Posts

TAKUKURU WAZINDUA KAMPENI YA LONGA NASI JIJINI DAR LEO.

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba kuashiria uzinduzi wa gari la matangazo ya Kampeni ya kupambana na Rushwa ya LONGA NASI kwa kupiga namba 113 na kutuma kutuma sms kwenda namba 113 ili kutoa taarifa ya kutoa au kupokea Rushwa kwa TAKUKURU. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za watu wanaotoa rushwa au kupokea rushwa kwaajili ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 unayoweza kupiga na kutuma sms za kawaida  Uzinduzi huo umefanyika leo  katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam. Mkuu wa Kitengo cha Tehama TAKUKURU, Neema  Mwalyelye akitoa maelekezo kwa  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea kwenye  ban

Tamko la Madiwani Misungwi: Kitwanga Hakulewa Kama Ilivyopotoshwa.

Image
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga. UTANGULIZI Ndugu Waandishi wa habari, Karibuni kwenye mkutano huu mfupi ambao lengo lake ni kutoa taarifa yetu fupi kuhusu ukweli uliojificha kuhusu kitendo kilichopelekea Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga. Tunaamini kwa uwezo mliona kama waandishi wa habari, taarifa hii itafikia umma wa Watanzania kama ilivyokusudiwa. UFAFANUZI Kama mnakumbuka mnamo tarehe 20 Mei mwaka huu, Rais Dk John Pombe Magufuli alichukuwa uamuzi wa kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga ambaye pia ni Mbunge wa Misungwi kwa kosa la kwamba Mhe. Kitwanga aliingia bungeni akiwa amelewa. Sisi wananchi wa Jimbo la Misungwi tumesikitishwa sana na taarifa na uamuzi huu kwa kuwa tunaamini kuwa kuna dhamira iliyojifika iliyopelekea Mhe Rais kufanya maamuzi haya. Ukweli ni kwamba huu ulikuwa mpango wenye dhamira ovu na uliogubikwa na uongo mwingi uki

Wakili Hashim Rungwe Aishauri Serikali Mambo Mazito

Image
Wakili Hashim Spunda. MMOJA wa wagombea Urais na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Umma (Chauma), Wakili Hashim Spunda Rungwe amefanya mahojiano maalum na wahariri wetu ili kutoa tathmini yake ya utawala wa miezi sita wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Pombe Magufuli tangu ashike madaraka ya kuongoza nchi. *Azungumzia mbinu ya kupunguza bei ya sukari, asema watu wana njaa! Wakili Rungwe ameshauri mambo mazito ya nini cha kufanya ili nchi iweze kusonga mbele kimaendeleo. Hata hivyo, ametoa maoni juu ya mjadala wa Bunge kutooneshwa laivu na sakata la sukari, fuatana nasi katika makala haya ujue kile alichokisema: Tupe maoni yako kuhusu utawala wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye amefikisha miezi sita akiwa madarakani, je, anakwenda vizuri? Rungwe: Miezi sita ya Serikali ya Awamu ya Tano sijasikia mpango wowote wa kuondoa njaa kwa wananchi. Lazima rais ajue kwamba watu wana njaa na zifanyike juhudi kuhakikisha kipato kwa mwananchi mmojammoja kinaon

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 24.05.2016

Image

RAIS MAGUFULI ATEUA NAIBU AG NA MSHAURI WAKE WA UCHUMI

Image
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akisoma taarifa ya Uteuzi wa viongozi mbalimbali uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23 Mei, 2016 imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mar

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA

Image
Mbunge wa CCM, Mhe. Mary Mwanjelwa akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge Mhe Najma Murtaza Giga akiwasili Bungeni kuongoza vikao vya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Mhe. Ally Keissy akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ameongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Jumanne Maghembe wakielekea Bungeni kuhudhuria vikao vya bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Naibu Waziri, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Masiliano, Mhe. Eng. Edwin Ngonyani akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhudhuria vikao ndani ya Bunge hilo leo 23 Mei, 2016 mjini Dodoma. Naibu Waziri, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Hamis Kingwangalla akiwasili viwanja vya Bunge mjini Dod