Posts

Mbinu mpya ya Mastaa kujiuza

Image
Masogange Na Mwandishi wetu, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Imevuja! Siri ya maisha mazuri ya baadhi ya mastaa wa kike Bongo ambao hawafanyi filamu, Bongo Fleva wala kazi yoyote imejulikana huku aibu kubwa ikiwafuata nyuma ya siri hiyo, Risasi Jumamosi limefungasha mzigo wa kutosha! Kwa mujibu wa chanzo chetu kikuu kikizungumza na Risasi Jumamosi, mastaa hao wamekuwa wakitumia njia ya kisasa ambayo ni Mtandao wa Kijamii wa Instagram kupata wanaume wenye fedha ambao hujitokeza na kuwataka kimapenzi, wengi wao wakiwa nje ya nchi. Giggy Money NCHI ZENYE WATEJA WENGI Chanzo hicho ambacho na chenyewe ni staa, kiliendelea kusema kuwa, nchi ambazo mastaa hao wana soko kubwa ni China, Dubai na Afrika Kusini. India ni kwa mbali sana! INAVYOKUWA SASA Chanzo: “Ili tuweze kuonwa na wateja wetu hao, huwa tunatupia kwenye mtandao huo, picha zetu zenye mvuto tukiwa kwenye mapozi ya ‘ki-hasarahasara’, wengine hutupia mpaka picha za nusu utupu ili wanaume wakiwaona wavu...

Talaka ya Jide Mazito Yaibuka!

Image
Mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ na mumewe Gardner G. Habash ‘Captain’. Na Musa Mateja Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Siku chache baada ya staa mwanadada mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ kupewa talaka mahakamani na mumewe Gardner G. Habash ‘Captain’ mazito yameibuka baada ya kubainika uwepo wa hati nyingine ya talaka aliyoitoa Gardner kwa mwanamke mwingine, Risasi limeinasa. Jide Chanzo makini kimepenyeza habari kuwa mbali ya Jide anayetarajia kuibuka na kishindo kikubwa cha mabadiliko ya muziki wake hivi karibuni, Gardner alimpa talaka mahakamani mkewe wa awali aliyefahamika kwa jina la Idda Pius Mkunja, mwaka 2003. “Mwenzangu Gardner anaonekana ndiyo kamchezo kake kumalizia ndoa mahakamani, ukiachana na Jide nimeona hati ya talaka nyingine aliyoitoa kwa Idda ambaye alimuona mwaka 1997,” kilisema chanzo hicho huku kikimpenyezea hati hiyo ya talaka (tazama pichani) mwanahabari wetu. Siku ya ndoa yao Kama hiyo haitoshi, c...

WAZIRI NAPE AONGEZA HAMASA MECHI YA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (kushoto)walipokutana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.( Picha na: Frank Shija,WHUSM) Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Mabeki wa Timu ya Simba wakiokoa mpira wa hatari katika lango lao wakati wa mechi dhidi ya Yanga iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Mechi hiy...

Things To Never Do With Or In Front Of Your Partner

Image
When you officially (and finally!) become a couple, every second of spending time together is bringing you joy and you having the happiest time of your life. Okay, that’s what all of us are dreaming of. Everything is sweet and lovely for the first few months, but… But things become more and more serious, you may even decide to live together, and that’s when disaster starts. Well, actually men undergo the first few months of this “living together” situation much easier than women. We all understand why: we’re sometimes afraid to do things that can surprise or shock our partner (and make him love you less!). There are a lot of exaggerations manifesting themselves in women’s heads. But certain things can really become some kind of turn-offs and start to ruin your relationship. Maybe you didn’t notice doing some of them before. Check the list now! Okay, first of all, even if you feel you’re best friends with your partner, remember, that this “bro stuff” don’t fully work b...

Yanga Jeuri, Simba Kiburi

Image
Wachezaji wa Yanga, Ngoma (kushoto) na Kamusoko (kulia). Waandishi Wetu, Dar es Salaam DAWA ya Jeuri ni Kiburi, Yanga na Simba leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa zinapambana katika mechi ya Ligi Kuu Bara huku nyuma yake kukiwa na vita kubwa. Awali, Simba ilionekana haitafanya lolote katika Ligi Kuu Bara msimu huu, lakini muda mfupi baada ya Jackson Mayanja kupewa kazi ya kocha msaidizi akiichukua timu kutoka kwa Dylan Kerr, raia wa Uingereza, mambo yamebadilika. Chini ya Mayanja raia wa Uganda aliyewahi kuinoa Bunamwaya ya nchini kwake, Simba imefanikiwa kushinda mechi sita mfululizo za ligi kuu na moja ya Kombe la FA dhidi ya Burkina Faso ya Morogoro. Wachezaji wa Ibrahimu Ajibu na Juuko Murshid (kulia) wakishangilia. YANGA JEURI Jeuri ya Yanga ipo zaidi katika fedha, kwanza ilikodi ndege kutoka Dar es Salaam hadi Cuepipe, Mauritius kucheza na Cercle de Joachim katika Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo ilishinda bao 1-0. Ndege hiyohiyo ikaipeleka Yanga Zanzibar Jum...

Barua ya Jack Cliff yazua simanzi upya

Image
Video Queen, Jack Cliff. NA Imelda Mtema, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Ikiwa imekatika miaka miwili tangu alipokamatwa na madawa ya kulevya huko Macau, nchini China, Video Queen, Jack Cliff ameibua simanzi upya baada ya kuandika barua ya wazi kwa Watanzania. Simanzi hiyo iliibuka mwanzoni mwa wiki hii mara baada ya barua hiyo kusomwa redioni na Mtangazaji Millard Ayo ambapo barua hiyo ilieleza kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuwaweka sawa wanaosambaza taarifa za uongo zinazomhusu. …Akiwa katika pozi. Katika barua hiyo, ameweka wazi kwamba anajuta kubeba madawa ya kulevya na mwisho wa siku kujikuta akiwa kwenye mikono ya polisi kitu ambacho hakukitegemea kabisa. Anahuzunika, ila pamoja na hayo yote, ameamua kuwaomba msamaha Watanzania wote kwa kile kilichotokea. “Inasikikitisha, Mungu amsaidie atoke jamani maana kama kujuta ameshajuta vya kutosha,” alisema John Jimy, mkazi wa Mwenge Dar. Huku taarifa zikiwa zimetolewa katika vyombo vya habari kuhusu uhusiano wa mpe...

WAZIRI MKUU ATINGA BANDARI YA TANGA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majliwa akizungumza na Mkuu wa bandari ya Tanga, Henry Arika (kulia kwake ) na Mhandisi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Felix Mahangwa ( kulia wakati alipotembelea bandari ya Tanga Februari 19, 2017.  Waziri Mkuu, Kssim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Bandari ya Tanga , Henry Arika (kulia kwake) kukagua bandari hiyo Februari 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Matishari matatu ambayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka apewe maelezo kwa maandishi kuwa ni nani aliyeidhinisha mchakato wa manunuzi yake bila kuzingatia viwango na ubora uliokusudiwa na serikali. mheshimiwa Majaliwa alifanya ziara katika bandari ya Tanga Februari 19, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) ……………………………………… WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Februari 19, 2016) amekagua bandari ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port Master), Bw. Henry Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya tishari ifikapo kesho (Jumamosi)...

Rais Museveni anaongoza matokeo ya awali Uganda

Image
Rais Museveni akitumbukiza kura yake katika kisanduku. MATOKEO ya awali ya Uchaguzi Mkuu nchini Uganda yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (EC), Eng. Badru Kiggundu leo asubuhi yanaonyesha Rais Museveni anaongoza kwa kupata kura 1,362,961 sawa na asilimia 61.75 huku mpinzani wake wa karibu Kizza Besigye akifuatia kwa kupata kura 738,628 sawa na asilimia 33.47 na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Amama Mbabazi mpaka sasa yeye ana kura 41,291 sawa na asilimia 1.87. Kizza Besigye  naye akitumbukiza kura yake kwenye kisanduku. Matokeo hayo ni kutoka katika vituo 6,448 kati ya 28,010 vilivyotumika kupigia kura. Jumla ya watu 15,277,198 walijiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu.

Mama amcharanga viwembe mwanaye!

Image
Majeraha aliyoyapata baada ya kujeruhiwa na viwembe. Stori: Joseph Ngilisho, Ijumaa Arusha: Ukatili wa watoto haukubaliki! Mama mzazi aliyetajwa kwa jina moja la Anna, mkazi wa Oysterbay maeneo ya Unga-Limited jijini hapa anadaiwa kumcharanga kwa viwembe mwanaye wa kumzaa mwenye umri wa miaka kumi anayesoma shule ya msingi (jina la mtoto na shule yanahifadhiwa). Tukio hilo la kusikitisha lilijiri mapema wiki hii nyumbani kwa mama huyo maeneo ya Oysterbay hivyo kumlazimu Diwani wa Kata ya Themi, Melance Kinabo kushirikiana na polisi kumkamata mzazi huyo kutokana na kitendo alichomfanyia mwanaye na kumwachia majeraha makubwa. Kwa mujibu wa mshuhuda wa tukio hilo, mama huyo anayefanya kazi kwenye moja ya viwanda vilivyopo Unga-Limited, anadaiwa kumfanyia mwanaye ukatili huo huku kisa kikielezwa ni kitendo cha mtoto huyo kukataa kuchota maji. Ilielezwa kuwa, mtoto huyo kwa sasa anapatiwa matibabu kwenye zahanati moja iliyopo Unga-Limited jijini hapa kufuatia majeraha ya ...

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 19.02.2016

Image