Posts

WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI BANDARI YA MTWARA

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua bandari ya Mtwara na kunusa harufu ya ufisadi katika utoaji wa zabuni  ya ujenzi wa gati mpya tatu. Wazi Mkuu ambaye alikagua eneo la ujenzi wa gati hizo jana (Jumamosi, Februari 27, 2016), alisema anazo taarifa juu ya utolewaji wa zabuni hiyo na mzabuni ameshashinda lakini kuna madai kwamba watu wa manunuzi kupitia PPRA  ndiyo wanakwamisha zabuni hiyo. Aliwaomba wabunge wa mkoa wa Mtwara washirikiane kusimamia suala hilo ili ujenzi wake uweze kuanza mara moja na kuleta ajira kwa wana Mtwara. “Ujenzi ukikamilika siyo tu ajira zitaongezeka bali hata meli nyingi zitaleta mizigo katika bandari hii na mapato ya mkoa yataongezeka”, alisema. “Natambua kwamba kuna mpango wa kujenga gati nne ambapo moja kati ya hizo itajengwa na TPA (Mamlaka ya Bandari) lakini hizi tatu zilitangazwa na kupata mzabuni ambaye ni kampuni ya Hyundai kutoka Japan. Lakini hii kampuni imekuwa ikizungushwa bila sababu. Tutafuatilia kubaini tatizo liko wapi,

Taswira ya Msiba wa Mapili

Image
Waombolezaji wakiwa msibani. Mtangazaji na Mdau wa Muziki wa Dansi, Rajab Zomboko akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani). Msanii wa muziki, Mrisho Mpoto akitoa ratiba ya maziko. Muimbaji wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akiwa na waombolezaji wengine. Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan akiwa msibani hapo. Mtangazaji wa Global TV Online, akimhoji Mkongwe King Kiki kuhusu marehemu. Mamia ya waombolezaji wamejitokeza mapema leo kumsindikiza Mkongwe wa Muziki wa Dansi na Mlezi wa Bendi ya Mjomba, Kassim Mapili baada ya kufariki ghafla akiwa nyumbani kwa mwanaye, Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam. Picha/ Chande Abdallah

AIBU M MPYA YA BOSI LADY.

Image
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Stori: Mwandishi, Wetu, Ijumaa D ar es Salaam: Aibu yake! Kitendo cha mwandani wa Mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutupia mtandaoni picha ya nusu utupu akiwa amelala na jamaa huyo, kimetafsiriwa kuwa ni kulipa kisasi kwani miezi kadhaa iliyopita naye alimtundika akiwa anaoga bafuni. Mpenzi wa mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Picha hiyo ya mapema wiki hii, inadaiwa Zari aliitupia kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram kisha kuitoa muda mfupi bila kujua imeshachukuliwa na wapenda ubuyu na kurushwa kwenye meza ya Ijumaa.   Zari The Boss Lady akiwa na Diamond Platinumz. DIAMOND FOFOFO Katika picha hiyo, Zari anaonekana ndiye aliyeipiga ikiwaonesha wakiwa wamelala kitandani huku Diamond akiwa fofofo bila kujua kilichoendelea. Picha hiyo iliibua gumzo

WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA NIDA, AWATAKA KUONGEZA KASI UANDAAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza upande wa kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika

Kajala sasa ajis’tukia kuzeeka

Image
Na Imelda Mtema Staa wa Filamu Bongo, Kajala Masanja amesema kuwa mambo ya kimjini kama wafanyavyo mastaa wengine kwa sasa ameyapa mgongo kwa madai kuwa anaona anaelekea kuzeeka. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Kajala alisema kila anapojiangalia anaona kabisa alivyokuwa zamani sivyo alivyo sasa hivyo ana kila sababu ya kubadilika. “Kiukweli najiona kabisa naelekea kuzeeka, ule usichana unapotea hivyo ni vyema sasa mambo mengine ya kimjini nikayapa kisogo. Kwenda klabu usiku nimepunguza na kuna siku nitaacha kabisa, nguo za ajabuajabu najifikiria mara mbilimbili,” alisema Kajala.

SERIKALI YAWAKUTANISHA VIJANA KUUNDA KANUNI ZA UENDESHAJI BARAZA LA VIJANA TAIFA.

Image
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw. Eric Shitindi akizungumza na vijana (hawapo pichani) alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.   Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.   Mwezeshaji Bw. Patrick Kipangula (aliyesimama) akitoa mada kwa wadau wa maendeleo ya vijana wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.   Mjumbe    wa maendeleo ya vijana akichangia mada wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.   Wawakilishi kutoka Mamlaka mbalimbali za Serikali, Asasi za kiraia,

Wasira: Nilianza kupigwa picha tangu natoka chooni, nahisi huyu katumwa

Image
Mwanasiasa mkongwe na Waziri wa zamani wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira ameeleza sababu zilimpelekea kugeuka mbongo na kutaka kumgonga na gari mwandishi wa habari aliyekuwa anampiga picha. Wasira ameeleza kuwa alipandishwa hasira na kitendo cha mpiga picha, Michael Samson kumpiga picha nyingi zisizo na idadi huku akimfuata kila anapoenda, punde tu alipotoka msalani. “Nilianza kupigwa picha wakati natoka chooni tukiwa pale Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza. Nikamuuliza yule kijana, ‘hizi picha zote unanipiga ni za nini?’ akananiambia ni za habari. Nikamuuliza picha zote hizo mia ni za habari? Yeye akaendelea tu kunipiga picha,” Wasira ananukuliwa na gazeti la Mwananchi. Wasira alikutana na tukio hilo katika jengo la Mahakama ya Biashara jijini Mwanza baada ya kutoka Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza, alipokuwa akifuatilia rufaa yake ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la Bunda Mjini yaliyompa ushindi Ester Bulaya (Chadema). Mwanasiasa huyo mkongwe alija

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMLILIA MZEE KASSIM MAPILI

Image

MAWAZIRI WAPEWA MWISHO LEO KUJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI, HATI YA UADILIFU

Image
  Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majliwa Majaliwa (kulia) akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki.   Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna. (PICHA ZOTE NA EBENEDICT LIWEN

Vigogo Watatu Wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Wafikishwa Mahakamani

Image
Vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), akiwemo Mtendaji Mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo, wamepandishwa kizimbani, kwa tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 83.5. Mbali na Asteria, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo ya uhujumu uchumi ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa mradi huo, Francis Kugesha na Mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe. Walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana na kusomewa mashitaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage. Walisomewa mashitaka na wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Jackline Nyantori akisaidiwa na Estazia Wilson na Stellah Mafuru. Nyantori alidai kati ya Septemba Mosi na Oktoba Mosi 2013, Kinondoni Dar es Salaam, Asteria, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia serikali hasa

BREAKING NEWZ: Mwanamuziki Mkongwe Kassim Kapili Afariki Dunia

Image
Mwanamuziki mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili akicharaza nyuzi za Gitaa lake chini ya Kundi zima la Mjomba Band . MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili amefariki dunia akiwa chumbani kwake, Tabata jijini Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi (CHAMUDATA) Hassan Msumari, amesema kuwa kifo cha Mapili kimegunduliwa usiku huu baada ya mlango wa chumba chake kuvunjwa. Mlango huo ulivunjwa baada ya Kassim Mapili kutoonekana tangu alipokwenda kutazama mpira wa Arsenal na Barcelona Jumanne usiku. Kwa mujibu wa Msumari, mara mlango ulipovunjwa Kassim Mapili alionekana akiwa ameshafariki akiwa amejifunga taulo, ishara inayoonyesha kuwa aidha alikuwa anakwenda kukoga au ametoka kukoga. Jumatatu jioni Kassim Mapili alishiriki vizuri mazishi ya mwanahabari Fred Mosha makaburi ya Kinondoni ambapo alipewa wasaa wa kuongea machache na kama vile hiyo haitoshi, Mapili aliimba makaburini hapo kuomboleza kifo cha Fred Mosha.

Lulu adaiwa kulipiwa mahari

Image
= Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. Dar es Salaam: Wakati akikanusha vikali taarifa mbaya za kuzushiwa kifo mwishoni mwa wiki iliyopita na watu ambao alisema hajui lengo lao, habari ya heri ni kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani) anaelezwa kuwa kwenye shamrashamra za ndoa baada ya kudaiwa kulipiwa mahari na mfanyabiashara maarufu jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa). Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu, hivi karibuni mrembo huyo alilipiwa mahari hayo kwa siri kwa kuwa mwanaume huyo hakutaka mambo hayo yafike kwenye vyombo vya habari. “Sasa mimi nawapa habari motomoto kuwa Lulu amelipiwa mahari na mwanaume wake wa sasa lakini ishu nzima ilikuwa kwa siri sana,” kilidai chanzo hicho na kuongeza: “Shughuli nzima ilifanyika nyumbani kwa Lulu (Mbezi-Beach, Dar) na sasa kinachoendelea ni taratibu za harusi lakini jamaa (huyo mwanaume) hataki iwe na mbwembwe. Lulu akiwa katika poz

Cement ya Dangote Yaanza Kusambaza Tanzania... Bei ya Mfuko Mmoja wa Cement yatajwa

Image
Kile kiwanda kikubwa cha Africa mashariki na Africa kwa ujumla kwa mara ya kwanza kimeanza kuzalisha kusambaza cement yake tar 21/02/ 2016. Kiwanda hicho ambacho ni tegemeo jipya kwa waakazi wa mikoa kusini Mtwara na Lindi kiliahidi ajira nyingi ya wakaanzi wa mikoa hiyo na watanzania kwa ujumla Cement tayari iko maduka kwa bei nafuu ya sh 13,500 tofauti na cement ya viwanda vingine. Tunawakaribisha wateja wa cement hiyo na wenye magari makubwa kufungua office mkoani Mtwara ili kuongeza ajira za madereva hapa mkoani TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Shuhudia Red Carpet ya Tuzo za Brit jana (Picha)

Image
Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mzuri kwa mastaa kibao wa muziki wa Pop na Hip Hop duniani kutokana na tuzo za dunia za Brit zilizotangazwa katika Ukumbi wa London’s O2 Arena, Uingereza. Nimekuletea picha ‘red carpet’ katika tuzo hizo ambazo zilifunikwa kwa shoo ya nguvu kutoka kwa Adele, Rihanna na Drake.