Posts

MAGAZETI YA LEO IJUMAA

Image
                                             

DIAMOND PLATINUMS ZARI THE BOSS LADY WALA SHAVU VODACOM

Image
 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(wapili kushoto) Balozi wa Vodacom Tanzania, Nasibu Abdul (Diamond Platinum) Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Rosalynn Mworia(kulia) na Zarina Hassan(kushoto)wakionesha mabango yenye ujumbe wa jinsi ya kujiunga na Promosheni ya “Ongea Deilee”, wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vodacom.  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao( kushoto) na Zarina Hassan(Kulia) wakionyeshwa tangazo la promosheni ya”Ongea Deilee” kwenye simu lililofanywa na msaanii wa muziki wakizazi kipya Abdul Nasibu”Diamond Platinum”( katikati) wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Promosheni hiyo itawawezesha wateja wa mtandao huo kuongea kwa muda wa saa 1 bure kila siku pindi wakiongea jumla ya dakika 10 Vodacom kwenda Vod

BREAKING NEWS : MOTO NWA MAGUFULI WATUA KINONDONI,VIGOGO WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Image
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kinondoni, tarehe 02/02/2016 imewafikisha washitakiwa wafuatao mahakamani:-Bw.Bryceson Kajigiri Mwangoma mwenye umri wa miaka 54, Bw.Abel Sebabil Slaa mwenye umri wa miaka 44 na Bw.Bernard Thomas Mkude mwenye umri wa miaka 42 kwa kuiibia Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni  Tsh.33,681,780. Washitakiwa hawa Bw.Mwangoma na Bw.Slaa wakiwa Maafisa watendaji wa Kata ya Kimara kwa vipindi tofauti, na Bw.Mkude akiwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kimara Baruti walitenda makosa kinyume na kifungu cha 31, 22, 28 (1) 3 vya sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 pamoja na kifungu cha 258, 270 vya sheria ya Kanuni za Adhabu. Washitakiwa wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya na kujipatia manufaa kwa kufanya wizi wa fedha hizo zilizokua zimewekwa na Wananchi katika akaunti ya Urasimishaji Ardhi kata ya Kimara iliyopo benki ya Wananchi wa Dar – es- Salaam (DCB) tawi la Magomeni kwa ajili ya kupimiwa maeneo y

Baa za Uwanjani Legho Zavunjwa

Image
Mwanadada akiwa anaangalia vitu alivyofanikiwa kuviokoa. Katapila likiendelea na kazi yake ya kubomoa . Watu mbalimbali wakiwa kwenye vikundi wakijadili tukio hilo. Eneo lililobomolewa. Nyumba hizi mbili baadaye nazo zikabomolewa. BAADHI ya baa zilizopo katika viwanja vya Legho, Ubungo jijini Dar, leo zimevunjwa kufuatia agizo la mahakama kwa kile kilichodaiwa wamiliki walivamia eneo ambalo siyo lao. Akizungumza na mwandishi wetu, dalali wa mahakama kutoka katika kampuni ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd, Elieza Mbwambo, alisema mmiliki halali  wa eneo hilo ni Dar Cool Makers Limited ambaye baada ya  kuvamiwa eneo lake alifungua kesi mahakamani mwaka 1993 ambapo iliendelea mpaka ilipofikia leo. Wavamizi wa eneo hilo ambao ni John Ondoro Chacha, Jumuiya ya Wazazi CCM na mtu mwingine mmoja baada ya kuona mmiliki halali amepeleka kesi mahakamani nao wakaenda kuweka zuio ambapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamuru eneo hilo lirudi kwa mmliki halali ambapo wavamiz

Breaking News: Wachimbaji wafukiwa na kifusi, Chunya-Mbeya

Image
Hali ya taharuki kwenye eneo la tukio Tinga tinga likiendelea na juhudi za uokoaji hivi sasa. Taarifa zilizotufikia hivi punde: Wachimbaji kadhaa wa migodi (idadi yao haijafahamika) hivi punde wamefukiwa na kifusi cha udongo katika Kijiji cha Sangambi kilichopo Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya hivi sasa, Juhudi za kuwaokoa bado zinaendelea muda huu. Endelea kufuatilia habari zetu ili kufahamu kitakachojiri kuhusu tukio hilo.

BREAKING NEWZ:Ukawa Yashinda Umeya Kinondoni

Image
Hali ilivyokuwa kwenye kikao hicho cha uchaguzi wa Meya wa Kinondoni na naibu wake kilichofanyika katika Ofisi za Manispaa ya Kinondoni. Mbunge wa Jimbo la Kibamba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika (katikati) akishiriki kikao hicho. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dk.Tulia  Ackson (katikati) akiwa amehudhuria mkutano huo wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni. Wajumbe wa kikao hicho wakishiriki kupiga kura za kumtafuta Naibu Meya. Zoezi la kupiga kura likiendelea. Zoezi la kuweka kura kwenye sanduku la kupigia kura likifanyika. Wajumbe walioshiriki kupiga kura wa upande wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakishangilia baada ya washindi kutangazwa. Kutoka kushoto ni Meya Mteule wa Kinondoni kupitia Chama Cha Demokrosia na Maendeleo (Chadema), Boniphace Jacob, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumnjuri na mwenyekiti wa usimamizi wa huo, Celestine Onditi. Meya Mteule wa Manispaa