Posts

HATIMAYE Snura awaomba radhi Watanzania, awasilisha video safi ya Chura kukaguliwa

Image
Snura amewaomba radhi watanzania kwa video ya wimbo wake ‘Chura’ inayowadhalilisha wanawake na iliyo kinyume na maadili. Snura akiongea na waandishi wa habari Alhamis hii Muimbaji huyo amekutana na waandishi wa habari Alhamis hii kwenye ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Jana video na wimbo huo vilifungiwa na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kwa madai kuwa inakiuka maadili ya Kitanzania. Pia alizuiwa kufanya maenesho ya hadhara kwakuwa hajajisajili kwenye baraza la sanaa la taifa, BASATA. Kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Snura amedai kuwa tayari amekamilisha mchakato wa usajili na BASATA imempa kibali. Pia amedai kuwa amewasilisha video mpya ya wimbo huo kwa bodi ya filamu ya Tanzania ambayo itaikagua.

Kikwete 'Agoma' Kumkabidhi Rais Magufuli Chama......Mwinyi,Mkapa,Malecela Kukutana kwa Dharura Kumjadili

Image
Hali si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na mchakato unaoendelea wa kumkabidhi Rais Dk. John Magufuli uenyekiti wa chama hicho, kukumbwa na sintofahamu. Taarifa kutoka ndani kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC), kilichofanyika juzi Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, zimethibitisha kutokea mgawanyiko wa vigogo ndani ya chama hicho. Hali hiyo imekuja baada ya kutokea kwa mvutano juu ya tarehe rasmi ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu uliopangwa Juni mwaka huu, ambao pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete atakabidhi kijiti kwa Rais Magufuli. Chanzo cha kuaminika ndani ya kikao hicho kilidokeza  kuwa, kabla kilifanyika kikao kidogo kilichokuwa na wajumbe wanne ambao pamoja na mambo mengine walijadili ajenda muhimu  ikiwamo ya kupanga tarehe kwa ajili ya mkutano huo. Kwa mujibu wa chanzo hicho, kikao hicho kidogo kilishirikisha viongozi wanne akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya

REAL MADRID WAICHAPA MAN CITY KWA BAO 1-0 NA KUTINGA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Image
Real Madrid imefanikiwa kufuzu kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa Mei 28 jijini Milan, Italia. Madrid imetinga fainali baada ya kuitwanga Man City kwa bao 1-0 katika mechi ya pili ya nusu fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid. Bao la Madrid limepatikana baada ya shuti la Gareth Bale aliyekuwa akipiga krosi kumgonga Fernando na kujaa wavuni. Pamoja na Madrid kutinga fainali, maana yake Kocha Zinedine Zidane ameandika rekodi yake ya kwanza kucheza fainali hiyo, safari hii akiwa kocha. Lakini Man City imeishia nusu fainali iliyokuwa ni mara ya kwanza kwake kuingia Ushindi huo wa bao 1-0, unaipitisha Madrid hadi fainali baada ya sare ya bila bao katika mechi ya kwanza jijini Manchester.

Mauaji ya Kutisha Kaole Bagamoyo Jana Jioni..Mama na Mtoto Wachinjwa Kama Kuku

Image
TAARIFA YA MAUAJI.BAG/IR/1078/2016.MNAMO 04/05/2016 MAJIRA YA SAA 16.30HRS HUKO KAOLE KWENYE VICHAKA KATA YA DUNDA (W)B'YO(M)PWANI OLVER S/O ERASTO,22YRS,MCHAGA,MKULIMA, WA KAWE DSM NA MTOTO WAKE EMMANUEL S/O FROWIN PETER,3YRS MHEHE WOTE WALIUAWA KWA KUCHINJWA SHINGONI KWA KUTUMIA KISU NA MME WAKE FROWIN S/O PETER,MBWALE,26YRS,MHEHE,DEREVA,MKAZI WA KAWE DSM AKISHIRIKIANA NA RAFIKI YAKE RAJABU S/O JUMA,20YRS,MKULIMA,MKAZI WA MAKONGO DSM.MIILI YAO IMEKUTWA UMBALI WA MITA 100 KUTOKA BARABARANI.CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI WIVU WA MAPENZI AMBAPO MUME WA MAREHEMU ALIMUHISI KUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA MTU AITWAYE HAMZA S/O ? MKAZI WA KAWE DSM .MBINU ALIMDANGANYA KWAMBA WAODOKE PAMOJA NA MTOTO WAO KWENDA KAOLE BAGAMOYO KUANGALIA NYUMBA YAO ANAYOENDELEA KUJENGA WALIKODI PIKIPIKI MC 235 AWR FECON HADI KAOLE PORINI.WATUHUMIWA WAMEKAMTWA NA WAMEKIRI KUFANYA MAUAJI HAYO = Samahani kwa Kuficha Picha , Sio Nzuri Watu wawili mama na mtoto wamenyongwa hadi kufa ki

BREAKING NEWS : SNURA AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA SANAA,VIDEO YA CHURA YATAKIWA KUFUTWA MTANDAONI

Image
 snura katika pozi Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla akiongea na waandishi wa habari Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza kumfungia Snura kujihusisha na masuala ya sanaa. Pia imeufungia wimbo wake Chura pamoja na video yake kutochezwa kwenye redio na TV nchini. Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo jijini Dar. Uamuzi wa kumfungia umekuja kutokana msanii huyo kutojisajili kwenye Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA.

Sumaye Amkejeli Rais Magufuli kwa kazi anayofanya

Image
FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na kuchukia kukosolewa Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli ameleza kushangazwa na hatua ya serikali kuminya uhuru wa habari na kwamba, kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu yanayofanywa na watendaji wake.   “Wapowatawala ambao hawapendi kusemwa lakini wanapenda sana kusifiwa. Kiongozi mwenye tabia ya udikteta hataki kusikia kingine zaidi ya sifa zake tu.   “Huyo ni mtu hatari na katika nchi ya namna hiyo hakuna uhuru wa habari wala uhuru wa kutoa maoni kwa woga wa kupotezwa kusikojulikana,” amesema Sumaye. Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoratibiwa na Cha

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOANI DODOMA

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakielekea kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipowasili mkoani Dodoma kwa ajili ya kikao hicho cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendesha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa kilichofanyika Mkoani Dodoma. K

Mwili wa Papa Wemba Wawasili DRC

Image
Kinshasa, Kongo Mamia ya watu wamekusanyika leo nje ya Uwanja wa Ndege wa Kinshasa nchini Kongo wakisubiri mwili wa mwanamuziki aliyefariki Jumapili iliyopita, Papa Wemba kuwasili nchini humo. Zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Papa Wemba litafanyika wiki ijayo Jumatatu katika uwanja wa Kinshasa, DRC ambapo mashabiki wake pamoja na raia wote watatoa heshima zao za mwisho kwa mwanamuziki huyo. Papa ambaye amefariki makiwa na umri wa miaka 66, ametajwa kuwa mmoja watu waliokuwa na ushawishi mkubwa Afrika ya Mashariki na kwamba ni miongoni mwa waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne ijayo baada ya kuagwa Jumatatu. Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini Abidjan ambapo mwanamuziki huyo alianguka alipokuwa akiimba. Mwanahabari

Kangi Lugola Afurahia Sefue Kutumbuliwa…..Ataka Majipu Sugu Wizara ya Kilimo Yaliyoota Sehemu Nyeti Yatumbuliwe

Image
Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Lugola jana alichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa hisia kali huku akimpongeza Rais John Magufuli kwa kumtumbua Katibu Mkuu Kiongozi. Ingawa hakumtaja kwa jina, Balozi Ombeni Sefue ndiye Katibu Mkuu Kiongozi aliyeondolewa na Rais Magufuli Machi mwaka huu bila kubainisha sababu ikielezwa kwamba angepangiwa kazi nyingine. Lugola alisema Rais Magufuli ameonyesha kwa vitendo kuwa anamuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kauli yake kuwa Ikulu ni mahali patakatifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba. Lugola alisema kwa kuwa alikuwa akichangia kwa mara ya kwanza bajeti ya Serikali ya Awamu ya Tano, ni vyema akampongeza Rais kwa namna anavyotumbua majipu kwa ujasiri na bila kupepesa macho. Lugola akirejea kauli inayosema “kama unataka mali utaipata shambani”, alimtaka Waziri Nchemba kutumbua majipu katika wizara yake.

UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO SIRI YA MAFANIKIO BARA LA AFRIKA – NDUGAI

Image
  Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika. Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa wabunge wa Afrika. Spika wa Mhe. Job Ndugai akiwa na baadhi ya Maspika wenzie kutoka mabunge ya Nchi za Bara la Afrika kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament) alikoalikwa kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa B

DAVID DE GEA AWEKA REKODI USIKU WA TUZO MAN UNITED

Image
David De Gea ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Manchester United kwa mara ya tatu mfululizo baada ya Jumatatu usiku kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo. De Gea ametwaa tuzo hiyo maarufu kama Matt Busby player of the year ikiwa ni baada ya kutoruhusu kufungwa bao lolote katika michezo 14 kati ya 32 ya Ligi Kuu England aliyoicheza Manchester United msimu huu wa 2015/2016 huku pia akifanya vizuri katika michuano ya kombe la FA.Mbali ya De Gea nyota mwingine aliyewahi kutwaa tuzo hiyo kubwa zaidi mara tatu lakini katika vipindi tofauti ni Mreno Cristiano Ronaldo. Ronaldo alitwaa tuzo hiyo mwaka 2004, 2007 na 2008. Akiongea baada ya kutwaa tuzo hiyo De Gea amesema: “Ni ngumu kusema chochote, kutwaa tuzo hii mara tatu mfululizo ni faraja na heshima kubwa. Napenda kuwashukuru mashabiki wetu ambao ni bora zaidi duniani”. Wengine walioshinda tuzo Jumatatu usiku ni: Chris Smalling aliyetwaa tuzo ya mchezaji

NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015

Image
Kamati Maalum iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015 imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume. Akizungumza Katika kikao cha Tume mara baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva kwa niaba ya Wajumbe wa Tume amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa. Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume imeridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa ya kuandaa Rasimu hiyo ikiwa ni pamoja na muda mfupi uliotumika katika kukamilisha kazi hiyo. Aidha, ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa taarifa hiyo inakamilika na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mapema mwezi Julai mwaka huu. Pongezi hizo pia zimetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchagu

NAFASI ZA KAZI MWANANCHI MWISHO WA KUTUMA MAOMBI TAREHE 13 MAY 2016

Image
FREELANCER BUSINESS EXECUTIVE-TANGA POSITION DESCRIPTION: Mwananchi Communications Limited publishers of leading Tanzania newspapers, Mwananchi, Mwanaspoti and The Citizen are looking for motivated and highly experienced individuals to fill the positions of: – Freelancer Business Executives (16 POSTS) Dar es Salaam (8), Mtwara (1), Lindi (1), Dodoma (1), Singida (1), Zanzibar (1), Tanga (1), Kigoma(1) and Tabor(1). Job Purpose: To develop, maintain and increase a solidly dependable client base, to sell advertising space and provide an effective service to clients so as to maximise advertising sales volumes and revenue targets. . Main Responsibilities: • The successful candidates will be responsible for the following key result areas: • Thoroughly familiarizes oneself with comparative (own and competition) readership, circulation and rates and cost of advertising in all print and electronic media. • Identifies potential advertising clients, studies their bus