Mama Salma Kikwete afunguka maisha yake kama mama
Mke wa rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma Kikwete amevitaja vitu anavyovipenda kufanya akiwa nyumbani. Mama Salma Kikwete ni msimamizi mkuu wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, inayowasaidia kuwasomesha watoto wa kike wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi. Akifanya mahojiano na waandishi wa habari wa Clouds Media waliomtembelea nyumbani kwake kuelekea siku ya mama duniani, siku ya Jumapili, Mei 8, amesema, “Mimi ni mama wa watoto tisa, kulea watoto tisa haikuwa shughuli ndogo lakini nashukuru Mungu kwa baraka ya kuwapata watoto wangu. Watoto wangu wamekuwa wakisaidiana sana wakati wa kuleana na kushirikiana katika kila jambo. Ukiacha hao tisa nina watoto wengine ninaowasomesha nina watoto wengi sana, nawapenda sana wanangu naamini hata wao wananipenda pia.” Aidha Mama Salma aliongeza, “ninapoona wanangu wanaandikwa vibaya kwenye magazeti, nachukizwa na jambo hilo kama mzazi, lakini natambua haya yanatokana na maisha tuliy