Posts

Maswali 6 utajiri wa Sh.bilioni 8 wa Diamond

Image
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz. Hashim Aziz na Musa Mateja, RISASI mchanganyiko Dar es Salaam: Hivi karibuni, Mtandao wa The Net Worth (www.the-net-worth.com) umetangaza utajiri wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ (26) ambapo kwa mujibu wa jarida hilo, nyota huyo ana utajiri wa dola milioni 4 za Kimarekani (sawa na zaidi ya shilingi bilioni 8.75), jambo lililozua maswali yapatayo 6 miongoni mwa Wabongo. Mtandao huo umekuwa ukijipambanua kwa kuanika utajiri wa watu maarufu barani Afrika wakiwemo David Adedeji Adeleke ‘Davido’ (shilingi bilioni 32), Ayodeji Balogun ‘Wizkid’ (bilioni 24) na wengineo kibao. Baadhi ya wasomaji wa gazeti hili wameuliza maswali hayo wakisema mwenye uwezo wa kuyajibu ni Diamond mwenyewe na si jarida hilo huku wakitia shaka kwamba, huenda waandaaji wa jarida hilio wamepewa taarifa za uongo na Diamond mwenyewe. AMEPATA WAPI UTAJIRI HUO WA HARAKA? Swali la kwanza ambalo wengi waliosikia taarif...

TCRA yawapa kibano akina lulu!

Image
Staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ Gladness Mallya na Ojuku Abraham, DAR ES SALAAM: Kufuatia tabia ya akina dada wengi kuweka picha za nusu utupu katika akaunti zao kwenye mitandao ya kijamii, wakiwemo mastaa kama Lulu, Masogange na wengineo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewapa kibano kikali, Risasi Mchanganyiko lina stori kamili. Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungi alisema ingawa jukumu la kuwakamata wote wanaoweka picha zinazokiuka maadili ni la jeshi la polisi kupitia kitengo cha makosa ya mtandao (Cyber Crime), taasisi hiyo inawasiliana na wamiliki wa mitandao ya kijamii ili kutafuta namna nzuri ya kuwadhibiti. Kidoa. “Tunachofanya ni kuzungumza na hawa watu ili kuwafungia wote wanaokiuka maadili, tunajua baadhi yao wanajiunga katika mitandao kwa kutumia majina ya uongo, lakini sisi tutazifungia ‘line’ maana kila moja ina namba zake za siri na hazifanani na zingin...

Fahamu mbinu 10 za vigogo kusafirisha unga

Image
Viatu vya kimasai  na zana nyingine zinazotumika kama urembo ambavyo vimetajwa kama zana muhimu zinazotumiwa katika usafirishwaji wa madawa hayo. Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Tanzania kwenye viwanja vya ndege vilivyopo nchini limekuwa likipambana na wauza madawa ya kulevya ‘unga’ kwa kugundua na kuzima mbinu zote wanazotumia kusafirisha biashara hiyo haramu, hivyo kupunguza kasi ya uingizwaji na utoaji wa unga kwa njia ya ndege, UWAZI limeambiwa. Akizungumza na gazeti hii katika mahojiano maalum yaliyofanyika wiki iliyopita Makao Makuu ya Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania yaliyopo jijini Dar, Kamanda wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno  (pichani) alizitaja mbinu kumi wanazotumia wauza unga hao kusafirishia bidhaa hiyo. “Kwanza napenda kuweka wazi kuwa, kwa sasa hatuna mchezo na wauza unga. Mbinu zao zote wanazotumia kusafirishia madawa yao tunazijua. Na napenda kuchukua nafasi hii kuwaambi...

CLOUDS FM YAIBOMOA RADIO YA MENGI EA RADIO KWA KUMCHUKUA DJ MAARUFU NA MTANGAZAJI WA RADIO HIYO

Image
Ile Vuta N’kuvute ya vituo vya redio inaendelea na sasa East Africa Radio imekuwa mhanga mpya. DJ Sinyorita na Mami Dj wa kike, Sinyorita na mtangazaji wa The Cruise, Mami wanadaiwa kuondoka East Africa Radio kuanzia wiki hii baada ya kupata dau kubwa kutoka kwa guess what? Clouds FM. Tetesi hizo zilianza kuvuma tangu wiki iliyopita lakini jana zimeonekana kupata ukweli baada ya wawili hao kutosikika kwenye kipindi cha The Cruise, kitu ambacho si cha kawaida. Tetesi zinadai kuwa tangu Dj Fetty aache kazi Clouds FM, wamekuwa wakitafuta mtangazaji wa kike anayeweza kuchukua nafasi yake na Mami anaonesha kuwa na caliber hiyo. Tayari wawili hao wamebadilisha profile zao za Instagram kwa kuondoa kipengele cha kuwa ni wafanyakazi wa East Africa Radio. Wawili hao wanatarajiwa kutambulishwa rasmi kwenye kituo chao kipya cha kazi soon.

Kigwangalla atembelea hospitali ya Haydom Mbulu-Manyara

Image
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Khamisi Andrea Kigwangalla akielezea machache juu ya ujio wake katika hospitali hiyo.  Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Kitengo cha Macho katika Hospitali hiyo ya Hydom. …Akipata maelezo juu ya kitengo maalum cha ufundi wa vifaa tiba. …Akipata picha ya pamoja na mtaalam wa masuala ya ufundi wa vifaa tiba vya kitaalam. …Akiangalia chumba cha CT-SCAN. Mashine ya kisasa ya CT-SCAN iliyopo katika hospitali hiyo ya Hydom.  …Akitembezwa katika moja ya wodi za hospitali hiyo. …Akiwasili katika Chuo cha Uuguzi cha Hydom kinachomilikiwa na Hospitali hiyo ya ya Hydom. …Akiwa katika Chuo cha Uuguzi. …Akisikiliza kwa risala fupi kutoka kwa msimamizi wa chuo hicho. …Akitoa maelezo kadhaa kwa uongozi wa Hospitaali hiyo baada ya kumaliza kuitembelea. Wanafunzi  wakifuatilia mkutano huo. Mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo akiuliza sw...

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 12.04.2016

Image