Posts

Mbunge Chadema Avuliwa Ubunge

Image
Aliyekuwa Mbunge wa Longido, Mhe. ONESMO NANGOLE. Kesi iliyokuwa inaunguruma kuanzia tarehe 29.02.2016 katika Mahakama Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii. Katika shauri hilo aliyekuwa mgombea Ubunge wa CCM, Jimbo la Longido, Dk. KIRUSWA alifikisha mahakamani shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi dhidi ya Mbunge wa Longido, Mhe. ONESMO NANGOLE. Akisoma hukumu hiyo, Jaji MWAGESI alisema kwamba mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa na Wakili Dk. Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka. Katika shauri hilo, dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikuwa ni; 1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa Mhe. Onesmo Nangole 2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mhe. Nangole 3.Kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura 4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje. 5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matok

MKUFUNZI WA MASWALA YA BIASHARA NA MASOKO REHEMA KASULE AWAPA ELIMU MANJANO DREAM MAKERS

Image
Mkufunzi wa maswala ya biashara Mama Rehema Kasule kutoka nchini Uganda akiwapa elimu wanafunzi wa Manjano Foundation jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwenye majukumu yao ya kila siku ikiwemo kutengeneza uhusiano na watu waliofanikiwa kwa kuwa itasaidia kujifunza mengi. Pia namna ya kujiamini kuwaza mafanikio zaidi kuwa lazima wafanikiwe na kuachana kabisa na mawazo ya kushindwa akiwa sambamba na Afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions, Mama Shekha Nasser.  Akieleza zaidi Mama Kasule amewataka Washiriki wa Manjano Dream Makers kama wanataka kufanikiwa kazi zao za upambaji na biashara zao ni lazima wafanye kwa moyo mmoja kutoka ndani ya nafsi pia kuachana na fikra za kukata tamaa na maneno ya watu ya kuwakatisha tamaa. Kwa upande afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na Mkurugenzi wa Manjano Foundation mama Shekha Nasser amewataka washiriki hao kuongeza juhudi pia kuyatekeleza kwa vitendo yale yote waliofundishwa katika mafunzo hayo. Mama Rehmah Kasule al

TP MAZEMBE YAIKONG’OLI YANGA KAMOJA UWANJA WA TAIFA

Image
Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Obrey Chirwa akiichambua ngome ya timu ya TP Mazembe, katika mtanange uliopigwa jioni hii kwenye dimba la Taifa (Uwanja wa Taifa) Jijini Dar es salaam, ikiwa ni Mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Hadi kupanga cha mwisho kinalia, Yanga wamelala kwa bao 1-0.(Picha na michuziblog) Mashabiki wakiwa wamefurikwa kwenye uwanja wa Taifa hata hivyo mwishowe wakaondoka vichwa chini baada ya timu yao kupoteza mchezo huo mbele ya mahasimu wao TP Mazembe

SEKTA YA MAWASILIANO KUPATA MWEKEZAJI ZAIDI

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake kwa nia ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Oracle Afrika Bw. Cherian Varghese (katikati) akielezea nia ya Kampuni yao katika ushirikiano wa kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA hapa nchini. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Dkt. Mhandisi Maria Sasabo (wa kwanza kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika walipotembelea sekta ya Mawasiliano na kueleza nia yao ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA. ……………………………………………………………………………. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uc

Black Coffee Ashinda Tuzo ya BET ya Best International Act Africa

Image
Black Coffee baada ya kupokea tuzo yake. Black Coffee akiwa na mkewe Enhle Mbali Mlotshwa. Black Coffee na mkewe wakiwa kwenye pozi na baadhi ya mastaa kutoka Afrika akiwemo Akon na AKA.   Black Coffee katika pozi. Black Coffee amekuwa mwanamuziki wa kwanza kutoka Afrika Kusini kutwaa tuzo ya BET katika kipengere cha ‘Best International Act Africa 2016’ na kuwapiku mastaa wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo akiwemo Diamond Platnumz. Black Coffee mwenye umri wa miaka 40, ametwaa tuzo hiyo huko Los Angeles nchini Marekani akiwabwaga wasanii wenzake ambao ni AKA‚ Cassper Nyovest‚ Diamond Platnumz‚ MzVee‚ Serge Beynaud‚ Wizkid na Yemi Alade waliokuwa wanawania tuzo hiyo.

Rais Magufuli Afanya Mabadiliko ya Ma RC na Ma DC

Image
Rais Dk. John Pombe Magufuli. Rais Dk. Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, atengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo na kuteua Ma DC 139. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika safu ya wakuu wa mikoa na amewateua wakuu wa wilaya 139. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam am

Meli ya Mizigo Yazama Unguja

Image
Zoezi la uokoaji likiendelea eneo ilipozama meli ya MV Happy. Meli ya mizigo iitwayo MV Happy iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Zanzibar imezama leo asubuhi kwenye Bahari ya Hindi eneo la Chumbe, Unguja. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba meli hiyo ilianza kuzama majira ya saa 10 alfajiri na kufikia saa moja asubuhi ilikuwa imezama kabisa ndani ya maji. Wananchi wakishuhudia zoezi la uokoaji. Mpaka sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa bali mizigo iliyokuwemo kwenye meli hiyo ndiyo iliyozama. Taarifa zaidi zitaendelea kuwajia kupitia tovuti hii.

Tanzia: Aliyekuwa Mbunge wa Biharamulo Magharibi (2010-2015) Afariki

Image
Dk. Antony Gervase Mbassa enzi za uhai wake. Aliyekuwa Mbunge wa Biharamulo Magharibi (2010-2015) kupitia CHADEMA, Dk. Antony Gervase Mbassa amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake.

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MPANGO WA KITAIFA WA KITUO CHA MAWASILIANO CHA JESHI LA POLISI (CALL CENTRE)

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest  Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine  wa sekta ya umma na binfasi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akikagua kituo cha mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi. .Pamoja naye ni Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest  Rwegasira, IGP Ernest manu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine  wa sekta ya umma na binfasi. Rais

PICHA 5: Muonekano wa helicopter inayotengenezwa Arusha

Image
Mtanzania Injinia Abdi Mjema ndiye anayeitengeneza helicopter hiyo katika chuo cha  ufundi Arusha na hadi kufikia mwezi wa saba mwanzoni itaanza majaribio ya awali, helicopter itakuwa na uwezo wa kuchukua abiria wawili na mpaka sasa shilingi million  3 zimeshatumika.

Kajala Akanusha Kutoka Kimapenzi na Msami

Image
Kajala na Msami Katika Pozi Msanii wa filamu Kajala Masanja amekanusha tetesi za kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatoka kimapenzi na mkali wa wimbo ‘Mabawa’, Msami. kajala Mwingizaji huyo ambaye hivi karibuni ilisambaa video inayomuonyesha akidendeka na rapa Quick Rocka, ameiambia Clouds Fm kuwa Msami ni mshkaji wake wa karibu sana na sio mpenzi wake. “Unajua kuna watu wanaweza wakawa labda ni washikaji au wana vitu vingi pembeni lakini watu wengine hawajui, mi na Msami ni washkaji sana,” alisema Kajala. Aliongeza, “Halafu sio kila siku watu watakuwa wanatuona barabarani au tunapostiana picha kwenye Instagram, lakini mimi na yeye tunaongea vitu vingi, kwa hiyo imekuwa rahisi mimi kuacha usingizi wangu kuja kwa Msami, sina uhusiano naye na vitu vingine mtavijua baadaye.” Wawili hayo wamekuwa wakioneka wakiwa pamoja mara nyingi hali ambayo imeibua hisia huenda wakawa wanatoka kimapenzi.

Wema Atoboa Siri Yake na Zari

Image
Wema Sepetu. Stori: Imelda Mtema, Ijumaa Dar es Salaam: Kwa mara ya kwanza, staa kiwango kunako sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ ametoboa siri iliyofichika anayoijua mwenyewe kati yake na mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akieleza kuwa, hajawahi kumchukia wala kufikiria kumchukulia bwana’ke ila baadhi ya wapambe wake wamekuwa wakichochea kuwepo kwa bifu kati yao.   Zari. KISIKIE CHANZO Mmoja wa watu wa karibu wa mlimbwende huyo wa Tanzania mwaka 2006/07 aliyeomba jina lisichorwe gazetini aliling’ata sikio Ijumaa kuwa, Wema amekuwa akiumizwa na madai kuwa anamchukia Zari ‘Mama Tiffah’ wakati katika uhalisia siyo hivyo. “Wema amekuwa mgumu sana kumzungumzia Zari lakini safari hii ni kama uzalendo umemshinda kutokana na maneno ya watu hasa hili la kumzushia kuwa karudiana na Diamond. “Mwenyewe anasema hana tatizo na Zari ila hizi Timu Zari, Timu Diamond na Timu Wema ndizo zinachochea mam