Posts

MABADILIKO KWA BAADHI YA MAKAMANDA WA MIKOA.

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda  wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini. Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa  kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.  Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia dawa za kulevya. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani Mungi anaenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake inachukuliwa na   Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe. Aliyekuwa Afisa mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa ...

MMILIKI WA MABASI YA NGORIKA AFARIKI DUNIA..AGONGWA NA GARI

Image
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Ngorika Bus service, yenye makao yake makuu Kisangara mkoani Kilimanjaro, bw. STEPHEN Mberesero amefariki dunia mjini hapa baada ya kugongwa na gari aina ya Land cruiser wakati akizungumza na simu. Kamanda wa polisi wa MKOA wa Tanga Mihayo msikhera alisema Jana kuwa ajali iyo ilitokea juzi SAA 2;30 usiku katika Barbara kuu ya segera-njiapanda ya himo mjini Korogwe. Alisema Mberesero ambae mabasi yake hufanya safari Kati ya mikoa ya Arusha,tanga,Daresalaam na singida,marehemu alikuwa amesimama pembeni ya kituo cha mafuta cha Lake oil na kugongwa na gari hilo. Mfanyakazi wa kampuni hiyo ,Adam Miraji alisema bosi wake huyo alikwenda Korogwe kuangalia Kiwanja kwajili ya kununua kujenga kituo cha mafuta. Kama unavyojua bosi wetu pamoja na kufanya biashara ya Mabasi,alikuwa anamiliki vituo mbalimbali vya mafuta mkoani Kilimanjaro,Dar es Salaam na Arusha,hivyo alipokuja Tanga alituambia anakwenda Korogwe kuangalia Kiwanj...

BREAKING NEWSS Vurugu Kubwa Zaibuka Wakati wa Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam

Image
VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya uchaguzi huo kuhairishwa  tena kwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda  UKAWA. Tukio hilo la aina yake limetokea leo katika ukumbi wa Karimjee  jijini Dar es salaam mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutangaza kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi  kuwekewa pingamizi na CCM mahakamani. Jambo hilo liliwachukiza   madiwani wa UKAWA ambao walidai kuwa hawajapata barua ya pingamizi hilo, hivyo wakataka waruhusiwe kufanya uchaguzi peke yao kwa kuwa akidi ya madiwani kufanya uchaguzi ilikuwa imetimia. Wakati UKAWA  wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo  wenyewe ,Polisi zaidi ya 15 walivamia ukumbi huo na kuwataka madiwan hao waondoke ukumbini,jambo lilowachukiza tena na kuibua patashika ndani ya ukumbi. ==...

Sinema ujambazi wa kivita jijini Dar

Image
UJAMBAZI wa kutumia vifaa vya kivita umeibuka jijini Dar es Salaam, ukiwemo uliofanyika katika uporaji wa Benki ya Access juzi, ambako majambazi walitumia bunduki za kivita aina ya SMG na mabomu ya kurusha kwa mkono. Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema mbali na uvamizi huo, pia Polisi imebaini na kukamata askari bandia, waliokuwa na sare rasmi za Jeshi la Polisi zenye vyeo na redio call, zenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya askari Polisi. Akizungumzia matukio hayo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema atakutana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, ili Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi, waanzishe msako wa pamoja dhidi ya wahalifu hao. Uvamizi, mauaji Mbagala Akisimulia ujambazi uliofanyika katika Benki ya Access Tawi la Mbagala, Kamanda Sirro alisema majambazi hao walikuwa 12, wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki sita na walifik...

Walimu Dar kusafiri bure – DC Makonda

Image
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Mwenyekiti wa Darcoboa, Sabri Mabrouk akifafanua jambo. Mwenyekiti wa Uwadar, William Masanja akizungumza na waandishi wa habari. Mwenyekiti wa Chama cha Madereva nchini (Tadu), Shaban Mdemu akichangia hoja mbalimbali. Wanahabari wakifuatilia mkutano huo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mapema leo hii ametangaza kuwa walimu wa shule za serikali zilizopo jijini Dar watasafiri bila kulipa nauli kwenye daladala. Akizungumza na waandishi katika Hoteli ya Ramada iliyopo Posta jijini Dar, Paul Makonda alisema kuwa ili kuendana na kasi ya rais hasa kwenye kuboresha sekta ya elimu nchini, alipata wazo la kuhakikisha wilaya yake inapambana ipasavyo na changamoto zinazowakabili walimu hasa suala la usafiri linalorudisha nyuma ufanisi wa walimu. Makonda alisema kuwa suala hilo litazigusa pia Wilaya za Temeke na Ilala ambapo mwalimu atapatiwa kitambulisho maalumu cheny...

Picha 15: Cheka alivyomkalisha Mserbia

Image
Bondia Francis Cheka ‘SMG’ jana usiku alifanikiwa kuiandikia Tanzania historia nyingine mpya baada ya kumchapa Muingereza, Geard Ajetovic katika pambano la kugombania Ubingwa wa mabara (WBF Intercontinetal). Katika pambano hilo la raundi 12 lililopigwa kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Cheka alioneka kucheza kwa uwoga mkubwa kitendo kilichopelekea kuangushwa nchini kwenye raundi ya kwanza tu kufuatia makonde makali kutoka kwa Ajetivic ambaye alikuwa amepania kumaliza pambano mapema kabisa. Mashabiki wengi waliokuwa kwenye Viwanja vya Leaders walionekana kuwa na hofu kutokana na Ajetovic kuachia ngumi kali za kushitukiza ingawa Cheka alipiga nyingi zaidi za kudokoa zilizomsaidia kupata pointi nyingi. Lakini kadiri mchezo unavyosonga mbele, kidogo akaanza kuonyesha cheche na kubadilika ingawa mpinzani wake aliendelea kupiga ngumi kali huku raundi ya tisa, Cheka akichanika na kuanza kuvuja damu, lakini bado alionekana kuwa mvumilivu na kuendelea k...

OMBAOMBA TISHIO ANAYEOMBA KWA KUTUMIA KISU IRINGA .

Image
Askari polisi  mjini Iringa akiwa ameshika kisu baada ya kufanikiwa  kumnasa kijana Mohamed Iddy (18) mkazi  wa mjini Iringa kutokana na kutishia maisha ya  wakazi wa mji  wa Iringa akiwa katika  shughuli yake ya kuomba hudaiwa  kuhatarisha maisha ya  wananchi kwa  kuwafukuza kwa kisu pindi anaponyimwa pesa , Kijana  huyo  omba  omba tishio akipelekwa  kituo cha polisi pamoja na kisu anachotumia kutishia  wananchi  wakati  akiomba  pesa  Askari  polisi  wakiwa  wamembana   lilivyo  kijana   huyo omba omba  Hapa  akiwa  eneo la  Miyomboni akipelekwa  kituoni  OMBA  omba  hatari anayeomba kwa nguvu kwa kutumia kisu kwa wananchi  wanaomnyima msaada  wa  pesa amekamatwa na jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa  kufuatia msako mkali  dhidi  yake. T...

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI ARUSHA KUONGOZA MKUTANO WA 17 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Image
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Msshariki Mhe Joshua Nassari aliyekuwa mmoja wa viongozi  na wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utofanyika jijini Arusha. Picha na IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa Balozi Agustine Mahiga mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi mbali...