NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP) ANG’OLEWA KWA TUHUMA YA KUMILIKI NYUMBA 40
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu, amemwondoa kwenye nafasi yake, Mnunuzi wa Vifaa na Boharia Mkuu wa jeshi hilo, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Adriano Magayane ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake. Kuondolewa kwa DCP Magayane katika nafasi hiyo kunatokana na taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari hivi karibuni, kuwa anamiliki nyumba zaidi ya 40 na kumbi kadhaa za starehe ndani na nje ya Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Gazeti la Mtanzania, IGP Mangu amefikia uamuzi huo kwa kile kinachodaiwa kuwa tuhuma hizo ni nzito na zinalenga si kumfedhehesha yeye kama ofisa mkuu wa Jeshi la Polisi, lakini kwa jeshi zima. “IGP Mangu amemwondoa mara moja DCP Magayane kutokana na tuhuma zinazomkabili, kwa kweli ni nzito, nadhani hatua zilizochukuliwa ni sahihi… unajua sisi askari tuna miiko ya utendaji kazi, sasa inapotokea tuhuma kama hizi kwa ofisa kama huyu, lazima uchunguzi wa ki