SERIKALI YAMKABIDHI CHEKA CHETI CHA PONGEZI KUTOKANA NA USHINDI WAKE.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akiwa ameambatana na Bondia Francis Cheka (wapili kulia) alipotembelea Wizarani leo jijini Dar es Salaam na Serikali imemkabidhi Cheti cha pongezi. Kushoto ni Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh). Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la kumkabidhi Cheti cha pongezi kutokana na ushindi Bondia Francis Cheka (kushoto) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge. Bondia Francis Cheka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa zoezi la kupokea Cheti cha pongezi kutoka kwa Serikali leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh) na Meneja wa Bondia huyo Chifu Ndambi