Posts

BREAKING NEWSS Vurugu Kubwa Zaibuka Wakati wa Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam

Image
VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya uchaguzi huo kuhairishwa  tena kwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda  UKAWA. Tukio hilo la aina yake limetokea leo katika ukumbi wa Karimjee  jijini Dar es salaam mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutangaza kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi  kuwekewa pingamizi na CCM mahakamani. Jambo hilo liliwachukiza   madiwani wa UKAWA ambao walidai kuwa hawajapata barua ya pingamizi hilo, hivyo wakataka waruhusiwe kufanya uchaguzi peke yao kwa kuwa akidi ya madiwani kufanya uchaguzi ilikuwa imetimia. Wakati UKAWA  wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo  wenyewe ,Polisi zaidi ya 15 walivamia ukumbi huo na kuwataka madiwan hao waondoke ukumbini,jambo lilowachukiza tena na kuibua patashika ndani ya ukumbi. ==

Sinema ujambazi wa kivita jijini Dar

Image
UJAMBAZI wa kutumia vifaa vya kivita umeibuka jijini Dar es Salaam, ukiwemo uliofanyika katika uporaji wa Benki ya Access juzi, ambako majambazi walitumia bunduki za kivita aina ya SMG na mabomu ya kurusha kwa mkono. Akizungumza jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema mbali na uvamizi huo, pia Polisi imebaini na kukamata askari bandia, waliokuwa na sare rasmi za Jeshi la Polisi zenye vyeo na redio call, zenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya askari Polisi. Akizungumzia matukio hayo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga alisema atakutana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, ili Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi, waanzishe msako wa pamoja dhidi ya wahalifu hao. Uvamizi, mauaji Mbagala Akisimulia ujambazi uliofanyika katika Benki ya Access Tawi la Mbagala, Kamanda Sirro alisema majambazi hao walikuwa 12, wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki sita na walifik

Walimu Dar kusafiri bure – DC Makonda

Image
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Mwenyekiti wa Darcoboa, Sabri Mabrouk akifafanua jambo. Mwenyekiti wa Uwadar, William Masanja akizungumza na waandishi wa habari. Mwenyekiti wa Chama cha Madereva nchini (Tadu), Shaban Mdemu akichangia hoja mbalimbali. Wanahabari wakifuatilia mkutano huo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mapema leo hii ametangaza kuwa walimu wa shule za serikali zilizopo jijini Dar watasafiri bila kulipa nauli kwenye daladala. Akizungumza na waandishi katika Hoteli ya Ramada iliyopo Posta jijini Dar, Paul Makonda alisema kuwa ili kuendana na kasi ya rais hasa kwenye kuboresha sekta ya elimu nchini, alipata wazo la kuhakikisha wilaya yake inapambana ipasavyo na changamoto zinazowakabili walimu hasa suala la usafiri linalorudisha nyuma ufanisi wa walimu. Makonda alisema kuwa suala hilo litazigusa pia Wilaya za Temeke na Ilala ambapo mwalimu atapatiwa kitambulisho maalumu cheny

Picha 15: Cheka alivyomkalisha Mserbia

Image
Bondia Francis Cheka ‘SMG’ jana usiku alifanikiwa kuiandikia Tanzania historia nyingine mpya baada ya kumchapa Muingereza, Geard Ajetovic katika pambano la kugombania Ubingwa wa mabara (WBF Intercontinetal). Katika pambano hilo la raundi 12 lililopigwa kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Cheka alioneka kucheza kwa uwoga mkubwa kitendo kilichopelekea kuangushwa nchini kwenye raundi ya kwanza tu kufuatia makonde makali kutoka kwa Ajetivic ambaye alikuwa amepania kumaliza pambano mapema kabisa. Mashabiki wengi waliokuwa kwenye Viwanja vya Leaders walionekana kuwa na hofu kutokana na Ajetovic kuachia ngumi kali za kushitukiza ingawa Cheka alipiga nyingi zaidi za kudokoa zilizomsaidia kupata pointi nyingi. Lakini kadiri mchezo unavyosonga mbele, kidogo akaanza kuonyesha cheche na kubadilika ingawa mpinzani wake aliendelea kupiga ngumi kali huku raundi ya tisa, Cheka akichanika na kuanza kuvuja damu, lakini bado alionekana kuwa mvumilivu na kuendelea k

OMBAOMBA TISHIO ANAYEOMBA KWA KUTUMIA KISU IRINGA .

Image
Askari polisi  mjini Iringa akiwa ameshika kisu baada ya kufanikiwa  kumnasa kijana Mohamed Iddy (18) mkazi  wa mjini Iringa kutokana na kutishia maisha ya  wakazi wa mji  wa Iringa akiwa katika  shughuli yake ya kuomba hudaiwa  kuhatarisha maisha ya  wananchi kwa  kuwafukuza kwa kisu pindi anaponyimwa pesa , Kijana  huyo  omba  omba tishio akipelekwa  kituo cha polisi pamoja na kisu anachotumia kutishia  wananchi  wakati  akiomba  pesa  Askari  polisi  wakiwa  wamembana   lilivyo  kijana   huyo omba omba  Hapa  akiwa  eneo la  Miyomboni akipelekwa  kituoni  OMBA  omba  hatari anayeomba kwa nguvu kwa kutumia kisu kwa wananchi  wanaomnyima msaada  wa  pesa amekamatwa na jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa  kufuatia msako mkali  dhidi  yake. Tukio  la kukamatwa kwa  kijana   huyo lilitokea leo majira ya saa 5 asubuhi katika  eneo la Posta  mjini Iringa baada ya  kuwepo kwa malalamiko mengi  kutoka kwa  wananchi wa mji wa Iringa  hasa  wanawake a

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI ARUSHA KUONGOZA MKUTANO WA 17 WA KAWAIDA WA WAKUU WA NCHI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Image
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Msshariki Mhe Joshua Nassari aliyekuwa mmoja wa viongozi  na wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) tayari kuongoza Mkutano wa 17 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utofanyika jijini Arusha. Picha na IKULU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa Balozi Agustine Mahiga mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi mbalimbal

WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI BANDARI YA MTWARA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua bandari ya Mtwara na kunusa harufu ya ufisadi katika utoaji wa zabuni  ya ujenzi wa gati mpya tatu. Wazi Mkuu ambaye alikagua eneo la ujenzi wa gati hizo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), alisema anazo taarifa juu ya utolewaji wa zabuni hiyo na mzabuni ameshashinda lakini kuna madai kwamba watu wa manunuzi kupitia PPRA  ndiyo wanakwamisha zabuni hiyo. Aliwaomba wabunge wa mkoa wa Mtwara washirikiane kusimamia suala hilo ili ujenzi wake uweze kuanza mara moja na kuleta ajira kwa wana Mtwara. “Ujenzi ukikamilika siyo tu ajira zitaongezeka bali hata meli nyingi zitaleta mizigo katika bandari hii na mapato ya mkoa yataongezeka”, alisema. “Natambua kwamba kuna mpango wa kujenga gati nne ambapo moja kati ya hizo itajengwa na TPA (Mamlaka ya Bandari) lakini hizi tatu zilitangazwa na kupata mzabuni ambaye ni kampuni ya Hyundai kutoka Japan. Lakini hii kampuni imekuwa ikizungushwa bila sababu. Tutafuatilia kubaini tatizo liko wapi,

Taswira ya Msiba wa Mapili

Image
Waombolezaji wakiwa msibani. Mtangazaji na Mdau wa Muziki wa Dansi, Rajab Zomboko akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani). Msanii wa muziki, Mrisho Mpoto akitoa ratiba ya maziko. Muimbaji wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akiwa na waombolezaji wengine. Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan akiwa msibani hapo. Mtangazaji wa Global TV Online, akimhoji Mkongwe King Kiki kuhusu marehemu. Mamia ya waombolezaji wamejitokeza mapema leo kumsindikiza Mkongwe wa Muziki wa Dansi na Mlezi wa Bendi ya Mjomba, Kassim Mapili baada ya kufariki ghafla akiwa nyumbani kwa mwanaye, Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam. Picha/ Chande Abdallah

AIBU M MPYA YA BOSI LADY.

Image
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Stori: Mwandishi, Wetu, Ijumaa D ar es Salaam: Aibu yake! Kitendo cha mwandani wa Mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutupia mtandaoni picha ya nusu utupu akiwa amelala na jamaa huyo, kimetafsiriwa kuwa ni kulipa kisasi kwani miezi kadhaa iliyopita naye alimtundika akiwa anaoga bafuni. Mpenzi wa mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Picha hiyo ya mapema wiki hii, inadaiwa Zari aliitupia kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram kisha kuitoa muda mfupi bila kujua imeshachukuliwa na wapenda ubuyu na kurushwa kwenye meza ya Ijumaa.   Zari The Boss Lady akiwa na Diamond Platinumz. DIAMOND FOFOFO Katika picha hiyo, Zari anaonekana ndiye aliyeipiga ikiwaonesha wakiwa wamelala kitandani huku Diamond akiwa fofofo bila kujua kilichoendelea. Picha hiyo iliibua gumzo