Posts

EXCLUSIVE: Rachel Kizunguzungu amrudia Mungu… ni baada ya yote aliyofanya na kupitia.

Image
Mwimbaji Rachel ambaye ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kujiunga na nyumba ya vipaji Tanzania ( THT ) na kuanza kuachia nyimbo zake, amekaa kwenye Excluvie na mtangazaji wa Amplifaya ya CloudsFM Millard Ayo na kueleza kilichotokea mpaka akakwama na kukaa kwenye nchi ya watu kwa zaidi ya miezi saba, ishu yake ya kuvuta bangi na mengine. KUHUSU KUMRUDIA MUNGU:   Ni kweli nimemrudia Mungu, ni maamuzi ambayo nimeyafanya mwenyewe baada ya kuona vitu ni vilevile, dunia ni ileile na watu ni walewale ndio maana nikaona sio vibaya nikaja na upande mwingine lakini hii haimaanishi kwamba nitakua nafanya muziki wa Injini, nitaendelea na bongofleva lakini muda mwingi nitautumia kanisani. KUHUSU OMAN: ‘Ni kweli nimekaa nchini Oman kwa zaidi ya miezi saba, nilikwenda kwa ajili ya kufanya shows tu lakini nikapata tatizo kwenye VISA yangu, nilifanya show za kuandaa mwenyewe ikafanikiwa mwanzoni lakini baadae hali ikabadilika, nilikua na VISA ya miezi mitatu na...

WEMA SEPETU AFUNGUKA JUU YA MCHEZAJI HARUNA NIYONZIMA

Image
Ibrahim Mussa, Dar es Salaa BAADA ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola, msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, amefunguka kuwa hajui ni kwa nini amekuwa akimpenda kiungo wa timu hiyo, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima. Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Championi Jumatatu lilimshuhudia msanii huyo ambaye pia alikuwa Miss Tanzanani mwaka 2006, akiwa amekaa Jukwaa la VIP A kwa ajili ya kutoa sapoti kwa timu yake hiyo. Akizungumza na Championi Jumatatu, Wema alisema kuwa upendo wake kwa kiungo huyo ni mkubwa mno kiasi kwamba hajui kwa nini inakuwa hivyo, lakini akaongeza kuwa inawezekana kuwa ni kutokana na uwezo wake anaouonyesha uwanjani ambapo katika mchezo huyo aliwapa wakati mgumu viungo wa Esperanca. “Mimi ni shabiki wa Yanga damu kabisa, tangu nazaliwa na utabiri wangu umeenda vizuri, maana nilisema kabla ya mchezo kuwa tutashinda na imekuwa kweli, ushindi huo n...

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI YA KUPAA KWA BWANA KATIKA PAROKIA YA TOLEO LA BWANA JIMBO LA ARUSHA

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia waumini aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.  Sehemu ya waumini wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa akiwsalimia  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia na wanakwaya  aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia baadhi ya watawa aliposhiriki ibada ya Jumapili ya Kupaa kwa Bwana katika Parokia ya Toleo la Bwana jimbo la Arusha leo Mei 8, 2016.    Rais wa Jamhuri y...

WAZIRI WA MAGUFULI AKWAA KISIKI JIMBONI KWAKE,APEWA MAJI MACHAFU ANYWE.

Image
Kijiji cha Nala na vitongoji vyake juzi walimpelekea maji machafu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Anthony Mavunde wakimtaka ayanywe kwa kuwa ndiyo wanayotumia. Mavunde alikutana na mkasa huo muda mfupi alipoingia kwenye kijiji hicho umbali wa kilomita tisa nyakati za jioni, ambako wakazi wa eneo hilo walikuwa wakimsubiri tangu asubuhi. Mama mmoja aliyekuwa eneo hilo, alifika na chupa ya maji akimtaka Naibu Waziri ayaonje mbele yao, kwani nao ni binadamu kama yeye na wanayatumia, lakini Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Paul Luhamo alimzuia kuyanywa.Pamoja na taarifa ya kijiji iliyotolewa na Ofisa Mtendaji wa Kata, Mathias Ndologa, wakazi hao walilipuka na kupiga kelele wakiipinga taarifa hiyo kwamba iligusa kwa juu matatizo yao, lakini ikaacha jambo kubwa la maji. Kwenye risala yake, Ndologa alikuwa ameelezea suala la maji, umeme, miundombinu na upungufu wa madawati, lakini kelele zilizidi kutoka kw...

LEICESTER CITY YAKABIDHIWA KOMBE LAO LA LIGI KUU ENGLAND

Image
 Leicester City wamesherekea ubingwa wao wa Premier League ambao ni wa kwanza katika historia ya klabu hiyo tangu ilipoanzishwa miaka 132 iliyopita. Furaha hiyo imechagizwa na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa King Power. Leicester wamekabidhiwa rasmi ubingwa wao baada ya kujihakikishia kutwaa taji hilo tangu siku ya Jumatatu wakati Tottenham iliposhindwa kuifunga Chelsea. Klabu hiyo imeandika historia ambayo imeuteka ulimwengu ambapo nahodha Wes Morgan pamoja na kocha Claudia Ranieri kwa pamoja walinyanyua taji la Premier League baada ya kumaliza safari ya kupambana kutoshuka daraja hadi kutwaa ubingwa katika kipindi cha miezi 12. Ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Everton ulikuwa unaendelea kudhihirisha uwezo, kujitoa na ubora uliowapa ubingwa, lakini siku ya Jumamosi ya May 7 ni zaidi ya mchezo wa soka kutokana na kufunikwa na hisia za kila aina.

DUNIA INA MAMBO MAZITO BI HARUSI AMPA SUMU MUMEWE

Image
Msichana mdogo alieolewaBi harusi wa miaka 14 nchini Nigeria ameshtakiwa kwa kuwaua watu wanne akiwemo mumewe wa miaka 35 baada ya kuweka sumu ya panya katika chakula alichoandaa kwa sherehe za haruysi yake. Kesi hiyo imewashangaza wahaharakati wa haki za kibinaadamu ambao wamesema kuwa msichana aliyeozwa kwa mume aliye mara mbili umri wake anafaa kuchukuliwa kama mwathiriwa na wala sio muhalifu. Wasila tasiu kutoka familia masikini katika eneo la waislamu la kazkazini huenda akakabiliwa na kifo iwapo atahukumiwa. Shahidi wa kwanza wa kiongozi wa mashtaka Lamido Abba Sorron-Dinka alikuwa msichana wa miaka 7 anayejulikana kama hamziyya,ambaye alikuwa akiishi katika nyumba moja na Tasi'u pamoja na mumewe Umar sani,wakati bi haru huyo alipoweka sumu ya panya katika chakula hicho. Hamziyya alijulikana tu kama dadaake mke wa kwanza wa bwana Sani,mwanamke aliyeolewa na marehemu awali katika eneo ambapo ndoa za wake wengi zimekithiri. Msichana huyo wa miaka 7...

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA BI LUCY KIBAKI

Image
 Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.  Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo kuhifadhi utu na wema katika familia.  Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya.

RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI MAAFISA 586 KATIKA CHUO CHA MAAFISA WA JESHI MONDULI

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride kabla ya kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 586 wa jeshi la Wananchi wa Tanzania kundi la 58/15 katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi cha Monduli TMA mkoani Arusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Afisa Mpya wa cheo cha Luteni Usu, Nasra Rashid ambaye alifanya vizuri zaidi kuliko Maafisa Wanafunzi wanawake katika chuo c...