenyeviti wa CCM waliyopita ambao ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa wala Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete hawakuwahi kupata kura zote zilizopigwa kwenye uchaguzi wa ngazi hiyo. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliyofanyika mjini Dodoma leo, Mwenyekiti wa CCM aliyemaliza muda wake, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema matokeo kuwa; ifuatavyo Kura zilizopigwa zilikuwa ni 2398, kura halali ni 2398, kura zilizoharibika ni 0, kura za hapana ni 0 na kura za Ndiy

NITAHAKIKISHA SERIKALI INAHAMIA DODOMA :RAIS MAGUFULI

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM uliofanyika mjini Dodomabaada ya kuchaguliwa kwa kupigiwa kura za kishindo leo, kulia anayecheka ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mzee Benjamin Williamo Mkapa.. Na. Immaculate Makilika- Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amesema katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha Serikali inahamishia makazi yake mjini Dodoma. Amesema hayo leo, wakati alipokuwa  akihutibia wajumbe  wa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika Mkutano Mkuu Maalumu  wa  Chama hicho uliofanyika  mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti. “Nitahakikisha katika awamu ya uongozi wangu, Serikali inahamia Dodoma, najua viongozi wengine wote nao watanifata, kwa kuwa sasa miundombinu ya Dodoma inaweza kukidhi mahitaji yote” alisema Rais Magufuli. Rais Magufuli aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi nane ya uongozi wake chini ya Serikali ya

JK AKABIDHI RASMI KIJITI CHA UENYEKITI KWA DKT JOHN POMBE MAGUFULI JIONI YA LEO MJINI DODOMA

Image
 Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake Dkt Jakaya Kikwete pamoja na Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli wakiwapungia mkono Wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum mara baada ya matokeo kutangazwa rasmi na Dkt John Pombe Magufuli kuibuka kwa kura zote za ndio ziapatazo 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika. Mwenyekiti Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akimkumbatia Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka kumi.   Mwenyekiti aliyemaliza muda wake leo,Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi mbalimbali vya chama cha Mapinduzi (CCM),Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli aliyepigiwa kura na Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum na kuibuka na kura zote za ndio kutoka kwa Wajumbe 2398 na hakuna kura zilizokuwa zimeharika  Makamu Mwenyekiti-Zanzibar Dkt Shein akimpongeza Mwenyekiti Mpya,Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa kuw

Lowassa na Sumaye Wapewa MAKAVU Ndani ya Mkutano wa CCM .........Mpendazoe Ahamia CCM, Mrema Alalama Kuitwa CCM B

Image
VIGOGO mashuhuri wa Chadema waliowahi kuwa mawaziri wakuu; Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana waligeuka gumzo ndani ya Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kumchagua Rais John Magufuli, kuwa Mwenyekiti wa tano wa chama hicho. Gumzo hilo, lilianzishwa na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba, alimpomtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuko na Uzima, Josephat Gwajima, asimpotoshe Magufuli ili yasije yakampata ya Sumaye, ambaye sasa anachezea mchangani Kibaha. Sumaye mchangani “Hata akina Sumaye hawakuunda vyama vyao. Bado wanahangaika; na sasa Sumaye anacheza mchangani Kibaha,”  alisema Makamba. Sumaye ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu na NEC ya CCM, kwa sasa anawania uongozi wa Kanda ya Pwani katika Chadema. Kabla ya kusema kuwa Sumaye anahangaika na siasa za mchangani, Makamba alimtaka Gwajima kuacha uongo na kusingizia viongozi wa CCM. Makamba aliyepewa nafasi ya kumuombea kura Rais John Magufuli kwa wajumbe wa Mkut

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WANAWAKE WA MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe Wanawake wa Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma ambapo aliwasihi kuendelea kudumisha umoja na mshikamano pamoja na kujishughulisha na shughuli mbali mbali za kiuchumi na kujiunga na Mabaraza mbali mbali ya kuwezesha wanawake.  Baadhi ya Wajumbe walishindwa kujizuia na kuamka kwa shangwe na vifijo.  Mke wa Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ,wilaya ya Lindi Mama Salma Kikwete akizungumza na Wajumbe Wanawake wa Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma .  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson akungumza kwenye mkutano uliowakutanisha Wajumbe Wanawake wa Mkutano Mkuu wa CCM pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma. Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tan