Posts
TRL KUSAFIRISHA SARUJI YA TANGA KWA NJIA YA RELI
- Get link
- Other Apps
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela akitoa taarifa ya hali ya miundombinu katika mkoa wa Tanga kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ofisini kwake. Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa pili kulia) akimwonesha moja ya nyaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (wa pili kushoto) kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tang
WAZIRI LUKUVU AWATIA KITANZI NHC
- Get link
- Other Apps
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameiagiza bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa Nyumba (NHC) kuacha kuanzisha miradi mipya ya ujenzi hadi kukamilishwa kwa miradi iliyokwishaanza. Akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo Dar es Salaam jana, Lukuvi alisema hakuna haja ya kuanzisha miradi mipya wakati iliyopo haijakamilika. “Nadhani miradi iliyopo mnaijua na tarehe za kukamilika ujenzi wake wote tunafahamu, hivyo nitoe agizo kuanzia leo hakuna kuanza kwa mradi mpya wowote mpaka imalizwe iliyokwishaanza,” alisema. Lukuvi pia aliiagiza bodi hiyo kutopandisha kodi za nyumba zake bila ridhaa yake huku akisisitiza gharama zipangwe kwa kuzingatia uwezo wa wananchi. “Hamuwezi kusema nyumba ya gharama nafuu wakati ina vyumba viwili na inauzwa kwa Sh52 milioni, hainiingii akilini na wala Mtanzania wa kawaida hawezi kuona unafuu wowote hapo,” alisema Lukuvi.
RC KIJUU: WATUMISHI HEWA ANZENI KUJIONDOA KABLA SIJAWAKAMUA MAJIPU
- Get link
- Other Apps
Mkuu mpya wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amewaagiza watumishi wasio na sifa za kuajiriwa kujiondoa kabla ya March 31 mwaka huu. Kijuu alitoa kauli hiyo jana wakati wa Makabidhiano ya ofisi baina yake na mkuu wa mkoa wa zamani,John Mongella ambapo alisema kwamba Tanzania inawatumishi hewa zaidi ya 2000, hivyo ana imani hata Kagera wapo. "Hao watumishi hewa endapo watang'ang'ania kubaki katika vitengo walivyopo nitawashughulikia wahusika wakuu wa vitengo hivyo," alisema Aidha, aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa mabaraza ya usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi mkoa ili kusimamia haki za wananchi. Pia aliwataka watumishi wa serikali mkoani humo kufahamu maudhui ya "Hapa Kazi Tu", kwa kufanya kazi kwa kasi,haraka, nguvu, maarifa na uadilifu. Aliwataka kutosubiri kusukumwa, lakini wajitambue wao ni akina nan
MAKABIDHIANO YA UONGOZI WA MKOA WA DODOMA
- Get link
- Other Apps
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akitoa salamu zake wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe Mhe. Chiku Gallawa (hayupo pichani) Machi 22,2016. Mkuu wa Mkoa mpya wa Songwe ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa salamu zake wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa wa Dodoma baina yake na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (hayupo pichani) Machi 22,2016. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Dini Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhiana uongozi wa Mkoa huo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Chiku Gallawa (wa tatu kushoto) Machi 22,2016 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (wa kwanza kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhiana uongo
Samatta hajakubali kuona rekodi ya Tanzania ikivunjwa na Chad mikononi mwake
- Get link
- Other Apps
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 imeshuka katika dimba la Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017. Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta akiichezea Taifa Stars kama nahodha wa timu hiyo, katika mchezo huo uliochezwa Chad , Taifa Stars imeibuka na ushindi wa goli 1-0, goli la Taifa Stars lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30, baada ya kutumia vyema krosi ya Farid Musa . Samatta amefanikiwa kuitunzia Tanzania rekodi dhidi ya Chad , kwani mara ya mwisho Taifa Stars alikutana na Chad , ugenini na kufanikiwa kuibuka kwa ushindi wa goli 2-1. Magoli ya Taifa Stars wakati huo yalifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 11 na Nurdin Bakari dakika ya 88, huku goli la Chad la kufutia machozi lilifungwa na Mahamat Labbo dakika ya 12. Taifa Stars itarudiana na Chad Jumatatu ya March 28 uwa
BREAKING NEEWWSS:RAIS MAGUFULI ATUMBUA JIPU TANESCO
- Get link
- Other Apps
Rais Dk. John Pombe Magufuli. Rais wa awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli anayesifika kwa utumbuaji wa majipu, safari hii ameifanya kazi hiyo kimyakimya, baada ya kuivunja Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) iliyokuwa ikiongozwa na Dk. Mighanda Manyahi, Risasi Mchanganyiko linathibitisha. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, bodi hiyo iliyokuwa na wajumbe wanane, ilivunjwa Machi 3, mwaka huu katika barua zilizosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mhandishi Mussa Ibrahim Iyombe na kusababisha kuongezeka kwa idadi ya bodi za mashirika mbalimbali ya serikali zilizovunjwa. Bodi hiyo ya wakurugenzi iliyovunjwa, licha ya mwenyekiti wake Dk. Manyahi ilikuwa na wajumbe ambao ni Dk. Haji Semboja (Makamu Mwenyekiti), Kissa Kilindu, Juma Mkobya, Shaaban Kayungilo, Dk. Mutesigwa Maingu, Boniface Muhegi, Felix Kibodya na Nyamajeje Weggoro. Mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, alisema ni kw
Basi la Super Sami Lapata Ajali Tabora
- Get link
- Other Apps
Aajali ilivyotokea. Ng’ombe wakiwa wamkufa baada ya kugongwa na basi hilo. Basi lapinduka na kujeruhi watu Igunga WATU kadhaa wajeruhiwa baada ya basi la Super Sami lenye namba za usajili T 819 DEN kutoka Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam kupinduka katika Kijiji cha Igogo, wilayani Igunga mkoani Tabora leo wakati likijaribu kukwepa ng’ombe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa taarifa za awali zinaonyesha dereva wa basi alikuwa anaongea na simu.
How do you block someone on Facebook?
- Get link
- Other Apps
Quick Answer To block someone on Facebook, sign into Facebook, click the lock icon at the top of the page, and then select "How Do I Stop Someone From Bothering Me?" Enter the name of the person you wish to block, click Block, and then confirm the block request. Full Answer Sign on Sign into your Facebook account. Click the lock icon Click the icon that resembles a lock in the upper-right section of any Facebook page. This icon opens the Privacy Shortcuts dropdown menu. Locate the user Select "How Do I Stop Someone From Bothering Me?" In the dropdown menu, enter the name or email address of the person you wish to block, and then click Block. This action opens the Block People dialog box with a list of people you can block. Block the user Click the name of the user you wish to block in the "Are You Sure You Want To Block" dialog box. Click Block to confirm. If the person you want to block is not on the list, go
PICHA ZA AY NA PREZOO ZILIVUNJA NDOA YA DAYNA NYANGE
- Get link
- Other Apps
Msanii wa muziki, Dayna Nyange amedai kilichosababisha wakaachana na mzazi mwenzake ni wivu wa mapenzi uliotokana na picha aliyopiga na wasanii wawili wa Kenya, Wahu na Prezzo pamoja na Mtanzania, Ambwene Yessaya ‘AY’. Muimbaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Rahma, ameliambia gazeti la Mtanzania, kuwa picha hizo alizipiga na wasanii hao kabla hajawa maarufu wala kujihusisha na muziki kwa kiasi kikubwa hivyo hiyo ilikuwa sehemu ya kutafuta marafiki wa kumsaidia kimuziki. “Kutokana na picha hiyo mchumba wangu huyo alihisi kwamba mmoja wa wasanii hao labda natoka naye kimapenzi hivyo akawa hataki nipige picha na wasanii na nisijihusishe tena na masuala ya kimuziki,” alisema Dayna. Aliongeza, “Muziki ni kitu ninachokipenda sana katika maisha yangu hapo nikaona wivu umezidi kwa mwezangu ambaye tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kike mwenye miaka 10, tukaamua kuachana nami nikaendelea na muziki wangu hadi leo bila mchumba, mpenzi wala nini na maisha yana
TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA DODOMA
- Get link
- Other Apps
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma kuanzia Jumatatu, tarehe 28 March 2016 kwenye ukumbi wa LAPF House Mkoani Dodoma. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Dodoma na mikoa ya jirani. Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanafikia malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Dodoma waliotuma maombi na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 26 Machi 2016 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa LAPF House Mkoani Dodoma. Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya
MWANASAYANSI ALIETENGENEZA VIRUS HATARI VYA UKIMWI
- Get link
- Other Apps
Ameua maelfu na maelfu ya watu, alitengeneza ugonjwa huu mnamo miaka ya 1970, na sasa daktari huyu kwa jina Robert Gallo ametoka adharani na kusema amepata dawa ya kutibu ugonjwa huo. Robert Gallo anaelezwa kwamba alihusika na vita vya kibaiolojia kwa lengo la kuwaondosha watu weusi na mashoga duniani katika miaka ya 1970