Posts

Dr Slaa Afunga Ndoa na Josephine Mushumbusi Ughaibuni

Image
Hatimaye aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Josephine Mushumbusi. Wawili hao walifunga ndoa nchini Canada jana katika kanisa  moja, lakini  habari zinaeleza si kanisa Katoliki ambalo Dr Slaa aliwahi kuwa Padri kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.  Ndoa hiyo imetimiza ndoto za muda mrefu  za Dr Slaa ambaye mwaka 2010 aliyekuwa mume wa Mushumbusi alikimbilia mahakamani  akidai bado anamtambua Josephine  kuwa ni mke wake wake halali. Mume huyo alidai Dr Slaa alimpora mke wake, hivyo akaitaka mahakama  impatie haki  yake. Hata hivyo kesi hiyo haikupewa mashiko makubwa. Misukosuko ya wawili hao iliendelea ambapo mwaka 2012 aliyekuwa  mke wake, Rose Kamili alifungua kesi kupinga ndoa hiyo huku akitaka alipwe milioni 50. Dr Slaa na Mushumbusi wanaishi kwa takribani miaka sita sasa na waliwahi kuanza maandalizi ya kufunga ndoa wakiwa hapa nchini ...

Hirizi ya Jambazi Yazua Balaa

Image
Hirizi ya jambazi huyo ikiwa shingoni. WAANDISHI WETU, AMANI Uvamizi wa majambazi kwenye Benki ya Access, Tawi la Mbagala Rangi Tatu wilayani Temeke jijini Dar, Ijumaa iliyopita umeibua mapya baada ya jambazi mmoja kukutwa na hirizi shingoni, Amani lina mlolongo wa mambo yote. Kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, Mkoa wa Temeke, jambazi huyo aliyekutwa na hirizi ni yule aliyesimama na bunduki mbili barabarani akifyatua risasi juu ili kuzuia magari yanayotoka Posta na Kariakoo yasipite eneo hilo. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Kamishna Simon Siro. SIKIA SIMULIZI HII “Hii kazi ngumu sana! Yule jambazi aliyeshika bunduki mbili na kusimama barabarani, tulipompiga risasi tulimkuta ana hirizi shingoni! Lakini mbaya zaidi ni kwamba, ile hirizi ilikuwa kama inahema. “Lakini cha ajabu sasa, baada ya kuonekana imetulia, yule jambazi naye akatulia, akawa ameshakata roho. Huu ujambazi wa kupewa ujasiri na hirizi naona unashika kasi. Maja...

RUBY AFUNGUKA MAZITO KUHUSU BIFU KUBWA KATI YAKE NA ALIKIBA

Image
Mwezi kama mmoja uliopita, Ruby alijikuta akishambuliwa vikali na mashabiki wa Alikiba baada ya kudai kuwa muimbaji huyo wa ‘Lupela’ alimfananisha na mbwa wakati akihojiwa kwenye kipindi cha The Sporah Show. Tumekaa na Ruby kuzungumza kuhusu suala hilo na amedai kuwa yaliisha. “Ni kwamba bro [Alikiba] hakunikosea chochote, hakuniita mimi mbwa kama inavyosemekana kwa watu kwamba ‘mbwa mbwa’ watu ndiyo wanajaribu kutengeneza beef lakini yule jamaa mimi sina chuki naye na hakuniita hivyo,” amesema Ruby. “Watu wake wa karibu ndiyo watu wanaomfahamu kwahiyo the way walivyoidefine nje huko ilifanya kuleta maana nyingine, iliniletea mimi maana nyingine kwamba bro ulimaanisha hivi nilivyoelewa au ni vile! Kwahiyo mimi nilifanya kama kuuliza lakini sio kumlaumu kwanini, hapana ila ni watu jinsi walivyoupokea,” ameongeza. “Walitakiwa kusoma kile nilichokiandika ila kwa sababu wamekurupuka siwezi kuwalaumu.” Ruby amesema hana mazoea na Alikiba kwakuwa hawakutani l...

Ray C, Hali Tete

Image
  Rehema Chalamila ‘Ray C’ baada ya hali kuwa tete (picha na maktaba). MUSA MATEJA, AMANI DAR ES SALAAM: Hali ya mrembo aliyekuwa akifanya vyema kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kabla ya kutopea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’, Rehema Chalamila ‘Ray C’, si shwari kwani sasa amerudishwa kwao, Bunju jijini Dar hivyo kuzua wasiwasi wa jinsi atakavyoweza kutumia dawa, tembea na Amani. Chanzo cha uhakika kilichopo ndani ya idara ya tiba katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar, kimesema mrembo huyo hali yake ya kiafya inatishia amani baada ya siku chache zilizopita kukaidi utumiaji wa dawa za kuondoa sumu akiwa hospitalini hapo hivyo kurudishwa kwao. “Ndugu yangu nimeamua kukuita ili kukusimulia kwa kirefu hali ya huyu mrembo ilivyokuwa baada ya kurudia tena matumizi ya dawa za kulevya na maendeleo yake. “Kwanza Ray C ameanza kuongea maneno yasiyoeleweka na mengine unajua kabisa hana uhakika nayo ingawa anasema kama ana uhakika,” kilise...

Rais Magufuli Aapa Kuwatumbua MAJIPU Viongozi wa Sekretarieti ya EAC.......Asema Pesa Walizotumia Kuandaa Mkutano ni Nyingi Sana

Image
WAKUU wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameazimia Rais John Magufuli awe Mwenyekiti wa jumuiya, kwa maana kwamba Tanzania iendelee mwaka mwingine kuongoza kipindi ambacho Burundi ndiyo ilipaswa kushika wadhifa. Dk Magufuli ambaye anaongoza jumuiya hiyo ambayo imepata mwanachama mwingine, Sudan Kusini, ameanza kwa kasi kubwa huku akipenyeza msimamo na falsafa yake ya ‘kutumbua majipu’ kuhakikisha nchi wanachama wanakwenda pamoja na kuleta maendeleo ya wananchi. Hayo yalifanyika katika mkutano wa kawaida wa 17 wa Jumuiya, ambapo wakuu hao wa nchi pia walikubaliana kwa pamoja Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kushirikiana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kutatua mgogoro wa Burundi. Magufuli aliahidi atafuatilia Sekretarieti ya EAC, kuhakikisha inafanya kazi kwa maslahi ya wananchi wa nchi wanachama na si kuwanyonya. Rais Magufuli alihimiza viongozi wakuu wa umoja huo, kutoa kipaumbele katika ujenzi wa viwanda. Alisisitiza msimamo wake kupitia Sekretarieti ya jum...

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 03.03.2016

Image

VIONGOZI WACHACHE WAJITOKEZA MSIBA WA KAKA YAKE RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) mara alipowasili nyumbani kwa maraehemu mzee Selemani Mrisho Kikwete kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya marehemu pamoja na ndugu wa marehemu akiwemo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha mzee Selemani Mrisho Kikwete kilichotokea nchini India.  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mzee Mohamed Seif Khatib (kulia) mara alipowasili nyumbani kwa maraehemu mzee Selemani Mrisho Kikwete kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya marehemu pamoja na ndugu wa marehemu akiwemo Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha mzee Selemani Mrisho Kikwete kilichotokea nchini India.  ...

RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN ASHIRIKI MKUTANO WA 17 WA EAC ARUSHA

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Museven baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC,(kulia) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kuwasili katika Hoteli ya Ngurdoto Mkoani Arusha palipofanyika mkutano wa 17 wa Nchi za Afrika ya Mashariki EAC. Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki wakisimama wakati wimbo wa umoja wa nchi hizo ukipigwa katika mkutano wa 17 wa EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngurdoto mkoani Arusha. Miongoni mwa Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania walioalikwa katika mkutano wa 17 wa Viongozi wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki EAC uliofanyika leo ukumbi wa Ngu...

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS KENYATTA NA RAIS KAGAME

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi. Baadhi ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.Rais Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi y...